Kuswali Nyuma Ya Shia Na Kufuata Nyakati Zao Za Kufuturu

  

SWALI: 

Assalamu alaikum warahmatullahi wabarakatu.

Ndugu waislamu, nina maswala mawili ninataka kuwauliza.  Suala la kwanza ni kuhusu kuswalishwa na mtu aliye mshi'a. Je, swala yangu inafaa?

Na suala la pili ni kuhusu mshi'a huyu huyu ambaye alinialika nyumbani kwake kufuturu an familia yake na kawaida sisi huku Canada tuna nyakati za kufungua (saumu)na wakati wetu wakufunguwa ni 7:34 sunset lakini huyu bwana akaniambiya kuna tafauti ya sunset na maghrib kwa hivyo haturuhusiwi kufunguwa wakati huo mpaka baada ya dakika kumi tusubiri ndiyo maghribi itakuwa imeshaingiya.  Na akanitoleya kalenda yao iliyo na swafu moja ya sema SUNSET 7:34 na swafu ya pili insema MAGHRIB 7:44. Ninge omba jawabu kuhusu haya masuali.

Shukran jaziran  

 


 

JIBU: 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho

Maulamaa walishaulizwa swali kama hilo mara kwa mara, na kwa kifupi tunakunukulia jibu la mmoja katika wanachuoni wakubwa kuhusu hilo. Anasema Shaykh 'Abdul-'Aziyz bin Baaz alipoulizwa hukumu ya kuswali nyuma ya Imam Mshia, alijibu: "Mtu asiswali nyuma ya Imaam yeyote ambaye anajulikana kwa kuwatukuza kwake Ahlul-Bayt (Watu wa nyumba ya Mtume)..." Fataawa al-Shaykh Ibn Baaz, mj. 12, uk . 107

Makusudio ya Shaykh Ibn Baaz hapo kuwa wanatukuza Ahlul-Bayt,  ni kwa sababu Mashia hujulikana kwa sifa ya kuwatukuza ma-Imaam wao 12 na kuamini kuwa wao ni bora kuliko hata Mitume na Malaika. Na kuwa wao wanajua hata Ghaibu!! Vilevile Mashia wanaamini kuwa Qur-aan haijakamilika; ina upungufu mkubwa! Itikadi hizo tu zinatosha kumfanya mtu kafiri, ingawa Mashia wana itikadi zaidi ya hizo kama kuwakufurisha na kuwatukana Maswahaba watukufu wakiwemo wake za Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam); mama wa waumini 'Aaishah na mama wa waumini Hafswah (Radhiya Allaahu 'anhuma) pamoja na baba zao ambao ni Makhalifa waongofu; Abu Bakr na 'Umar (Radhiya Allaahu 'anhuma). Vitabu vingi vya kishia na tovuti (websites) zao zinapatikana ndani yake kuwakufurisha Maswahaba kuwalaani na hata ukitaka utapata mawaidha na video za Maulamaa wao zenye kuwatukana waziwazi Maswahaba na wake za Mtume!

Soma viungo hapa chini ujue zaidi kuhusu itikadi zao:

Itikadi Za Ushia Kutoka Katika Vitabu Vyao - 1 Qur-aan (Imani Yao Juu Ya Qur-aan) 

Itikadi Za Ushia Kutoka Katika Vitabu Vyao - 2 (Itikadi Zao Kuhusu Allaah) 

Itikadi Za Ushia Kutoka Katika Vitabu Vyao - 3 (Ndoa Ya Muda Au Uzinifu Uliohalalishwa) 

Maoni Ya Maimaam Kuhusu Mashia  

Pia kumruhusu Mshia kukuswalisha wewe au kuwaswalisha Waislam msikitini au sehemu ya watu wengi, kuna madhara makubwa sana kwani kutawapelekea wale wasiojua wakaona kuwa huyo mwenye kuswalisha ndiye mbora na hivyo kumwamini na kutomtilia shaka na hivyo kupelekea yeye huyo kujipenyeza katika jamii na kuwaingiza Waislam kwenye 'Aqiydah yake hiyo potofu na mwisho watu kuondoshwa katika Uislam wao safi na kutumbukizwa kwenye upotofu wao. 

Kuhusu kuchelewa kufuturu hiyo pia ni ufahamu usio sahihi wanaoutumia kutokana na kutokufahamu vizuri Aayah na Hadiyth au kuzipindua kwa matamanio ya nafsi zao potofu ili ziendane na wanavyotaka wao.

Imependekezwa mtu kukimbilia kufutari wakati wa kuchwa kwa jua. Sahl Ibn Sa'ad (Radhiya Allaahu 'anhu), ameripoti kuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Watu wataendelea kuwa katika kheri madhali watakuwa wanaharakisha kufutari" [Al-Bukhaariy na Muslim]

Maelezo yake yameelezewa kirefu katika Swali lifuatalo:  

Inafaa Kufuturu Wakati Wekundu Bado Haujamalizika?  

