045-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Wajibu Wa Tashahhud Ya Kwanza Na Hukmu Ya Du'aa Ndani Yake Pamoja Na Matamshi Yake

 

WAJIBU WA TASHAHHUD YA KWANZA NA HUKUMU YA DU'AA NDANI YAKE

 

Kisha alikuwa  (صلى الله عليه وآله وسلم) akisoma At-Tahiyyaatu kila baada ya rakaa mbili([1]).

 

Na alikuwa kitu cha kwanza anachokisema anapokaa ni: ((At-Tahiyyaatu LiAllaah)).([2])

 

Na anapoisahau Tashahhud katika rakaa  mbili za mwanzo, husujudu Sajdatus-Sahw-).([3])

 

Alikuwa akiiamrisha Tashahhud - kwa kusema: ((Mtakapokaa katika kila rakaa mbili, semeni: 'At-Tahiyaatu …..na kila mmoja wenu ajichagulie du'aa anayoipenda zaidi amuombe Allaah (عزوجل) [kwayo]))([4]).  Katika riwaaya nyingine: ((Semeni katika kila kikao 'At-Tahiyyaatu'))([5]), na alimuamrisha aliyeswali vibaya kufanya hivyo kama ilivyotajwa.

 

Alikuwa  (صلى الله عليه وآله وسلم)akiwafundisha Tashahhud kama alivyokuwa akiwafundisha Surah katika Qur-aan([6]) na "Sunnah ni kuisema kimya kimya.([7])

 

 

 

 

MATAMSHI MBALI MBALI YA TASHAHHUD

 

Mtume  (صلى الله عليه وآله وسلم)aliwafundisha matamshi mbali mbali ya Tashahhud:

 

1- Tashahhud ya Ibn Mas'uud ambaye amesema: "Amenifundisha Mjumbe wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) Tashahhud, viganja vyangu baina ya viganja vyake   (صلى الله عليه وآله وسلم) kama anavyonifundisha Surah katika Qur-aan:

 

 

 

At-Tahiyyaatu LiAllaahi, Was-Swalawaatu, Wat-Twayyibaatu, As Salaamu ‘Alayka Ayyuha-Nnabiyyu Warahmatu Allaahi Wabarakaatuh, As Salaamu ‘Alaynaa Wa’alaa ‘Ibaadi Allaahis Swaalihiyn, Ash-Hadu Al-Laa Ilaha Il-La Allaah Wa Ash-Hadu Anna Muhammadan ‘Abduhu Warasuuluhu.

 

Maamkuzi mema,([8]) na rehema([9]) na mazuri yote([10]), ni kwa Allaah, amani([11]), zishuke juu yako Ewe Mtume na Rehma za Allaah, na Baraka Zake ([12]),  amani ishuke juu yetu, na juu ya waja wa Allaah walio wema, (kwani mtu anaposema hivi, inajumuisha kila mja mwema mbinguni na ardhini) nashuhudia kwamba hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila  Allaah, na nashuhudia kwamba Muhammad ni mja Wake na ni Mjumbe Wake. [Na hali ya kuwa yeye (صلى الله عليه وآله وسلم) yu pamoja nao (Hivi alivyokuwa na sisi, lakini) alipofariki tukawa tunasema:

 

As Salaamu ‘Alan-Nabiyyi

Amani ishuke juu ya Mtume).([13])

 

 

2- Tashahhud ya Ibn 'Abbaas, amesema: "Mjumbe wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akitufundisha Tashahhud kama anavyotufundisha [Suraah katika] Qur-aan. Alikuwa akisema:

 

At-Tahiyyaatu Al-Mubarakaatu Aswalawaatu, At Twayyibaatu LiAllaahi, [As] Salaamun ‘Alayka Ayyuha-Nnabiyyu Warahmatu Allaahi Wabarakaatuh, [As] Salaamun ‘Alaynaa Wa’alaa ‘Ibaadi Allaahis Swaalihiyn, Ash-hadu Al-Laa Ilaha Il-La Allaah, Wa [Ash-hadu] Anna Muhammadan Rasuulu Allaah, [‘Abduhu Wa Rasuuluhu].

