Adhkaar Zenye Thawabu Tele

 

Adhkaar Zenye Thawabu Tele

 

 Alhidaaya.com

 

Zifutazo ni Adhkaar ambazo Muislamu anapozisoma, atajichumia milioni za thawabu  kwa muda usiozidi dakika moja kila moja!  Zote zimetokana na mafunzo Sahihi katika Sunnah. 

 

 

 سُبْحـانَ اللهِ وَبِحَمْـدِهِ عَدَدَ خَلْـقِه ، وَرِضـا نَفْسِـه ، وَزِنََـةَ عَـرْشِـه ، وَمِـدادَ كَلِمـاتِـه 

 

SubhaanaLLahi wa Bihamdihi ‘adada Khalqihi wa Ridhwaa Nafsihi wa Zinata ‘Arshihi wa Midaada Kalimaatihi  (mara 3)

 

Namtakasa Allaah (na kila sifa hasi) na namhimidi kwa idadi ya Viumbe Vyake, na kwa idadi ya vilivyoridhiwa na Nafsi Yake, na kwa uzito wa ‘Arshi Yake, na kwa wingi wa wino wa (kuandikia) Maneno Yake. [Muslim]

 

الْحَمْدُ لِلَّهِ عَدَدَ مَا خَلَقَ، وَالْحَمْدُ لِلَّهِ مِلْءَ مَا خَلَقَ، وَالْحَمْدُ لِلَّهِ عَدَدَ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الأَرْضِ، وَالْحَمْدُ لِلَّهِ عَدَدَ مَا أَحْصَى كِتَابُهُ،  وَالْحَمْدُ لِلَّهِ مِلْءَ مَا أَحْصَى كِتَابُهُ، وَالْحَمْدُ لِلَّهِ عَدَدَ كُلِّ شَيْءٍ، وَالْحَمْدُ لِلَّهِ مِلْءَ كُلِّ شَيْءٍ،

 

AlhamduliLLaahi ‘adada maa Khalaq, wal-HamduliLLaahi  mil-a maa Khalaq, wal HamduliLLaahi ‘adada maa fis-samaawati wa maa fil-ardhi, wal-HamduliLLaahi ‘adada maa ahswaa Kitaabuhu, wal-HamduliLLaahi mil-a maa ahswaa Kitaabuhu, wal-HamduliLLaahi ‘adada kulli shay-in, wal-HamduliLlaahi mil-a kulli shay-in. (mara 3)

 

Himdi Anastahiki Allaah kwa idadi ya Alivyoviumba.  Himdi Anastahiki Allaah kwa ujazo wa Alivyoviumba. Himdi Anastahiki Allaah kwa idadi ya vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini.  Himdi Anastahiki Allaah kwa idadi ya vilivyorekodiwa na Kitabu Chake. Himdi Anastahiki Allaah kwa ujazo wa vilivyorekodiwa na Kitabu Chake.  Himdi Anastahiki Allaah kwa idadi ya kila kitu, na Himdi Anastahiki Allaah kwa ujazo wa kila kitu.

 

 

سُبْحانَ اللهِ عَدَدَ مَا خَلَقَ فِي السَّماءِ، سُبْحانَ اللهِ عَدَدَ مَا خَلَقَ فِي الأَرْضِ، سُبْحانَ اللهِ عَدَدَ مَا  بَيْنَ ذَلِكَ، سُبْحانَ اللهِ عَدَدَ مَا هُوَ خَالِقُ، وَاللهُ أَكْبَرْ مِثْلُ ذَلِكَ، وَالْحَمْدُ لِلَّهِ مِثْلُ ذَلِكَ، وَلاَ إِلَهَ إِلاَّ اللهَ مِثْلُ ذَلِكَ، وَلاَ حَوْلَ وَلاَ قُوَّةَ إِلاَّ بِاللهِ مِثْلُ ذَلِكَ
 

Subhaana-Allaah ‘adada maa Khalaqa fis-samaai, wa Subhaana-Allaah ‘adada maa Khalaqa fil-ardhi, wa Subhaana-Allaah ‘adada maa bayna dhaalika, wa Subhaana-Allaah ‘adada maa Huwa Khaaliq, wa-Allaahu Akbar mithlu dhaalika, wal-HamduliLLaahi mithlu dhaalika, wa laa ilaah illa-Allaaha mithlu dhaalika, wa laa hawla wa laa quwwata illa bi-Allaahi mithlu dhaalika. 

 

 

Ifuatayo ni aina ya Tahmiyd (Kumsifu na Kumshukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Na kisa chake kinafuatilia kutaja uzito wa thawabu zake:

 

اللَّهُمَّ لَكَ الْحَمْدُ كَمَا يَنْبَغِى لِجَلالَ وَجْهِكَ وَعَظِيمِ سُلْطَانِكَ

 

Allaahumma Lakal-Hamdu kamaa yanbaghiy li-Jalaali Waj-hika wa ‘Adhwiymi Sultwaanika

  

Kutoka kwa ibn 'Umar kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  amesema:

 

 إن عبدًا من عباد الله قال: (( يا رب،  لك الحمد كما ينبغي لجلال وجهك وعظيم سلطانك ،  فعضلت بالملكين فلم  يدريا كيف يكتبانها، فصعدا إلى السماء فقالا يا رب،  إن عبدا قد قال مقالة لا ندري كيف نكتبها،  قال الله - وهو أعلم بما قال عبده :  ماذا قال عبدي؟  قالا يا رب إنه قد قال:  يا رب لك الحمد كما ينبغي   لجلال وجهك  وعظيم سلطانك.  فقال الله لهما: اكتباها كما قال عبدي حتى يلقاني فأجزيه بها))  إبن ماجه

 

"Mja katika waja wa Allaah alisema: Ee Rabb wangu! Zako wewe tu sifa zote njema Unayestahiki kushukuriwa kama inavyopasa Utukufu Wako na nguvu Zako kubwa kabisa. Malaika wawili walibabaika hawakujua vipi waandike maneno hayo (jinsi alivyomtukuza utukufu wa Rabb wake) Wakaenda kwa Allaah wakasema: Ee Rabb wetu! Hakika mja wako kasema aliyoyasema na wala hatujui vipi tuyaandike. Akasema Allaah: Kwani kasema nini mja wangu? (Na Allaah Anajua aliyoyasema mja Wake bila ya malaika kumwelezea) Wakasema amesema: Ee Rabb wangu! Zako Wewe tu sifa zote njema Unayestahiki kushukuriwa kama inavyopasa Utukufu Wako na nguvu Zako kubwa kabisa. Allaah akasema: Yaandikeni kama alivyosema mja Wangu mpaka atakaponikuta (siku ya malipo) basi nitampa jazaa yake kwa hayo (aliyoyasema" [Ibn Maajah 2:1249]

 

 

 

Share