Zingatio: Vitu Vya Duniani Vinapungua Ladha, Pepo Haipo Hivyo

 

Zingatio: Vitu Vya Duniani Vinapungua Ladha, Jannah (Pepo) Haipo Hivyo

 

 Naaswir Haamid

 

 

Alhidaaya.com

 

 

Tafuta riziki ya halali uitie tonge kinywani, mwishowe itayeyushwa na kutolewa tumboni. Jenga nyumba nzuri ya ghorofa uzipendazo, mwishowe utahitaji nyumba iliyojengwa kwa lulu. Jaza fanicha ndani ya nyumba yako, mwishowe utataka kuzibadili zote kwani machoni mwako zimechoka kuangaliwa. Nunua gari iliyo brand new (mpya) uipendayo, siku chache zinaingia nyengine mpya, nawe wahitaji.

 

Juu ya raha zote hizi za dunia, ni matajiri wangapi waliohodhi kila kitu wamejidhulumu nafsi zao kwa kujitia vitanzi? Ni matajiri wangapi ambao wanakosa kupata usingizi usiku? Hio sio hali waliyokuwa nayo Swahaba za Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), ambao walipata kichache wakakinai, na walipopata kingi wakikitumia katika njia ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa).

 

Hiyo ndio ladha ya dunia ambayo inapungua na kumalizika, inakosa ladha kwa ulimi, inakosa nuru katika macho na inakwisha muda kwenye nafsi. Kutwa roho ya mwanaadamu ni yenye kutamani na kutapatapa kama mfa maji. Iwapo hali ndio hiyo, kumbuka maneno ya wahenga: 

 

"بانوا بانوا وما سكنوا, ساروا ساروا وما رجعوا"

Wamejenga na kujenga bila ya kukaa, Wamekwenda na kwenda bila ya kurejea

 

 

Juu ya raha zote hizi za dunia, ni matajiri wangapi waliohodhi kila kitu wamejidhulumu nafsi zao kwa kujitia vitanzi? Ni matajiri wangapi ambao wanakosa kupata usingizi usiku? Hio sio hali waliyokuwa nayo Swahaba za Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), ambao walipata kichache wakakinai, na walipopata kingi wakikitumia katika njia ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa).

 

Dunia ndugu zangu ni ya kupita tu, maisha yapo Aakhirah huko. Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Ametuandalia mambo mazuri ambayo macho hayajapata kuona, wala sikio kusikia, wala moyo kuwahi kufikiria na unachotaka wakipata humo.

 

Kila kitu kina expiry date yake, na kwa hakika hata roho ina expiry date yake, seuze nyumba, gari, fanicha na mengineo. Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Ameisifu Jannah kwamba ni ya kifakhari kuliko chochote duniani, humo watu wake wataishi milele, daima wa dawaam: 

 

إِنَّ أَصْحَابَ الْجَنَّةِ الْيَوْمَ فِي شُغُلٍ فَاكِهُونَ ﴿٥٥﴾ هُمْ وَأَزْوَاجُهُمْ فِي ظِلَالٍ عَلَى الْأَرَائِكِ مُتَّكِئُونَ ﴿٥٦﴾ لَهُمْ فِيهَا فَاكِهَةٌ وَلَهُم مَّا يَدَّعُونَ ﴿٥٧﴾ سَلَامٌ قَوْلًا مِّن رَّبٍّ رَّحِيمٍ ﴿٥٨﴾

Hakika watu wa Jannah leo wamo katika kushughulika wakifurahi. Wao na wake zao, wakiwa katika vivuli, juu ya makochi ya fakhari wakiegemea. Watapata humo kila aina ya matunda, na watapata wanavyoomba. Salaamun! Kauli kutoka kwa Rabb Mwenye kurehemu. [Yaasiyn: 55-58].

 

Naye Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameisifu Jannah kwa maneno yafuatayo:

 

"Hakika wakaazi wa Jannah (Peponi) watakula na kunywa lakini hawatakuwa wanatema, Wala hawendi haja ndogo au kubwa, Wala kutokuwa na uchafu puani. Waliuliza Swahaba: kitakuwaje chakula? Alijibu Nabiy (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) kitakuwa kitamu kama utamu wa miski na watakuwa wamejazwa na Tasbihi na Tahmidi kama walivyojaaliwa kupumua."

 

[Imesimuliwa na Jaabir (Radhwiya Allaahu ‘Anhu) na kupokelewa na Muslim].

 

Enyi makundi ya Waislamu, tusipumbazwe na lahwa za dunia tukasahau neema alizotuahidi Rabb wetu Mlezi. Hivyo, tujihimize kumuabudu Yeye bila ya kumshirikisha kwa jambo lolote, insha Allaah tutayakuta yote tuliyoahidiwa, anza leo usisubiri kesho.

 

 

Share