Wito Kwa Mashia Wenye Akili

Wito Kwa Mashia Wenye Akili

 

Imetarjumiwa na:

 

Muhammad Faraj As-Sa'ay Na Abu 'Abdillaah

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

Napenda kuzungumza katika mlango huu kuhusu maudhui haya ninayopenda kuyaita, “Wito Kwa Mashia Wenye Akili”. Na mazungumzo yangu ni ibara ya utata mwingi nilioupata katika madhehebu haya ya kishia, na nimependa kuwahutubia nao hao wenye akili, hao ambao wanatafiti haki miongoni mwa vizazi vya Mashia pengine watapata jawabu katika utata huu ambao nimeuona umejaa katika vitabu vya Kishia. Na huo ni utata unaobainisha mgongano katika itikadi hii, na huenda nikaifafanua kwa haraka haraka kwani ni mengi ya kuandikwa, na nataka kutoka kwa hao wenye akili wanaofanya utafiti wa haki wajivue na wafanye ikhilasi kwa nia zao kwa ajili ya Allaah Ta’alaa na wachambue utata huu ikiwa ni kweli wako hivyo. Na mimi sishuku kuwa wao wanatafuta ukweli.

 

 

 

Miongoni Mwa Utata Unaopingana Kwa Mashia.

 

 

Kwanza: 

 

Mashia wanaamini kuwa ‘Aliy ni Imamu aliyehifadhiwa ‘Ma’aswuum[1] , kisha tunamwona kwa kukiri kwao wenyewe kuwa amemuozesha mwanawe wa kuzaa Umu Kulthuum, dada wa Hasan na Husayn (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) amemuozesha ‘Umar bin Khatwaab (Radhwiya Allaahu ‘anhu) Na hili limethibitika kwenye vitabu vyao vyenye kutegemewa kwa Mashia, yaani: Kuthibitika kwa ndoa hii imeandikwa katika kitabu cha Kulayn kinachoitwa, ‘Al-Kaafi’ katika Juzuu ya Sita Uk. 115 na vile vile katika kitabu: “Tahdhiibul-Ahkaam” cha Tuus, na kitabu, “Al-Istibsaar”.

Vile vile na vitabu vingi vyenye kutegemewa kwa hiyo ikiwa ‘Aliy bin Abi Twaalib na yeye ni Imamu Ma’aswuum aliye hifadhiwa anamuozesha binti yake Umu Kulthuum dada yake Hasan na Husayn kwa ‘Umar bin Khatab. Kwa hiyo Mashia itawalazimu moja ya mambo mawili kila utamu wa mawili hayo ni uchungu.

 

 

Ya Mwanzo: ‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) sio Ma’aswuum, kwa kuwa amemuozesha mwanawe kwa kafiri, na hii inatengua misingi ya madhehebu ya Shia bali inaonyesha kuwa wengine miongoni mwa Maimamu sio Ma’aswuum.

 

 

Ya Pili: Inalazimika kuwa ‘Umar bin Al-Khattwaab ni Muislamu ambaye ‘Aliy ameridhia kumuozesha mwanae na kuwa mkwewe, na hili linapinga itikadi ya Shia, kwa kumkosoa kwake na kumkufurisha ‘Umar, na jawabu hizi mbili ndio msingi wa utata huu.

 

 

Utata Mwengine: Mashia wanadai kuwa Abu Bakr na ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) walikuwa makafiri, kisha tunaona kuwa ‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye ni Imamu Ma’aswuum ameridhia ukhalifa wao, kwa hiyo hili linalazimisha kuwa sio Ma’aswuum kwa sababu aliwabai’ (aliwapa mkono wa utiifu) makafiri na wala hakuwaasi, na alikiri ukhalifa wao, na jambo hili yaani! Kukubali kuwabai hawa makafiri wawili madhalimu – Allaah Atulinde – kuna vunja huko kuhifadhiwa – na ndani yake ni kusaidia udhalimu (dhulma). Na hili halitokei kwa Ma’aswuum abadani.

