Kumlipa Anayekufanyia Ruqyah Inapasa Na Hali Mwenye Kuponyesha Ni Allaah?

 

Kumlipa Anayekufanyia Ruqyah Inapasa Na Hali Mwenye Kuponyesha Ni Allaah?

 

Alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Assalaam aleykum,

Nimepitia jambo hili katika mafunzo yenu:

"Kuna ushahidi unaothibitisha kuwa malipo ya ruqya yatolewe iwapo mgonjwa amepona kabisa ugonjwa wake. Kwa maneno ya Abdul Barr '...malipo ya kitu ambacho hakileti tija yoyote ni dhuluma na haramu" [At-Tamhiid]." 

http://www.alhidaaya.com/sw/node/916

 

Naomba mtusaidie ushahidi huu umetoka kwa nani. Nilivyofaham ni kua tukifanya hivi tutakua tunamlipa msomaji Ruqya kwa kuweza kumponesha mgonjwa. Asipopoa hatumlipi kwa kua ruq-ya yake haijaleta tija. Ukweli ni kwamba anaeponesha ni Allah mtakatifu; ile ruqya ni sababu tu. Kupona na kutopona iko ndani ya Qudra ya Allaah. Kumlipa baada na kumlipa qabla hamna tofauti kwani si yeye anaeponesha. Kinyume na hivo tutakua tumekiuka sharti la 3 la ruqya. 

 http://www.alhidaaya.com/sw/node/915

 

Kama nimefaham vibaya naomba kukosolewa. 

 

Wabillahi-ttawfiyq.

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho

 

Tuna furaha kuwa umeisoma mada hiyo vizuri na kuja na maswali mazuri muhimu kama hayo.Tunapenda kukujulisha kuwa msimamo ambao unamili zaidi kwenye usawa ni wa kutopokea malipo kwa kazi hiyo.

 

Ni kweli Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Ndiye Mponeshaji na Mhuishaji, lakini haina maana kuwa kulipia matibabu ni haraam na kuwa daktari ndiye mponeshaji, la! Daktari au mtu kwenda Hospitali kutibiwa, ni sababu na ni njia ambazo zinakubalika kisheria japokuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Ndiye Mpangaji wa aponaye na asiyepona. Hivyo, mtu kutibiwa, haina maana kuwa atakayemtibu ndiye mponeshaji na haina maana mtu asilipie gharama za matibabu kwa sababu tu hajapona. Na ndiyo maana tunaona pamoja na rai hiyo ya ‘Abdul-Barr hapo juu, lakini msimamo sahihi ni kuwa ikiwa kuna malipo basi yalipwe kwa kazi hiyo ikiwa mtu atapona au haponi kwani hiyo ni ajira na ajira ina nidhamu zake maadam ajira hiyo inakubalika kisheria.

 

Lakini msimamo sahihi ni kutopokelewa ujira katika Ruqyah na mwenye kuifanya na mwenye kufanyiwa kutotoa. Na ni bora zaidi mtu kama ana uwezo ajifanyie mwenyewe, na akiwa hawezi ima kwa kutokujua au kuzidiwa na ugonjwa wake, basi apatikane mtu mwaminifu mwenye ujuzi asiyechukua gharama ambaye atamfanyia Ruqyah hiyo.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share