Mume Kamtamkia Mkewe Talaka Kisha Akataka Kumrejea Katika Eda, Mwanamke Anayo Haki Kukataa Kurudiana Na Mumewe?

SWALI:

 

Mimi swali langu linahusu talaka. Je! kama mume kamtamukia talaka moja mkewe halafu katikati ya eda yule mume akamtamkia mkewe kwamba nimekurejea na mke hayuko radhi je! bado ni mkewe kwasababu ametamka hivo au mwanamke nae ana haki ya kukubali au kukataa.naomba mnitolee na ushahidi kwenye kuran na hadithi asanteni

 


 

 

JIBU:

 

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho

.

Shukrani zetu za dhati kwa swali hilo kuhusu mume kutoa talaka na kabla ya kumalizika kwa eda kutaka kumrejea mkewe.

 

Ama kuhusu suala hili tayari Uislamu umetupatia uongozi na suluhisho kuwa mume akitaka kumrudia katika eda anaweza bila nikaah mpya kwani hakika bado wao ni mume na mke.

 

Kile ambacho anaweza kufanya mke ikiwa anaona mumewe ana makosa ni kujaribu kuzungumza naye ili ajirekebishe kuhusu hayo. Ikiwa hakufanikiwa basi inabidia aitishe kikao baina yake, mumewe, wawakilishi wake na wa mumewe ili kujadili mashtaka hayo yake.

 

 

 

((وَإِنْ خِفْتُمْ شِقَاقَ بَيْنِهِمَا فَابْعَثُواْ حَكَمًا مِّنْ أَهْلِهِ وَحَكَمًا مِّنْ أَهْلِهَا إِن يُرِيدَا إِصْلاَحًا يُوَفِّقِ اللّهُ بَيْنَهُمَا إِنَّ اللّهَ كَانَ عَلِيمًا خَبِيرًا))

 

 

 

((Na mkichelea kutakuwapo mfarakano baina ya mke na mume basi pelekeni muamuzi kutokana na jamaa za mume, na muamuzi kutokana na jamaa za mke. Wakitaka mapatano Allaah Atawawezesha. Hakika Alllaah ni Mjuzi Mwenye khabari))  [An-Nisaa: 35]

 

 

 

 

Ikiwa anaona hakuna suluhisho basi inabidi aende kwa Qaadhi kutafuta ufumbuzi wa yanayomkumba.

 

Tunawaombea kila la kheri katika kupata ufumbuzi kwenye matatizo hayo kama yapo na ikiwa hayapo isipokuwa ni yale matatizo madogo madogo tu yanayowakabili wanandoa basi pia kwa hayo Allaah Aliyetukuka Atawaondoshea ili waweze kuishi kwa furaha na masikilizano inshaAllaah kama Anavyosema Subhaanahu wa Ta'ala:

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share