 

 

Ama jambo jingine: Ni kuwa kitendo cha ‘Aliy ni kitendo cha sawa wakati alipowabai’ Abu Bakr na ‘Umar kwa kuwa makhalifa hawa wawili walikuwa waumini, wa kweli waadilifu kwa hiyo Mashia katika hilo wanakuwa wamemkhalifu Imamu wao kwa kuwakufurisha na kuwatukana na kuwalani na kukosa kuuridhia ukhalifa wao. Na sisi wakati tunapojiuliza tunaangukia katika mshangao katika mambo yetu, ima tufate njia ya Abul Hasan na Husayn katika kuwasifu Makhalifa wawili, au tufuate njia ya Mashia wafuasi wake waasi ambao wanamtukana Abu Bakr na ‘Umar katika mema yao, na huu ni mushkeli tunaotaka ujibiwe!

 

 

Utata Mwengine: ‘Aliy alioa wanawake wengi baada ya kifo cha Faatwimah, na hapa tunataka tusikilize vizuri utata huu, na tunataka jawabu la wazi toka kwa wanazuoni wa Kishia. Ninasema: ‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) alioa wanawake wengi baada ya Faatwimah na wanawake wote hao  wamemzalia watoto mfano wao ni ‘Abbaas bin ‘Aliy bin Abi Twaalib, ‘Abdullaahi Bin ‘Aliy bin Abi Twaalib, Jaafar bin ‘Aliy bin Abi Twaalib, ‘Uthmaan bin Ali bin Abi Twaalib, hao wote mama yao ni mjakazi Binti Hizaam ni Daarim. Na hili limetajwa katika kitabu, ‘Kashful-Ghummah Fil Ma’arifatil – Aimmah’ cha ‘Aliy Al-Arbaly na huyo ni katika Maimamu wa wanazuoni wa Kishia, na pia yuko pia katika watoto wa ‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ‘Ubaydullah bin ‘Aliy bin Abi Twaalib na Abu Bakr bin ‘Aliy bin Abi Twaalib na huyu nae mama yao ni Laylaa bint Masuud Daaramiyah, hili pia amelitaja Al-Arbaly katika ‘Kashful-Ghummah’ Na pia yupo Yahya yaani: Miongoni mwa watoto wa ‘Aliy bin Abi Twaalib na Muhammad Al-Asghar na ‘Aun bin ‘Aliy bin Abi Twaalib na mama yao ni Asmaa binti Umaysi.

 

 

Pia yuko Ruqayyah binti Ali bin Abi Twaalib, yupo pia ‘Umar bin ‘Aliy bin Abi Twaalib na ‘Umar huyu alikufa akiwa na miaka thelathini na tano na huyu ni tumbo moja na Ruqayyah binti ‘Aliy bin Abi Twaalib na mama yao ni Ummu Hubayb binti Rabi’ah hilo pia amelitaja mwenye kitabu ‘Kashful Ghumah’.

 

 

Pia yupo Ummu Hassan binti ‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) na Ramlah Al-Kubraa binti ‘Aliy bin Abi Twaalib na mama yao ni Ummu Masuud binti Urwah bin Masuud Thaqafi. Swali na utata ambao tunataka ujibiwe na wenye wanazuoni wa Kishia ni, Je, inawezekana kwa mtu kuwaita wanawe kwa majina ya adui zake wakubwa? Awaite ‘Umar, ‘Uthmaan, na Abu Bakr? Hivi mtu mwenye akili atawaita wapendwa wake kwa majina ya adui zake? Je mnajua kuwa ‘Aliy bin Abi Twaalib ndie Mkureishi wa kwanza kuwaita wanawe kwa majina ya Abu Bakr na ‘Umar? Yeye ni Imamu ‘Aliy bin Abi Twaalib, kwa hiyo tunataka tutatuliwe mushkeli huu, na tunataka majibu sahihi ya wazi ili wana akili wa Shia wajue haki.

 

 

Utata Mwengine: Ndani ya kitabu cha ‘Nahjul-Balaaghah’ ukurasa wa 136, Na hicho ni kitabu cha kutegemewa kwa Mashia, imeandikwa kuwa ‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) alikataa ukhalifa, akasema: “Niacheni na tafueni Mwengine”, Imamu Ma’aswuum wa kwanza kwa Mashia anasema niacheni tafuteni Mwengine.

 

 

Nasema: Hii inaonyesha ubatilifu wa madhehebu ya Shia, kwa kuwa vipi anakataa ukhalifa na huu ukhalifa ni faradhi kutoka kwa Allaah tena ya lazima kama vitabu vya Shia vinavyodai, na vipi ‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) anaikataa nguzo ya kwanza kwa Mashia, nayo ni nguzo ya Uimamu? Anasema: ‘Niacheni tafuteni Mwengine?’

