Mwanamke Anaweza Kutia Wudhuu Akiwa Katika Hedhi?

 

Mwanamke Anaweza Kutia Wudhuu Akiwa Katika Hedhi?

 

 www.alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Asalam Alaykum Warahmatullahi Wabarakatuh

 
Baada ya salam naomba kuuliza kuwa mwanamke anaweza kutia udhu akiwa katika siku zake za hedhi.

 

 

JIBU:

 

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Hakuna pingamizi lolote kuhusu kuchukua wudhuu ukiwa katika hedhi. Hata hivyo, kuchukua kwako wudhuu hakutakuwa na taathira yoyote kwako hutaweza kufanya ‘Ibaadah zote kwani ‘Ibaadah zinataka utohara. Na utohara wa hedhi ni kuoga mwili mzima sio kuchukua wudhuu. Hata hivyo, ni vyema kuchukua wudhuu kama unataka kwenda kulala kwani hilo ni agizo la Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  kwa wakati huo kama alivyofanya alipokuwa katika janaba kama alivyosema:

 

 

((إِذَا أَتَى أَحَدُكُمْ أَهْلَهُ، ثُمَّ أَرادَ أَنْ يَعُودَ فَلْيَتَوَضَّأ  ْ(بينهما وضوءاً)  ( وفي رواية: وضوءه للصلاة )، فَإِنَّهُ أَنْشَطُ لِلْعَوْدِ))

((Mmoja wenu anapomjia mkewe kisha akipenda kumrudia mara nyingine, basi achukue wudhuu baina ya nyakati (vitendo) mbili (katika riwaaya nyingine wudhuu ule ule kama wa Swalaah) kwani hakika itampa (nashati) uchangamfu kurudia kwake))  [Muslim, Ibn Abi Shaybah na wengineo]

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share