Achari Ya Ndimu Na Karoti
Achari Ya Ndimu Na Karoti

Vipimo
Ndimu – 20
Karoti - 3
Pilipili nyekundu - Kiasi mteko wa mkono
Ndimu ziada za kukamulia - Nyingi kiasi
Chumvi - kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Kata ndimu katikati bila ya kuachana vipande (slit)
 - Kwangua karoti ukate vipande virefurefu
 - Kata pilipili katikati bila ya kuchana
 - Changanya vizuri vyote katika bakuli kubwa kisha tia katika chupa ya achari.
 - Kamua ndimu juisi yake ifunike ndimu na karoti katika chupa.
 - Weka juani muda wa siku chache mpaka zilainike na kuwa tayari
 
Kidokezo:
Hakikisha huingizi maji katika achari ili isiharibike.
Bis-swihhah wal-hanaa (kunywa kwa siha na kufurahika)
    
    