Inakupasa usome vizuri kuhusu 'Aqiydah zao ili utambue hatari ya kuandamana na marafiki wenye 'Aqiydah potofu kwani wengi wao wana hima kubwa ya kueneza dini yao na kwa njama zao huenda akakuathiri usipotahadhari. Na fahamu kuwa hao ni wajanja sana, wanaweza kuwa na wewe kwa miezi na miaka bila wewe kujua madhara yao kwa sababu huwa wanatumia itikadi yao ya 'Taqiyyah' ambayo ni kuficha kile wanachokiamini, au kwa maana nyingine ni 'Unafiki'. Mwanzoni mwa uhusiano wake na wako, hatokuonyesha chuki zao juu ya Maswahaba, na hata anaweza kumuombea radhi Abu Bakr na 'Umar wanapotajwa, na akawa hata anawataja Maswahaba kwa uzuri., na pia akakusisitizia undugu wa Kiislam na kukukinaisha kuwa nyinyi wote mnatamka shahada na mnakwenda Hija pamoja. Lakini kadiri masiku yanavyosogea na ukawa karibu naye zaidi, basi polepole utaanza kusikia lugha yake inabadilika, chuki zadhihirika kwa wasio Mashia, Maswahaba wataanzwa kukanyagwa, Abu Hurayrah utaambiwa alikuwa muongo anatunga Hadiyth... 'Umar alisababisha kifo cha Faatwimah... Abu Bakr alimnyang'anya Faatwimah urithi wa shamba aliloachiwa na Mtume... Utasikia mama 'Aaishah akitukanwa kuwa hakuwa muaminifu kwa Mtume (Allaah Atulinde na madai machafu kama hayo)... na utasikia mengi mengi machafu kutoka kwao.

Jambo la msingi la kujiuliza,  (ikiwa Shia anadai yeye ni Muislam) wapi umeona Muislam anapigania kumtoa Muislam mwengine kwenye Uislam wake na kumuingiza kwenye Uislam mwengine!? Yaani kuwa Shia, wale wote wasio Shia hawana Dini!! Yaani Masunni (Ahlus Sunnah wal Jama'ah) na wengine hawawezi kuwa Waislam hadi wawe ni Shia na waamini maimamu wao 12. Asiyewaamini maimamu 12 kwao si Muislam na hawezi kupata pepo.

Pia fahamu kuwa wao ni watu wajanja sana na wenye subira kwa yale wanayoyataka na kuyapigania, kwani watakwenda na wewe kwa utaratibu na kukubalia kila jambo hadi wewe ukishawaamini kikamilifu, basi hukutia mikononi na kuanza kukutupia sumu moja baada ya nyingine hadi unaleweshwa na sumu hizo na hata ukitahamaki basi ushakuwa Shia!! Mwanzo, utajikuta huwachukii, na ukisikia mtu anataja maovu yao, basi utajikuta wewe ndio wa mwanzo kuwatetea na kudai kuwa ni Waislam na wanatamka shahada!! Kisha, polepole utaanza kutetea 'Aqiydah zao moja baada ya moja na hadi mwishowe utakuwa huchukii kuitwa Shia au kufananishwa nao! Haya ni kwa mujibu wa uzoefu wa yale yanayojulikana kwa wale walioingizwa kwenye Ushia.

Tunakutahadharisha sana, uepukane na huyo mtu haraka na jitenge naye. 

Pia ingia katika viungo vifuatavyo usome yote yanayohusu wao na pia tunakuwekea viungo vya mawaidha usikilize kwa manufaa yako ya dunia na Aakhirah. 

Makala: 

"Mimi Ni Mji Wa Elimu Na 'Ali Ni Mlango Wake"

Qur-aan Na Uimamu Wa Mashia

Mashia (Maraafidhah) Na Uharibifu Wa Qur-aan

Mashia Ithna ‘Ashariyah (Wenye Kufuata Maimamu Wao Kumi Na Mbili) Na Hadhi Ya Maimamu Wao

Shida Wanazopata Masunni Huko Iran

Wito Kwa Mashia Wenye Akili

Ukweli Juu Ya Al-Kaafiy (Kitabu Cha Hadiyth Cha Kutegemewa Cha Mashia)

Wanakufurisha Ahlus Sunnah Na Waislamu Wote Wasiokubali Maimaam Wao

Ijue Itikadi Ya Shia Ithnaa-'Ashariyah (Ithnasheri)

 

Mawaidha:

USHIA NA MASHIA

Ni vizuri umpe da'wah rafiki yako huyo kwani kufanya hivyo huenda akapokea da'wah yako na akapokea nasaha akapata uongofu, na hapo ukaweze kuendeleza urafiki naye bila ya shaka.  

 Pia chapisha makala ifuatayo umpe asome.   

Nasaha Kwa Kila Shia

Na Allaah Anajua zaidi  

 

  

Share