Itikadi Potofu Za Qadiyani

 

Itikadi Potofu Za Qadiyani

 

Alhidaaya.com

 

 

SWALI: 

 

Nasikitika sana kuwa ndugu zangu wengi tunaoishi pamoja hapa Dublin -Ireland wakutokoea Kenya na Tanzania wamejiunga nao. Tena kwa mori na hamasa. Nawaamabilii neno. wataka uwasikize wao na si wewe. Nimefwatilia baadhi ya itkadi zao nikapata kuwa wana husiana na ahmadiya anjuman Baadhi Ya Itikadi Zao.

 

1. Wanaamini Kuwa Nabiy 'Iysa ('Alayhis-salaam). Amesulubiwa Na Kufa Na Kufufuka Wala Hakupazawa Mbinguni. Alifia Hapa Hapa.
 
2. Utume Bado Ungaliko Na Unabii Ndio Umekwisha. Na Nabiy Wao Ni Elijah Mohamed.
 
3. Hawaamini Miujza Ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Alowapa Rusuli Yake 4. Hawaamini Kuwa Nabiy Adam (Alaayhis-salaam) Alikuwa Peponi Na Ile Pepo Ilotajwa Kwenye Qur'an Ni Bustani Lilioko Basra Na Baghdad.
 
4. Hawaamini Kuwa Majini Ni Viumbe Bali Ni Binaadam Waovu Na Mayahudi 6. Wadai Kuwa Almasihi Na Al Mahdi Ni Mtu Mmoja Na Ndiye Shekhe Wao Alotangulia

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho

 

 

 

Hakika Muislamu hafai kuwaita hao Maqadiyani kuwa ni Ahmadiya. Wao wanataka waitwe hivyo ili Waislamu wasiweze kuwatambua na hivyo kuwafuata kwani hilo jina, Ahmad ni jina jingine la Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).

 

Hakika hawa ni watu wabaya kabisa kwani wana sifa nyingine mbali na hizo ulizotaja. Mfano ni:

  1. Hakika ni kuwa wao hawahusiani na Nation of Islam ambayo iliongozwa na Elijah Muhammad. Japokuwa hao Nation Of Islam wana ukafiri kama hao Maqadiyani.

 

  1. Jihadi hakuna tena, na ni wajibu kuwatii wakoloni na hasa Waingereza.

 

  1. Wana kitabu chao ambacho kinaitwa Kitaabul Mubiyn (Kitabu cha wazi).

 

  1. Qadiyan, ambao ni mji ulioko India na unakaribiana na Pakistan ni mtukufu kwao kama Makkah na hata mahekalu yaliyomo huko ya Maqadiyani ni matukufu kwao kama vile Msikiti wa Makkah.

 

  1. Mtume wao wa mwisho na ambaye pia ni masihi ni huyu mwandishi wao aliyesaidiwa sana na Uingereza, Mirza Ghulam Ahmad.

 

Ni nasaha kwako uendelee na Da‘wah ya kuwaelezea hao ndugu zetu huenda wakaja kuwafahamu na kuwaacha.  Na soma na wafikishie makala hizi zilizomo ndani ya ALHIDAAYA kuhusiana na kundi hilo potofu:

 

 

Tatizo La Uqadiyani

 

Jihadhari Na Kundi La Ahmadiya (Maqadiyani) Dhidi Ya Uislam

 

 

Tunakutakiwa kila la kheri katika ulinganizi wako huo na ujira wako uko kwa Allaah Aliyetukuka.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 
Share