Vitabu Hivi Vinafaa?

 

Vitabu Hivi Vinafaa?

 

Alhidaaya.com

 

 

 

Swali:

 

Asalam Alayku Arhamatulahi Wabarakatu Ndugu Zangu Wa Alhidaaya. Nawaombea Allaah Awapeni Kila La Kheri Na Baraka Afya Na Uhayi Mrefu Na Awalipe Kwa Pepo Ya Fardhowsa Amin. Swali Langu Ni Kuwa Nina Vitabu Ambavyo Nataka Kujua Kama Ni Sahihi Au Sio, Majina Ya Vitabu Ni, Mkweli Mwaminifu Juzu 1 Mpaka Ya 4 Kilicho Tungwa Na Kheikh Said Moosa Mohamed Al-kindy, Na Kitabu Kiitwacho Dua, Nyiradi Na Malipo Yake Aakhirah Na Duniani. Kilicho Tungwa Na Ustadh Said Kh Mkama. Na Kitabu Kiitwacho Kitabu Cha Madua, Kilicho Tungwa Na Said Bin Abdullah Seif L-hatimiy.

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho

 

 

Hakika ukitaka kitabu cha du’aa na adhkaar ambacho kinaaminika na kiko karibu zaidi na usahihi, basi ni kitabu cha Hiswn Al-Muslim ambacho kinapatikana kwa lugha mbalimbali. Unaweza kukipata hapa alhidaaya kwenye kiungo hiki:

 

Hiswnul-Muslim: Du’aa Na Adhkaar Kusoma Na Kwa Kusikiliza (Toleo Lilohaririwa)

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

Share