Maamkuzi mema, maneno ya Baraka, Swalah, mazuri yote ni ya Allaah, amani ishuke juu yako ewe Mtume na Rehma za Allaah na Baraka Zake. Amani ishuke juu yetu na waja wema wa Allaah, nashuhudia kwamba hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Allaah,  na (nashuhudia) kwamba Muhammad ni Mjumbe wa Allaah, [na katika riwaaya …mja wake na Mjumbe wake][14]

 

 

3- Tashahhud au Tahiyyaatu ya Ibn 'Umar ambaye ameripoti kwamba Mjumbe wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema katika Tashahhud:

At-Tahiyyaatu LiAllaahi [Wa] Sswalawaatu, [Wa] Ttwayyibaatu, As-Salaamu ‘Alayka Ayyuha-Nnabiyyu Warah-Matu Allaahi – Wabarakaatuh -, As- Salaamu ‘Alaynaa Wa’alaa ‘Ibaadi Allaahis Swaalihiyn, Ash-hadu Al-Laa Ilaha Il-La Allaah, Wah-dahu Laa Shariyka Lahuu, Ash-hadu Anna Muhammadan ‘Abduhu Wa Rasuuluhu.

Maamkuzi mema ni ya Allaah, (na) Swalah (na) mazuri, amani ishuke juu yako ewe Mtume na Rehma za Allaah - Ibn 'Umar amesema: "Nimeongezea([15]) …. na Baraka Zake – Amani ishuke juu yetu na waja wema wa Allaah, nashuhudia  kwamba hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Allaah – Ibn 'Umar amesema: "Nimeongozea([16]) - … Pekee Hana mshirika - na nashuhudia kwamba Muhammad ni mja Wake na ni Mjumbe Wake.([17])

 

 

4- Tashahhud ya Abu Muusa Al-Ash'ariyy ambaye amesema kwamba, Mjumbe wa Allaah  (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((… Mnapokaa, kauli ya mwanzo ya kila mmoja wenu iwe:

At-Tahiyyaatu At-Twayyibaatu As-Swalawaatu LiAllaahi, As-Salaamun ‘Alayka Ayyuha-Nnabiyyu Warah-Matu Allaahi Wabarakaatuh, As-Salaamun ‘Alaynaa Wa’alaa ‘Ibaadi Allaahis Swaalihiyn, Ash-Hadu Al-Laa Ilaha Il-La Allaah, Wah-Dahu Laa Shariyka Lahuu Wa Ash-Hadu Anna Muhammadan ‘Abduhu Wa Rasuuluhu.

Maamkizi, mazuri, Swalah ni kwa ajili ya Allaah, amani ishuke juu yako ewe Mtume na Rehma za Alalh na Baraka Zake, amani ishuke juu yetu na juu ya waja wema, nashuhudia kwamba hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah, [Pekee Hana mshirika] na nashuhudia kwamba Muhammad ni mja Wake na Mjumbe Wake.([18])

Matamshi saba ndio Taahiyyaatu.([19])

 

5- Tashahhud ya ‘Umar bin Al-Khatwtwaab ambaye alikuwa akiwafundisha watu Tashahhud huku akiwa juu ya Minbar akisema: "Semeni:

At-Tahiyyaatu LiAllaahi, Az-Zaakiyaatu LiAllaahi, At-Twayyibaatu [LiAllaahi], As-Swalawaatu LiAllaah, As-Salaamun ‘Alayka Ayyuha-Nnabiyyu Warah-matu Allaahi Wabarakaatuh, As-Salaamun ‘Alaynaa Wa’alaa ‘Ibaadi Allaahis Swaalihiyn, Ash-hadu Al-Laa Ilaha Il-La Allaah, Wa Ash-Hadu Anna Muhammadan ‘Abduhu Wa Rasuuluhu.

Maamkizi ni ya Allaah, kutakasika kote ni kwa Allaah, mazuri [ni kwa ajili ya] Allaah, Swalah ni kwa ajili ya Allaah, amani ishuke kwako ewe Mtume na  Rahma za Allaah na Baraka Zake, amani ishuke kwetu na kwa waja wema wa Allaah, nashuhudia kwamba hapana apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah, na nashuhudia kwamba Muhammad ni mja Wake na Mjumbe wake.([20])

 

[1] Muslim na Abu 'Awaanah.

[2] Al-Bayhaqiy amesimulia katika usimulizi kutoka kwa 'Aaishah ikiwa na isnaad nzuri kama ilivyohakikishwa na Ibn Al-Mulaqqin (28/2).

[3] Al-Bukhaariy na Muslim. Imetolewa katika Al-Irwaa Al-Ghaliyl (338).