 

 

Utata Mwengine: Mashia wanadai kuwa Faatwimah (Radhwiya Allaahu ‘anha) ambaye ni Mtoto wa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) naye Bibi mtukufu. Mashia wanadai kuwa Bi-Faatwimah amedhalilishwa wakati wa uongozi wa Abu Bakr (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kiasi cha kuvunja mbavu yake wakati watu wakiunguza nyumba yake na kusababisha kutoka kwa mtoto wake kabla hajazaliwa ambae alikuwa alikusudiwa aitwe kwa jina la Al-Muhsin au Muhsin, swali tata ni kuwa ‘Aliy bin Abi Twaalib alikuwa wapi Bi-Faatwimah akifanyiwa haya yote? Alikuwa wapi Simba wa Masimba? Alikuwa wapi shujaa yule? Kwa nini hakuchukua haki ya mke wake Bi-Faatwimah (Radhwiya Allaahu ‘anha) binti wa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)? Hili ni tatizo na swali muhimu lapasa kujibiwa.

  

 

Utata Mwengine. Tumepata mengi kutoka kwa wakuu wa Kiswahaba wanaingiliana kwa kuoza na kuoa na si hivyo tu bali hata kinyume chake wameoana na Ahlul-Bayt (‘Alayhimus Salaam) Hususan Abu Bakr na ‘Umar, na hili limeafikiwa na wana historia na baina ya wenye kuhamisha habari kutoka kwa Sunni na kutoka kwa Shia, kuwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amemuoa ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anha).

 

 

Na vile vile amemuoa Hafswah bint ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhu) naye akamuozesha mwanawe Ruqayyah, Kisha Umu Kulthuum kwa Khalifa wa tatu Bwana mkarimu, mwenye staha ‘Uthmaan Bin ‘Affaan (Radhwiya Allaahu ‘anhu) na kwa ajili hiyo alipewa Laqab[2]  ya Dhuu Nurayn (mwenye nuru mbili).

 

 

Kisha mwanawe ‘Uthmaan bin ‘‘Affaan aitwae Abaan alimuoa Ummu Kulthum binti ‘Abdullaah bin Jaafar bin Abi Twaalib. Kadhalika Marwaan Bin Abaan bin ‘‘Uthmaan alimuoa Umul-Qasim bint Husayn bin ‘Aliy bin Abi Twaalib. Kadhalika Zayd bin Amri bin ‘Uthmaan alimuoa Salama binti Al-Husayn na ‘Abdullaah bin Amri bin ‘Uthmaan alimuoa Faatwimah bint Al-Husayn bin ‘Aliy bin Abi Twaalib (Radhwiya Allaahu ‘anhu).

 

 

Inatutosha kutaja Makhalifa watatu (Radhwiya Allaahu ‘anhum) bila ya kuwataja wengine. Swali linalojitokeza hapa ni kwa nini kukosolewa huku kwa Makhalifa hawa watatu peke yao? Na kwa nini kukoselewa hawa watatu tu na kudaiwa kuwa eti walikufuru na kuritadi”. Hata hivyo wanazuoni wa Kishia hawaweki wazi mbele ya wengine na mbele ya Waislamu isipokuwa wenye akili katika Mashia wanaojua kwa yakini kuwa wanazuoni wao wanamtukana Abu Bakr, ‘Umar, na ‘Uthmaan ndani ya Husayniyaat[3], basi ni kwa nini Maimamu wa Kishia wanawaozesha binti zao kwa watoto wa watu hao?

 

 

Ama waliowaita watoto wao kwa jina la ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhu) katika Maimamu miongoni mwao ‘Aliy kama tulivyotaja punde, alimwita mwanae ‘Umar Akbar na mama yake kama tulivyotaja ni Ummu Habiib binti Rabiiah, ‘Umar huyu aliuawa maeneo ya Karbalaa Tuff yaani katika usiku pamoja na ndugu yake Husayn (Radhwiya Allaahu ‘anhu) wala haitajwi kabisa kuwa ‘Umar alikufa kwa kuuawa –akiwa Shahidi – kwa Allaah, wala hatajwi katika maombolezo ya Husayniyaat wakati wa msiba wa Husayn na wakati wa kupokea taazia (rambirambi) ambayo inaitwa rambi rambi ya Husayn, hawamtaji ‘Umar.

