Juisi Ya Melon Na Embe

Juisi Ya Melon Na Embe

 

Vipimo

 

Tikiti la asali (honey melon) - 1

Embe - 3

Tangawizi - 1 Kijiko

Ndimu - 1

Sukari - ¼ Kikombe cha chai

Arki rose - 2 Matone

 

Namna Ya Kutayarisha

  1. Limenye melon na ulikate kate kisha tia kwenye blender.
  2. Tia embe iliyokatwa katwa katika blender
  3. Kisha tia ndimu iliyokatwa vipande kiasi pamoja na maganda yake
  4. Halafu weka sukari
  5. Saga vizuri hadi ilainike
  6. Mimina kwenye jagi kisha tia matone mawili ya arki rose ukoroge na tayari kwa kunywewa

Kidokezo:

 

Ukiweka ndimu weka na maganda yake unapata ladha nzuri zaidi.

 

 Bis-swihhah wal-hanaa (kunywa kwa siha na kuburudika)

 

 

 

Share