[4] An-Nasaaiy, Ahmad na Atw-Twabaraaniy katika Mu'jam Al-Kabiyr (3/25/1) ikiwa na isnaad Swahiyh. Maana halisi ya Hadiyth ni dalili ya kuamrishwa du'aa katika kila Tashahhud hata isiyoungana na Tasliym. Na hii ni rai ya Ibn Hazm (رحمه الله  ).   

[5] An-Nasaaiy ikiwa na isnaad Swahiyh.

[6] Al-Bukhaariy na Muslim.

[7]Abu Daawuud na Al-Haakim aliyekiri kuwa ni Swahiyh, na Adh-Dhahabiy amewafikiana.

[8] "At-Tahiyyaatu" yaani, maneno yote yanayoambatana na amani, ufalme na kudumu ni kwa ajili ya Allaah.  (An-Nihaayah)

[9] "As-Swalawaatu" yaani, 'du'aa zote zinazotumika kumtukuza Allaah Ta'ala, kwani Yeye ni Mwenye kustahiki nazo, na hakuna apasaye kustahiki nazo isipokuwa Yeye. (An-Nihaayah)

[10] "At-Twayyibaatu" yaani, maneno mazuri na masafi yote yanayofaa kumsifu Allaah, na sio yale ambayo yasiyofanana na sifa Zake ambayo hutukuzwa kwazo wafalme. (Fat-hul-Baariy)

[11] Maana, kujikinga na Allaah na kutiwa nguvu Naye kwa vile As-Salaam (amani) ni Jina la Allaah khasa. Hivyo maamkizi yanamaanisha: Allaah Awe Muwakilishaji na Mlinzi wako. Kama inavyosemwa: 'Allaah Ma'ak' (Allaah Awe nawe) yaani Ulinzi Wake, msaada na ihsani.

[12] Ni neno linalotumika kwa mazuri yote yanayotoka kwa Allaah.

[13] Al-Bukhaariy, Muslim, Ibn Abi Shaybah (1/90/2) Siraaj na Abu Ya'laa katika Musnad yake (258/2). Imetolewa katika Al-Irwaa (321).

 

Kauli ya Ibn Mas'uud: "Tulisema: 'Amani ishuke juu ya Mjumbe', inabainisha kwamba Maswahaba (رضي الله عنهم) walikuwa wakisema: Amani ishuke juu yako ewe Mtume صلى الله عليه وآله وسلم) katika Tashahhud alipokuwa  Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) yuhai, lakini alipofariki, waliacha hivyo na badala yake wakawa wakisema: 'Amani imshukie Mtume'. Bila shaka, hii ilikuwa ni kwa uidhinishaji wa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم). Hii imetiliwa nguvu kwa vile Mama wa Waumini 'Aaishah (رضي الله عنها) alifundisha Tashahhud katika Swalah kwa: 'Amani ishuke juu ya Mtume' kama ilivyosimuliwa na Siraaj katika Musnad yake (9/1/2) na Mukhlisw katika Al-Fawaaid (11/54/1) ikiwa na isnaad mbili Swahiyh kutoka kwake.

 

Ibn Hajar amesema: 'Ziada hii inaonyesha dhahiri kwamba walikuwa wakisema: 'Amani ishuke kwako ewe Mtume' wakimuelekezea yeye wakati wa uhai wake, lakini alipofariki Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) waliacha kumuelekezea hivyo wakimtaja kama ni mtu wa nafsi ya tatu badala yake wakisema: 'Amani ishuke juu ya Mtume'". Amesema pia sehemu nyingine, 'As-Subkiy amesema katika Sharh Al-Minhaaj baada ya kutaja usimulizi kutoka kwa Abu 'Awaanah pekee, 'ikiwa usimulizi huu ni Swahiyh kutoka kwa Maswahaba, inathibitisha kwamba baada ya (kufariki) Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم), sio lazima kumuelekezea Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) maamkizi ya amani, hivyo mtu aseme: 'Amani ishuke juu ya Mtume'. (Ibn Hajar anaendelea: "Hii ni Swahiyh bila ya shaka (kwa sababu imethibitishwa katika Swahiyh Al-Bukhaariy) na pia nimepata dalili ya kutilia nguvu". 'Abdur-Razzaaq amesema: "Ibn Jurayj ameniarifu: 'Atwaa amenijulisha kwamba Maswahaba walikuwa wakisema 'Amani ishuke kwako ewe Mtume' alipokuwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) yuhai, lakini baada ya kufariki walikuwa wakisema: 'Amani ishuke juu ya Mtume', na hii ni isnaad Swahiyh. Ama usimulizi wa Sa'iyd bin Manswuur kutoka kwa 'Ubaydah bin 'AbdiAllaah bin Mas'uud, ambaye ameripoti kutoka kwa baba yake kwamba Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) amemfundisha Tashahhud kisha yeye (‘Abdullaah bin Mas'uud) akaisema (Tashahhud), Ibn 'Abbaas amesema: "Tulikuwa tukisema 'Amani ishuke juu yako ewe Mtume' alipokuwa yuhai pekee", ambayo Ibn Mas'uud amejibu akisema: "Hivi ndivyo tulivyofundishwa na hivi ndivyo tunavyofundisha". Inavyoelekea ni kwamba Ibn 'Abbaas amesema kuwa hili ni jambo la kujadiliana lakini Ibn Mas'uud hakulikubali. Lakini usimulizi wa Abu Ma'mar (yaani usimulizi katika Al-Bukhaariy) ndio ulio Swahiyh zaidi, kwa vile Abu 'Ubaydah hakusikia (Ahaadiyth) kutoka kwa baba yake, na juu ya hivyo, isnaad inayoelekea hadi kwa Abu 'Ubaydah ni dhaifu" (mwisho wa kunukuu kutoka kwa Ibn Hajar).