 

 

Kadhalika Hasan bin ‘Aliy aliwaita wanawe majina ya Abu Bakr na’Umar na hili lipo katika vitabu vya Shia ‘Al-Irshaad’ cha Mufiid, ukurasa wa 194 na vile vile katika kitabu cha ‘Muntahal-Aamal’ Juzuu ya Kwanza ukurasa wa 240. Vile vile katika kitabu ‘Jalaaul-‘Uyuun’ cha Majlisy ukurasa wa 582. Kwa nini hawatajwi hao? Basi kwa nini wanawatukana hao (Radhwiya Allaahu ‘anhum) utata ni mwngi tutautaja hapa kwa haraka haraka.

 

 

Utata Mwengine: Kulayn ametaja katika kitabu chake, ‘Al-Kaafii’ sikilizeni vizuri, nasema: Kulayn ametaja katika kitabu chake, ‘Al-Kaafii’ kuwa Maimamu wanajua lini watakufa na kuwa wao hawafi isipokuwa kwa hiari yao, na hili limeandikwa katika ‘Usuulul- Kaafi’ cha Kulayn Juzuu ya Kwanza, ukurasa wa 258 Kulayn aliweka mlango kwa kauli yake, ‘Hakika Maimamu wanajua lini watakufa, na wao hawafi isipokuwa kwa hiari yao’.

 

 

Kisha akataja Majlisy katika kitabu chake ‘Bihaaru Al-Anwaar’ Juzuu ya 3, ukurasa wa 364, Anasema: “Hakika Maimamu wanajua lini watakufa. Na kuwa wao watakufa kwa hiari yao” na hili lipo katika, ‘Al-Kaafi’, Al-Majlis katika kitabu chake anataja hadithi inayosema: “Hakuna Imamu yoyote isipokuwa amekufa kwa kuuwawa au kwa sumu.” Na hapa kuna utata Mwengine tunasema: Ikiwa Imamu anajua ghaibu, kama alivyotaja Kulayn.

 

 

Na vile vile ametaja Al-Hurul Al-’Amily, ‘Kuwa iwapo Imamu huyu Ma’aswuum anajua ghaibu, kwa hiyo atajua kinacholetwa kwake, katika vyakula na vinywaji, na akijua kuwa chakula au maji kina sumu atajiepusha nacho. Na hapana budi ajiepushe nacho, na akila chakula hicho atakufa hali ya kuwa amejiua kwa kuwa yeye kwa itikadi ya Shia, anajua kuwa chakula hiki kina sumu akila atakuwa amejiua’. Na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema kuwa, “Mwenye kujiua mwenyewe ni mtu wa motoni”, Je Shia wanaridhia hili.

 

Kuhusu Imamu, nyinyi mnasema kuwa: “Imamu wanajua ghaibu, na wanajua lini watakufa.”  Majlisy anasema: “Hawi Imamu isipokuwa amekufa kwa kuuwawa au kwa sumu.”

 

Kwa hiyo akiletewa chakula nae anajua kina sumu akala, huku kutakuwa ni kumtukana Imamu huyu, kwani atahesabiwa ni punguani, na hali ya kuwa wao wametakaswa na hili. Kwa hiyo tunataka majibu ya mushkeli huu.

 

 

Utata Mwengine: Hasan bin ‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) alijiuzulu kwa Mu’aawiyah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) katika wakati  ambao wafuasi wakimnusuru walikuwa wakikusanyika kwake na kuunda jeshi na neema kukusanya itakayomuwezesha kuendeleza vita dhidi ya Mu’aawiyah katika hali hii ndugu yake Husayn alitoka kwa ajili ya kupigana na Yazid akiwa na watu wa chache katika familia yake, katika wakati ambao angeweza kujisalimisha. haiwezekani mmoja wao kuwa katika haki na mwengine kuwa katika batili, kwa sababu iwapo Hasan alijiuzulu pamoja na kuwa na nguvu na jeshi lenye kumuwezesha vita, kwa ukweli kutoka Husayn bila nguvu akiwa dhaifu pamoja na kuweza kwake kujisalimisha, hili lilikuwa ni batili na kosa kwake yeye Husayn kwa kuwa kama Husayn kutoka pamoja na udhaifu wake ni haki, basi kujiuzulu Hasan pamoja na nguvu alizokuwa nazo ni batili.

