046-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Kumswalia Mtume Pahala Pake Na Matamshi Yake Mbali Mbali

 

KUMSWALIA MTUME PAHALA PAKE NA MATAMSHI YAKE MBALI MBALI

 

Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akijiswalia mwenyewe katika Tashahhud ya kwanza na nyingineo([1]). Na akaifanya kuwa ni amrisho kwa Ummah wake, kwani aliwaamrisha kumswalia yeye baada ya kumuombea amani([2]), na aliwafundisha matamshi mbali mbali ya kumswalia.

1-

Allaahumma Swalli ‘Alaa Muhammadin, Wa ‘Alaa Ahli Baytihi, Wa ‘Alaa Az-Waajihi Wa Dhurriyaatihi, Kamaa Swallayta ‘Alaa Aali Ibraahiyma, Inaka Hamiydun Majiydun, Wa Baarik ‘Alaa Muhammadin, Wa ‘Alaa Aali Baytihi, Wa ‘Alaa Az-Waajihi Wa Dhurriyaatihi, Kamaa Baarakta ‘Alaa Aali Ibraahiyma, Inaka Hamiydun Majiydun

 

Ee Allaah! Mswalie Muhammad([3]) Na Watu Wa Nyumbani Kwake, Na Wake Zake, Na Kizazi Chake Kama Ulivyowaswalia Jamaa Zake Ibraahiym, Hakika Wewe Ni Mwenye Kusifika Mtukufu. Na Mbariki Muhammad([4]) Na Jamaa Wa Nyumba Yake, Na Wake Zake, Na Kizazi Chake Kama Uliyowabariki Jamaa Zake Ibraahiym, Hakika Wewe Ni Mwenye Kusifika Mtukufu. 

 

Du'aa hii alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akiitumia kwa kuomba yeye mwenyewe([5]).

2-

 

Allaahumma Swalli ‘Alaa Muhammadin, Wa ‘Alaa Aali Muhammadin, Kamaa Swallayta ‘Alaa [Ibraahiyma, Wa ‘Alaa] Aali Ibraahiyma, Inaka Hamiydun Majiydun, Allaahumma Baarik ‘Alaa Muhammadin, Wa ‘Alaa Aali Muhammadin, Kamaa Baarakta ‘Alaa [Ibraahiyma Wa ‘Alaa] Aali Ibraahiyma, Inaka Hamiydun Majiydun

 

Ee Allaah! Mswalie Muhammad, Na Jamaa Wa Muhammad, Kama Ulivyomswalia [Ibraahiym Na Juu Ya]([6]) Jamaa Zake Ibraahiym, Hakika Wewe Ni Mwenye Kusifika Mtukufu. Ewe Allaah! Mbariki Muhammad Na Jamaa Zake Muhammad Kama Ulivyombariki [Ibraahiym Na Juu Ya]([7]), Jamaa Zake Ibraahiym, Hakika Wewe Ni Mwenye Kusifika Mtukufu.([8])

 

3-

Allaahumma Swalli ‘Alaa Muhammadin, Wa ‘Alaa Aali Muhammadin, Kamaa Swallayta ‘Alaa Ibraahiyma [Wa Aali Ibraahiyma], Inaka Hamiydun Majiydun, Wa Baarik ‘Alaa Muhammadin, Wa ‘Alaa Aali Muhammadin, Kamaa Baarakta ‘Alaa [Ibraahiyma Wa] Aali Ibraahiyma, Inaka Hamiydun Majiydun

 

Ee Allaah! Mswalie Muhammad Na Jamaa Zake Muhammad Kama Ulivyomswalia Ibraahiyhm [Na Jamaa Zake Ibraahiym], Hakika Wewe Ni Mwenye Kusifika Mtukufu. Na Mbariki Muhammad Na Jamaa Zake Muhammad Kama Ulivyombariki [Ibraahiym Na] Jamaa Zake Ibraahiym Hakika Wewe Ni Mwenye Kusifika Mtukufu.([9])

 

4-

Allaahumma Swalli ‘Alaa Muhammadin [An Nabiyyil Ummiyyi], Wa ‘Alaa Aali Muhammadin, Kamaa Swallayta ‘Alaa [Aali] Ibraahiyma, Wa Baarik ‘Alaa Muhammadin [An Nabiyyil Ummiyyi], Wa ‘Alaa Aali Muhammadin, Kamaa Baarakta ‘Alaa [Aali] Ibraahiyma Fil ‘Aalamiyna, Inaka Hamiydun Majiydun

 

