Sosi Ya Nyanya Za Kuchoma

Sosi Ya Nyanya Za Kuchoma

Vipimo  

Kitunguu - 1 kikate slice

Nyanya za duara - 7 zikate nusu mbili

Dania (kotmiri) iliyokatwa - 3 vijiko vya chakula

Mafuta ya Zaituni (olive oil) - ¼ kikombe cha chai

Kitunguu saumu(thomu/galic) iliyosagwa - 2-3 chembe          

Chumvi - kiasi

Pilipili  mbuzi - ½ ya pilipili

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Anza kuwasha oveni moto wa 350’c.
  2. Kata nyanya zako vipande viwili upande wa ngozi ya nyanya utazame juu weka kwenye treya ya kuchomea pamoja na pilipili iliyokatwa.
  3. Kisha nyunyizia mafuta kama vijiko viwili vya chakula tia kwenye oven kwa muda wa dakila 10-15 kwa moto wa chini(bake) 360’c kisha kwa moto wa juu (grill) 500’c mpaka nyanya iwe na rangi ya kuungua (unaweza pia kuchoma nyanya zako kwenye jiko la mkaa weka nyavu kisha choma.
  4. Ukishatoa kwenye oven ipondeponde kwenye bakuli huku ukiacha mabuja buja ya nyanya (yaani usiisage sana)
  5. Kisha tia chumvi, thomu, kitunguu na dania ichanganyike vizuri
  6. Weka kikaangio(frying pan) jikoni tia mafuta yaliyobaki wacha yapate moto sana kisha mimina mafuta hayo kwenye mchanganyiko huo. (tahadhari na mafuta ya moto wakati wa kumimina ndani ya mchanganyiko mara nyingi mafuta huruka kutokana na maji maji)
  7. Mwisho changanya vizuri ikiwa bado ya motomoto pakuwa tayari kuliwa na mkate au ugali.

 

 

Share