 

 

Na hili linawaweka Shia katika eneo wasilohusudiwa ndani yake, kwa kuwa wao wamesema: Hao wote Hasan na Husayn walikuwa katika haki, kiukweli ni kwamba wao wamekusanya mambo mawili yenye kupingana na kauli hii inavunja misingi ya Itikadi ya Shia kwani wakisema ubatili wa Hasani italazimika mbali wa Uimamu wake na wakisema ubatilifu wa Uimamu wake italazimu kubatilika Uimamu wa baba yake kwani ndie aliyemteua. Na yeye ndie aliemsimika baada yake kama Shia wanavyoitakidi, na kama hivi, na huu ni Mushkeli mkubwa inapasa wenye akili wa Kishia wafikirie.  

 

 

Mushkeli Mwengine: Kulayn ametaja katika kitabu chake (Al-Kaafii) Juzuu ya Kwanza ukurasa wa 239 ametaja Hadithi. Wametuhadithia wafuasi wetu wengi toka kwa Ahmad bin Muhamad kutoka kwa ‘Abdullaah bin Hajaan toka kwa Ahmad bin ‘Umar Al-Halabiy toka kwa Abi Basair amesema: Nilingia kwa Abu Abdillaah (‘Alayhis Salaam) nikamwambia: Nimekufanya mkombozi mimi na kuuliza mas-ala. Je, kuna yeyote anayesikia maneno yangu? Abu Abdillaahi akainua pazia lake, baina yake na nyumba nyingine akaangalia kitambo kisha akasema: ‘Ewe, Abu Muhamad uliza utakacho’. Nikasema, Mimi ni kombozi lako, kisha nikanyamaza kitambo kidogo, kisha akasema, kwa hakika kwetu kuna msahafu wa Faatwimah unajuaje Msahafu wa Faatwimah?

 

Nikamuuliza:

“Ni kitu gani hiki kinachoitwa msahafu wa Fatima?”

Akasema:

“Msahafu, ndani yake mna mfano wa Qurani yenu hii mara tatu! Wallahi hamna ndani yake yaliyomo ndani ya Qurani yenu hii hata herufi moja”.

 

Sikiliza vizuri, Imamu anaapa na kusema, ‘Wa-Allaahi hakuna herufi moja iliyomo kwenye Qur-aan yenu’ Nikasema: ‘Wa-Allaahi hii ni elimu’ akasema, ‘Ehee, Hakika hiyo ni elimu…’

 

Kwa hivyo: Je Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anajua msahafu wa Faatwimah? Kama alikuwa haujui basi ni vipi Ahlul Bayti waliweza kujua ilhali yeye hajui? Naye ni Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)? Na kama alikuwa anaujua ni vipi aliuficha dhidi ya Ummah wake na Allaah Anasema:

 

يَا أَيُّهَا الرَّسُولُ بَلِّغْ مَا أُنزِلَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ ۖ وَإِن لَّمْ تَفْعَلْ فَمَا بَلَّغْتَ رِسَالَتَهُ ۚ  ﴿٦٧﴾

Ee Rasuli! Balighisha yale yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Rabb wako. Na usipofanya, basi utakuwa hukubalighisha ujumbe Wake. [Al-Maaidah: 67]

 

Huu ni mushkeli mkubwa Enyi ndugu zangu tunataka jawabu.

 

 

 

Mushkeli Mwengine: Katika Juzuu ya Kwanza ya kitabu, ‘Al-Kaafii’ cha Kulayn kuna majina ya watu waliopokea Hadithi toka kwa Nabiy zinazotegemewa na Mashia Hadithi za Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na juu ya ali zake na Swahaba zake na amani, na wamepokea kauli za Ahlul Bayt miongoni mwao ni majina yafuatayo: hao ni wapokezi wa kitabu, ‘Al-Kaafi’ cha Kulayn watu waliopokea Hadithi za Shia, sikiliza vizuri majina na mnapata nini ndani yake? Mufadhal bin ‘Umar – Ahmad bin ‘Umar Halabi, ‘Umar bin Abaan ‘Umar bin Adhiinah – ‘Umar bin Abdil-Aziyz – Ibrahim bin ‘Umar –’Umar bin Handhalah – Musa bin ‘Umar – ‘Abbaas bin ‘Umar  na jina lililokusanya majina yote haya ni jina la ‘Umar ni sawa sawa kama ni jina la mpokezi au jina la baba yake.