 

Maneno haya ya Ibn Hajar yamenukuliwa na Maulamaa wengi katika utafiti wao, mfano; Al-Qastwalaaniy, Az-Zarqaaniy, Al-Laknaawiy n.k. Wote wamechagua kutoa maneno yake bila ya kutoa tanbihi zaidi. Hoja hizi zimetajwa kikamilifu zaidi katika Al-Aswl.

 

[14]    Muslim, Abu 'Awaanah, Ash-Shaafi'iy na An-Nasaaiy.

[15] Taz. Tanbihi inayofuatia.

[16] Ziada mbili hizi zimethibitika kuwa ni sehemu ya Tashahhud kutoka kwa  Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم). Ibn 'Umar hakuziongeza kwa upendekezo wa nafsi yake (hasha ameepukana na hayo); bali amejifunza hayo kutoka kwa Maswahaba ambao wameziripoti kutoka kwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم), kisha ndio akaziongezea katika Tashahhud ambayo amesikia  moja kwa moja kutoka kwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم).     

[17] Abu Daawuud na Ad-Daaraqutwniy ambaye amekiri ni Swahiyh.

[18] Muslim, Abu 'Awaanah, Abu Daawuud na Ibn Maajah.

[19] Kifungu kile kile kilichotajwa hapo mbeleni.

[20] Maalik na Al-Bayhaqiy ikiwa na isnaad Swahiyh. Ingawa Hadiyth hii ni Mawquuf, lakini ina hukmu ya Marfuu' kwani inajulikana kuwa haisemwi tu kutokana na rai ya mtu, na lau kama ingelikuwa ni rai, basi kauli hii isingelikuwa ni dhikr bora miongoni mwa adhkaar nyingine kama alivyosema 'Ibn 'Abdil-Barr.

 

TANBIHI: Hakuna ziada ya 'wa maghfiratuhu…' (na maghfirah Yake) katika Tashahhud yoyote katika hizi, kwa hiyo isiwe desturi ya mtu kusema. Kwa ajili hiyo baadhi ya Masalaf wameikanusha kutokana na usimulizi ufuatao:

 

Atw-Twabaraaniy (3/56/1) ameripoti ikiwa na isnaad Swahiyh kutoka kwa Twalha bin Muswarrif ambaye amesema: "Rabiy' bin Khaytham ameongeza katika Tashahhud, '…wa Barakaatuhu, wa Maghfiratuhuu!' Hivyo 'Alqamah akasema: "Tumesita tulipofundishwa:  'amani ishuke juu yako ewe Mtume, na Rahma za Allaah na Baraka Zake". 'Alqamah alikuwa akifuata khaswa mfano wa Mwalimu wake ‘Abdullaahi bin Mas'uud (رضي الله عنه) ambaye kutoka kwake imeripotiwa kuwa ni Swahiyh. Alikuwa akimfundisha mtu Tashahhud, na alipofika katika neno: 'Nakiri kwamba hakuna mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah…', yule mtu alisema: "Pekee, Hana mshirika", na ‘Abdullaah akasema: "Yeye ni hivyo lakini tunakomea pale tulipofunzwa". [Imesi;;;/

muliwa na Atw-Twabaraaniy katika Mu'jam Al-Awswat Namba. 2848 ikiwa na isnaad Swahiyh].

 

 

Share