Maharage Ya Sosi Ya Mchuzi Na Nazi

Maharage Ya Sosi Ya Mchuzi Na Nazi

 

  

 

Vipimo 

 

Maharage -  3 Vikombe 

Tui la nazi zito - 1½ kikombe 

Kitunguu - 1 kikubwa 

Nyanya -  2 au tatu

Kitunguu saumu (thomu/galic) iliyosagwa - 1 kijiko cha supu  

Bizari ya mchuzi - 1 kijiko cha chai

Bizari ya manjano - robo kijiko

Pilipili mbichi -  3 

Chumvi -  Kiasi  

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika   

  1. Roweka maharage, kisha chemsha maharage  hadi yawive yabakie na supu yake kidogo
  2. Katakata kitunguu, nyanya,  na thomu
  3. Kaanga kitunguu kidogo kisha tia thomu, nyanya,  kisha kaanga,
  4. Tia bizari ya mchuzi na ya njano kaanga kidogo. 
  5. Tia tui la nazi na acha kidogo tu katika moto. 
  6. Weka chumvi kiasi na koroga iliuonje, kisha tupia pilipili mbichi, mimina katika chombo yakiwa tayari kuliwa 

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

  

 

 

Share