Ee Allaah! Mswalie Muhammad [Nabii Ummiy (Asiyejua Kusoma Au Kuandika)] Na Jamaa Zake Muhammad Kama Ulivyowaswalia [Jamaa Zake] Ibraahiym, Na Mbariki Muhammad [Nabii Ummiy] Na Jamaa Zake Muhammad Kama Ulivyowabariki [Jamaa Zake] Ibraahiym Miongoni Mwa Ummah, Hakika Wewe Ni Mwenye Kusifika Mtukufu.([10])

 

 

5-

 

Allaahumma Swalli ‘Alaa Muhammadin ‘Abdika Wa Rasuulika, Kamaa Swallayta ‘Alaa [Aali] Ibraahiyma, Wa Baarik ‘Alaa Muhammadin [‘Abdika Wa Rasuulika], [Wa ‘Alaa Aali Muhammadin], Kamaa Baarakta ‘Alaa Ibraahiyma [Wa ‘Alaa Aal Ibraahiyma]

 

Ee Allaah! Mswalie Muhammad Mja Wako Na Mjumbe Wako Kama Ulivyowaswalia [Jamaa Zake] Ibraahiym, Na Mbariki Muhammad [Mja Wako Na Mjumbe Wako] [Na Jamaa Zake Muhammad] Kama Ulivyowabariki Jamaa Zake Ibraahiym [Na Jamaa Zake Ibraahiym]([11])

 

6-

 

Allaahumma Swalli ‘Alaa Muhammadin, Wa [‘Alaa] Az-Waajihi Wa Dhurriyaatihi, Kamaa Swallayta ‘Alaa [Aali] Ibraahiyma, Wa Baarik ‘Alaa Muhammadin, Wa [‘Alaa] Az-Waajihi Wa Dhurriyaatihi, Kamaa Baarakta ‘Alaa [Aali] Ibraahiyma, Inaka Hamiydun Majiydun

 

Ee Allaah! Mswalie Muhammad Na Wake Zake Na Kizazi Chake, Kama Ulivyowaswalia [Jamaa Zake] Ibraahiym, Na Mbariki Muhammad Na Wake Zake Na Kizazi Chake Kama Ulivyowabariki [Jamaa Zake] Ibraahiym, Hakika Wewe Ni Mwenye Kusifika Mtukufu.([12])

 

 

7-

Allaahumma Swalli ‘Alaa Muhammadin Wa ‘Alaa Aal
Muhammaadin, Wa Baarik ‘Alaa Muhammadin, Wa ‘Alaa Aal Muhammadin, Kamaa Swallayta ‘Alaa Ibraahiyma Wa ‘Alaa Aal Ibraahiyma Inka Hamiydin Majiydun

 

Ee Allaah! Mswalie Muhammad Na Jamaa Zake Muhammad, Na Mbariki Muhammad Na Jamaa Zake Muhammad Kama Ulivyomswalia Na Ukambariki Ibraahiym Na Jamaa Zake Ibraahiym, Hakika Wewe Ni Mwenye Kusifika Mtukufu.([13])

 

 

[1] Abu 'Awaanah katika Swahiyh yake (2/324) na An-Nasaaiy.

[2] Wamesema, "Ewe Mjumbe wa Allaah! Tumefundishwa kukuombea amani (yaani katika Tashahhud) lakini vipi tukuswalie?" Akasema: "Semeni Allaahumma Swalli 'alaa Muhammad…" n.k. Hivyo hakubainisha kuwa khaswa kwa Tashahhud moja na bila ya nyingine. Hivyo kuna dalili hapa ya kuamrishwa kumswalia katika Tashahhud ya kwanza pia. Hii ni madhehebu ya Imaam Ash-Shaafi'iy kama alivyonukuu katika kitabu chake Al-Umm, nayo ni Swahiyh kwa wafuasi wake kama alivyoeleza  An-Nawawiy katika Al-Majmuu' (3/460) na ikatiliwa nguvu na  Rawdhwah At-Twaalibiyn (1/263). Ni rai pia ya Al-Waziyr bin Hubayrah Al-Hanbaliy katika Al-Ifswaah kama Ibn Rajab alivyonukuu na akaipa nguvu katika Dhayl Twabaqaat (1/280). Hadiyth nyingi zimekuja kuhusu kumswalia  (صلى الله عليه وآله وسلم) katika Tashahhud. Hakuna hata mojawapo iliyoeleza bayana kuhusu yaliyotajwa, bali Hadiyth hizo ni za ujumla zimejumuuisha Tashahhud zote. Na nimetaja hii katika Al-Aswl kama ni ta'liyq (kiambatisho) lakini sio katika matini kuu kwani haziridhishi shuruti zetu za (kutambulisha) usahihi. Lakini zinakubaliana katika maana, na wale wanaokanusha na kupinga hii, hawana dalili sahihi kutumia kama ni ushahidi, kama nilivyopambanua katika Al-Aswl. Kama kauli ya kuonyesha kuongeza chochote katika 'Allaahumma Swalli 'alaa Muhammad' ni Makruuh (inachukiza), pia haina asili katika Sunnah, wala hakuna dalili inayokinaisha. Bali tunaona kwamba anayesema hivi hafuati maamrisho ya nyuma ya Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم), 'Allaahumma Swalli 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad ...' na hoja zaidi za hii zipo katika Al-Aswl.

