Uwajibu Wa Kuweka Sutrah (Kizuizi) Katika Swalaah

 

SWALI: 

salamun alaykum

habari za kazi zenu?

mm nilikua nashangazwa na pale mlipomjibu huyu mtu ambae alietaka kujua kwa nini sala ya mtu inakatika ikiwa mtu atapita mbele yake? Sasa nami nauliza hivi kwani kuna maana gani kuweka kitu mbele ya mtu anaesali ili sala ya mtu mwengine isikatike na hivi ndio mtume alivyokua akifanya au sisi tu ndio tufanye hivyo naomba japo hadithi moja inoonyesha kama mtume aliweka kitu mbele yake.

 


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kuweka sutrah katika Swalah.

Hakika sisi hatufanyi mambo isipokuwa yawe na dalili kutoka kwa Qur-aan au kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Ikiwa tunapata dalili tunafanya, na ikiwa hakuna basi tunakuwa mbali na jambo hilo. Tuzingatie maneno ya Allaah Aliyetukuka pale Aliposema:

Na anachokupeni Mtume chukueni, na anachokukatazeni jiepusheni nacho. Na mcheni Allaah. Hakika Allaah ni Mkali wa kuadhibu” (Al-Hashr 59: 7).

Kisha Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametuagizia:

Swalini kama mlivyoniona nikiswali” (Al-Bukhaariy).

 

Sasa tukiangazia swali lako utakuta hakuna utata wowote kwani zipo Hadiyth nyingi za Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) zinazotuelezea kuhusu suala hilo la sutrah. Hizi hapa chini ni baadhi yake:

 

1.     Imepokewa na Abu Juhaym bin al-Haarith (Radhiya Allaahu ‘anhu) kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Lau angejua mwenye kupita mbele ya mwenye kuswali madhambi anayopata, ingekuwa bora kwake kusimama (asipite mbele yake) arobaini kuliko kupita mbele yake” (Al-Bukhaariy na Muslim). Na katika riwaya ya al-Bazzaar inasema: “Miaka arobaini”. Hadiyth hii inatuonyesha dhambi kwa mtu kupita mbele ya mwenye kuswali.

 

 

2.     Imepokewa na Sabrah bin Ma‘bad al-Juhaniy (Radhiya Allaahu ‘anhu) kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Mmoja wenu aweke sutrah katika Swalah japokuwa ni mshale” (al-Haakim). Na maana yake ni kuwa kinachotakiwa ni kuweka kitu ili mwenye kupita ajue kuwa unaswali.

 

 

3.     Imepokewa na Abu Dharr al-Ghifaariyy (Radhiya Allaahu ‘anhu) kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Swalah ya mmoja wenu Muislamu inakatika – ikiwa hakuna mbele yake mfano wa shogi (la mnyama)” (Muslim). Na Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘anhu) naye amepokea mfano wa hayo.

 

 

4.     Na Ma-Imaam Abu Daawuud na an-Nasaaiy wamepokea mfano wa Hadiyth hiyo ya juu (namba 3) kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhuma)

 

5.     Imepokewa na Abu Sa‘iyd al-Khudriy (Radhiya Allaahu ‘anhu) kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Akiswali mmoja wenu, akiwa ameweka sutrah (mbele yake) kutokana na watu, mmoja (miongoni mwa watu) akataka kupita mbele yake, basi na amzuilie. Akiwa mtu huyo atakataa basi amzuilie kwa kutumia nguvu, kwani yeye ni Shaytwaan” (Al-Bukhaariy na Muslim). Na katika riwaya nyingine: “Kwani yuko pamoja naye Shaytwaan”.

 

 

6.     Na Abu Juhayfah (Radhiya Allaahu ‘anhu) amesema kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliswali Swalah ya Dhuhr na Aswr rakaa mbili mbili ilihali ameweka mbele yake fimbo yenye kichwa kama mkuki kama sutrah (al-Bukhaariy).

 

7.     Ibn ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhuma) alikuwa akimweka kipando chake mbele yake kama sutrah. (Imepokewa na Maalik). Katika riwaya ya Al-Bukhaariy akasema Ibn ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhuma): “Nimemuona Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akifanya hivyo”.

 

Tunatumai kuwa Hadiyth hizi zitatosha kabisa kuonyesha umuhimu wa mtu kuweka sutrah mbele yake wakati anaposwali.

 

Na Allaah Anajua zaidika kitu ili mwenye kupita ajue kuwa a bora kwake kusimama (asipite mbele yake) arobaini

 

 

Share