Du'aa Ya Nabiy Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Kwa 'Aaishah (رضي الله عنها) Na Ummah Wake

 

Du'aa Ya Nabiy Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Kwa 'Aaishah (رضي الله عنها) Na Ummah Wake

 

 

Alhidaaya.com

 

عَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ الله عَنْهَا قَالَتْ: لَمَّا رَأَيْتُ مِنَ النَّبِيِّ صَلَّى الله عَلَيْهِ وَسَلَّمَ طِيبَ النَّفْسِ, قُلْتُ:  يَا رَسُولَ اللهِ، ادْعُ الله لِي  قَالَ: ((اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِعَائِشَةَ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِهَا وَمَا تَأَخَّرَ وَمَا أَسَرَّتْ وَمَا أَعْلَنَتْ))  فَضَحِكَتْ عَائِشَةُ حَتَّى سَقَطَ رَأْسُهَا فِي حِجْرِ رَسُولِ اللهِ صَلَّى الله عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مِنَ الضَّحِكِ, فَقَالَ: ((أَيَسُرُّكِ دُعَائِي؟))  فَقَالَتْ: وَمَا لِي لا يَسُرُّنِي دُعَاؤُكَ؟
فَقَالَ: ((وَاللهِ إِنَّهَا لَدَعْوَتِي لأُمَّتِي فِي كُلِّ صَلاة))

Kutoka kwa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) ambaye alisema:
"Nilipomuona Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) yuko na furaha, nikamwambia, 'Ee Rasuli wa Allaah niombee mimi du'aa kwa Allaah."

Akajibu:
((Ee Allaah Mghufurie 'Aaishah madhambi yake yaliyopita na yajayo, na yale ayafanyayo kwa siri na dhahiri)).

'Aaishah akacheka hadi kichwa chake kuangukia kwenye paja la Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kucheka sana.  

Kisha Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamuuliza:
((Je, du'aa yangu ndio inayokufanya uwe na furaha?))

Akajibu ('Aaishah):
"Vipi nisiwe na furaha kwa du'aa yako."

Kisha Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema:
((Naapa kwa Allaah, hii ni du'aa yangu ninayowaombea Ummah wangu katika kila Swalaah))

 

[Imekusanywa na Al-Bazzaar, na Imaam Al-Albaaniy akasema ni Hasan katika Silsilat Al-Ahaadiyth Asw-Swahiyhah, namba 2254]

 

 

Share