Urithi Kwa Mke Aliyefiwa Na Mumewe

SWALI:

Asalaam Aleikum Warahmatullahi Taalah Wabarakatu.

Nashukuru sana kupata wasaa huu wa kuweza kuuliza maswali kuhusiana na URITHI - mume  kwa mke aliefariki.  Suala langu ni hili, utaratibu ulokuwa hapa chini, nimeusoma kwenye suala lililoulizwa na mke aliefiwa na mume na kupatiwa jibu hilo hapo chini. Suala langu linahusu mke aliefiwa na mume. 

Je, mpangilio huu pia unahusu mume aliefiwa na mke, , je, mpangilio ni kama hivi ilivi au mume anarithi nini au theluthi ngapi kwa mke aliefariki endapo ataacha nyumba na mali.

Shukran nyingi ziwafikie wote ambao wanataarisha na kushughulikia kuelimisha Umma wa Kiislamu kuhusu mambo yanayotuhusu.  JazalAllaahu kheir. Asalaam Aleikum.

 

 Warithi

Uhusiano na aliyekufa

Hela

Hukumu

1

Mama

16.667

Kwa sababu ya kuwepo kwa mtoto wa aliyefariki anapatiwa sudus (1/6).

2

Mtoto 1

70.833

Mtoto anachukua baki ya urithi.

3

Mke 1

12.5

Kwa sababu ya kuwepo kwa mtoto sehemu yake ya wirathi itakuwa ni thumun (1/8)

4

Kaka 1

0

Kaka na dada wanazuiliwa kurithi kwa sababu ya kuwepo kwa mtoto.

5

Kaka 2

0

  

6

Kaka 3

0

  

7

Dada 1

0

  

8

Dada 2

0

  

9

Dada 3

0

  

  

Jumla

100

  

 

 

 


 

JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukrani zetu za dhati kwa muulizaji ndugu yetu kuhusu swali nyeti la mirathi ya mume aliyefiliwa na mkewe. Uhakika wa mwanzo ni kuwa mpangilio wake ni tofauti kabisa na ule wa mke aliyefiliwa na mumewe.

Kwa swali lako hili lile ambalo tunaweza kukueleza ni yale aliyotueleza Allaah Aliyetukuka katika Qur-aan. Allaah (Subhaanahu wa Ta‘ala) Anasema:

Nanyi (waume) mtapata nusu ya mali walizoacha wake zenu, kama wao hawana mtoto (wala mjukuu). Na ikiwa wana mtoto (au mjukuu), nyinyi mtapata robo ya walivyoacha. Hayo ni baada ya kutoa walivyousia na kulipa deni” (4: 12). Kwa hiyo, mke akifa kabla ya mume, mume atarithi nusu ya mali yake akiwa mkewe hana watoto (mtoto) wala wajukuu (mjukuu) na ikiwa ana mtoto au mjukuu basi atapata robo ya mali ya mkewe.

Haya ni kwa ufupi lakini ili sisi tuweze kuweka jadwali kama ilivyo hapo juu itabidi utueleze watu walio jamaa na aliyefariki walio hai ili tupate kuonyesha vigawanyo hivyo. Tunatumai kwa maelezo hayo tutakuwa tumejibu swali lako.

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share