Biriyani Ya Nyama Ng'ombe - 1

Biriyani Ya Nyama Ng'ombe - 1

 

Vipimo Vya Masala

Nyama vipande - 3 LB

Mtindi - ½ kopo

Kitunguu (thomu/galic) - 1½ kijiko cha supu

Tangawizi - 1½ kijiko cha supu 

Nyanya - 2  

Pilipili mbichi - kiasi  

Nyanya kopo - 4 vijiko vya supu

Vidonge supu - 2

Pilipili nyekundu paprika - kiasi 

Bizari zote saga - 2 vijiko vya supu 

Viazi - 4

Mafuta - 2 mug

Samli - ½ kikombe

Vitungu - 6

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Kwenye sufuria tia nyama, saga nyanya na thomu, pilipili mbichi, tangawizi. Mimina kwenye nyama na mtindi, tia na nyanya kopo, bizari paprika, vidonge vya supu, chumvi kisha changanya  vyote pamoja weka motoni.
  2. Katika sufuria nyengine tia mafuta na samli kaanga vitungu mpaka viwe rangi ya hudhurungi toa weka pembeni.
  3. Kanga viazi  weka pembeni.
  4. Chukua mafuta kidogo uliyokangia tia kwenye nyama  acha katika moto wa kiasi mpaka nyama iwive na maji ya punguke.
  5. Tia  viazi na vitunguu vivunje vunje tia ndani ya nyama  acha moto mdogo.

 

Vipimo Vya Wal

Mchele - 5 mug

Maji - kiasi

Chumvi - kiasi

Mafuta uliyokaanga vitungu - kiasi

Rangi ya biriani - ¼  kijiko cha chai

*Zafarani - ½ kijiko cha chai

*roweka rangi  na zafarani

 

Namna Ya Kutarisha Na Kupika Wali

  1. Osha mchele roweka muda wa saa.
  2. Chemsha maji kama magi 10 hivi  na chumvi tia mchele.
  3. Uache uchemke ukishaiva kiini nusu, mwaga maji chuja.
  4. Mimina juu ya nyama tia rangi na mafuta kwa juu funika.
  5. Aacha kidogo katika oveni kwa muda wa dakika 20 hivi kisha epua ikiwa tayari.
Share