[3] Rai ya mwanzo kabisa kuhusu maana ya 'kumswalia  Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم)" ni ya Abu Al-'Aaliyah (kwa marejeo ya Suratul-Ahzaab 33: 56), 'Swalah ya Allaah kwa Mtume ina maana kudhibiti na kumpa utukufu; Swalah ya Malaika na wengineo ni kuomba hivyo kwa Allaah, na hapa inamaanisha kuomba Swalah zizidishwe na sio asili ya Swalah yenyewe". Ibn Hajar amenukuu katika Fat-h Al-Baariy, na amepinga kauli mashuhuri kwamba Swalah ya Mola ni Rahmah, akaipambanua hii Ibn Al-Qayyim katika Jalaa Al-Ahkaam, akiacha nafasi ndogo kwa maoni zaidi.

[4] Kutokana na barakah: ukuaji, uongezaji na kukua, kubarikika. Hivyo du'aa hii inamdhamini Muhammad mema ambayo Allaah Amewajaalia familia ya Ibraahiym, kumdumishia na kumthibitishia na pia kumuongezea maradufu.  

[5] Ahmad na Atw-Twahaawiy ikiwa na isnaad Swahiyh.

[6] Taz. Tanbihi ifuatayo.

[7] Nyongeza hizi mbili ni ushahidi wenye kuthibitika katika Al-Bukhaariy, Atw-Twahaawiy, Al-Bayhaqiy, Ahmad na An-Nasaaiy. Pia zimekuja katika njia mbali mbali za usimulizi katika aina nyinginezo za du'aa (Taz. Namba 3, 7). Hivyo usichanganywe na rai ya Ibn Al-Qayyim katika Jalaa Al-Afhaam (Uk. 198) akifuata nyayo za Mwalimu wake mkuu Ibn Taymiyyah katika Al-Fataawa (1/16). "Hakuna Hadiyth Swahiyh kuhusu ibara 'Ibraahiym wa aali Ibraahiym' pamoja". Hapa tumekuonyesha Hadiyth zilizo Swahiyh. Kosa la Ibn Al-Qayyim limebainika kutokana na mwenyewe kukiri kuwa (aina ya kumswalia) Namba 7 (inayofuatia) ni Swahiyh ambayo imetaja aliyokanusha kabla! 

[8] Al-Bukhaariy, Muslim, Al-Humaydiy (138/1) na Ibn Mandah (68/2) ambaye amesema kuwa kuna makubaliano kuwa Hadiyth hii ni Swahiyh.

[9] Ahmad, An-Nassaiy na Abu Ya'laa katika Musnad yake (44/2) ikiwa na isnaad Swahiyh.

[10] Muslim, Abu 'Awaanah, Ibn Abi Shaybah (2/132/1) na Abu Daawuud, na Al-Haakim amekiri ni Swahiyh.

 

[11] Al-Bukhaariy, An-Nasaaiy, Atw-Twahaawiy, Ahmad na Ismaa'iyl Al-Qaadhwi katika Fadhwl As-Swalaah 'alan-Nabiyy  (صلى الله عليه وآله وسلم) (Uk. 28 Chapa ya mwanzo, Uk. 62 Chapa ya pili ikiwa na utafiti wangu).

[12] Al-Bukhaariy, Muslim na An-Nasaaiy.

[13] An-Nasaaiy, Atw-Twahaawiy, Abu Sa'iyd bin Al-'Araabiy katika Al-Mu'jam (79/2) ikiwa na isnaad Swahiyh. Ibn al-Qayyim ametoa chanzo chake katika Al-Jalaa Al-Afhaam (Uk. 14-15) ya Muhammad bin Is-haaq As-Siraaj na akakiri kuwa ni Swahiyh. Kauli hii inajumuisha zote mbili 'Ibraahiym na jamaa zake Ibraahiym' jambo lililokanushwa na wote wawili; Ibn Al-Qayyim na Mwalimu wake Ibn Taymiyah, kama ilivyoelezwa juu.

 

Share