Amesomewa Kisomo Akatokea Mtu Inayesemekana Ni Jini Kuja Kumbainishia Mbaya Wake, Je, Inawezekana?

 

Amesomewa Kisomo Akatokea Mtu Inayesemekana

Ni Jini Kuja Kumbainishia Mbaya Wake, Je, Inawezekana?

 

Alhidaaya.com

 

SWALI:

 

Aslam alykum warhmatullahi wabarakatu,ahsanteni sana kwa kunijbu email yangu, In shaa Allaah mola atakupeni kila la kheri, sasa mimi meondoka kwenye nyumba mpya, mama yangu ndio yupo,in shaa Allaah kwa uwezo wa allha nitarudi mwezi wa saba mola akinijaalia,msm yenu nitasoma hapa nilipo, na nitampelekea yeye mama yangu pia,namshukuru mola ndie ninae mtengeme,hofu bado nawasiwasi ninao,kwa uwezo wake utaondoka,sasa baada ya kusomwa na dua na kur an, siku kidongo kupita alikuja mtu mwanamme,akasema nilionyeshwa nyumba yako na mkweo fulani, na kanambia nifanye ubaya, watu tofauti  wamesema huyo sio mtu ni sheitani,kajigeuza kua mtu, Mola anakubainishia nani mbaya wako, baadaya ya kusomwa na watu tofauti ndani ya nyumba, ndio kaja, sasa je inawezekana kua ni sheitani,na yule mtu hatumjui, na kama kanambia mkweo ndio mbaya wako nifanye nini?   

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho

 

Hayo ni mambo ya kubabaishwa na kuchezewa akili yako na kutiwa wasiwasi ili uamini hayo unayoambiwa na hao wajanja. Mambo kama hayo ya kusomewa na kutabiriwa mambo yako, si mambo ya Kiislamu na yanaingia katia uchawi na ulozi na kumsukuma mtu katika ushirikina. Usiwaamini watu kama hao, maana kuna wengine wanakuwa tayari wameshaulizia habari zako na kukufahamu vyema, kisha wanapokujia na kukueleza mambo yako fulani fulani, wewe unaweza kulaghaika na kuwaamini kwa sababu umeona kuwa wanajua ya ndani na hali wewe huwafahamu. Hivyo tahadhari na hizo mbinu zinazofanywa na matapeli kama hao wenye lengo la kukufanya uamini hayo wanayokuambia, na baada ya hapo ujenge wasiwasi na uwe unawategemea wao kukulinda na kukutatulia matatizo yako hayo ambayo hukuwa nayo bali wamekupandikizia wao wasiwasi huo katika nafsi yako. Mwishowe utakuja kuingia katika ushirikina na kuacha kumtegemea Allaah na kuelekea kuwategemea hao matapeli na washirikina.

 

Lakini hakuna la kufanya upande wako ila tu kujikinga kwa kusoma Qur-aan, kuomba Du'aa, kuamka usiku kuswali tahajjud, na kusoma nyiradi za kinga ambazo tumeshakupa kila siku bila ya kuacha. Ukifanya hivyo utakuwa huna shaka tena kwani itakuwa umeshamuelekea Rabb Muumba Mwenye uwezo wa kila jambo Akuhifadhi na kila shari.

 

Na hasa usiache kusoma nyiradi za asubuhi na jioni zinazopatikana katika kiungo kifuatacho pamoja na nyinginezo:

 

027-Hiswnul-Muslim: Nyiradi Za Asubuhi Na Jioni

 

028-Hiswnul-Muslim: Nyiradi Za Kulala

 

128-Hiswnul-Muslim: Du’aa Ya Kuzuia Vitimbi Vya Mashaytwaan

 

 

Nasaha zetu za dhati na za muhimu kabisa ni kwamba, usije nawe ukaingia katika shirki na kufru hiyo kwa kwenda kwa waganga na kufanya nawe kama wafanyao hao majahili. Kufanya hivyo utaingia katika ghadhabu za Mola wako na hutakuwa na mafanikio ila khasara duniani na Akhera. Unachopasa ni kubaki mbali na kufru hizo usalimike na dini yako na upate Radhi za Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa).

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share