 

Mushkeli ni kwa vipi hao wapokezi wataitwa kwa jina la ‘Umar nae ndie adui mkuibwa wa? Ahlul Bayt.

 

 

 

Mushkeli Mwengine: Allaah Anasema:

 

 ۗ وَبَشِّرِ الصَّابِرِينَ ﴿١٥٥﴾ الَّذِينَ إِذَا أَصَابَتْهُم مُّصِيبَةٌ قَالُوا إِنَّا لِلَّـهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ﴿١٥٦﴾
 

155. Na wabashirie wenye kusubiri. 156. Wale ambao unapowafika msiba husema: Hakika sisi ni wa Allaah na hakika sisi Kwake ni wenye kurejea. [Al-Baqarah:155-156]

 

na Anasema tena Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)

 

 وَالصَّابِرِينَ فِي الْبَأْسَاءِ وَالضَّرَّاءِ وَحِينَ الْبَأْسِ ۗ أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ صَدَقُوا ۖ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُتَّقُونَ ﴿١٧٧﴾ 

.Na wanaosubiri katika dhiki za ufukara na maafa ya magonjwa na njaa na katika vita. Hao ndio waliosadikisha na hao ndio wenye taqwa. [Al-Baqarah:177]

 

 

Subira ni jambo kubwa imetajwa katika Nahjul Balaaghah. Athari hii: ‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema baada ya kufa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akimhutubia yeye (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) Ali anasema kwa tamshi hili, ‘Lau usingekuwa umekata kubabaika na ukaamrisha subiri tungelia kwako maji ya Shani nyingi’

 

 

Hili limo katika (Nahjul Balaaghah) kadhalika katika (Al-Mustadrak) na imetajwa tena kuwa ‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: ‘Mwenye kupiga mapaja yake wakati wa msiba basi amali zake zimepotea’, hili limo ndani ya kitabu “Al Khiswaal) cha Sudduuk ukurasa wa 621 na katika kitabu, ‘Wasaail Shay Twaan’.Ali ndio Imamu wa mwanzo kwa Shia ana waonya wafuasi wake akiwaambia: Mwenye kupiga mkono wake wakati wa msiba juu ya  paja lake amani yake imeanguka, na vile vile Husain Imamu wa  zama zake na Imamu wa dunia (Radhwiya Allaahu ‘anhu) anamwambia dada yake Zaynab katika Karbalaa kama alivyopokea mwenye kitabu  ‘Muntahal Al-Aamaal’ kwa lugha ya Kifursi kimefasiriwa kwa lugha  ya Kiarabu kinapatikana katika juzuu ya kwanza ukurasa wa 248.

 

 

Husayn anasema: Na yeye ni Imamu wa tatu kwa Mashia akimuusia Dada yake Zaynab anasema: Ewe dada yangu, nakuapia kwa Allaah wajibu wako kuhifadhi kiapo hiki, nikiuwawa basi usichane nguo zako (kwa kulia),wala usiparure uso wako kwa kucha zako, wala usiomboleze maangamizi  juu ya Shahada yangu (Kufa kwangu Shahid) anamuapia Allaah.

 

Abu Jaafary Qamy amenakili: Kuwa amiri wa waumini (‘Alayhis-salaam) amesema katika ambayo wafuasi wake walikuwa anawausiana Hili  liko katika kitabu “Man laYahdhuruhul-faqiih” na vile vile katika kitabu, ‘Wasaail’ cha Harul Al-Aamily, na tukihitaji kuainisha utajo wake Al-Hurul Aamiliy katika,‘Wasaail Shiiah’ Juzuu ya pili ukurasa  wa, 916 Qamy ametaja ndani ya kitabu, ‘Man laYahdhuuruhul-Faqiih’ katika Juzuu ya kwanza ukurasa wa 232

 

Amiri wa waumini  anawajuza wafuasi wake na anasema: ‘Msivae nguo nyeusi kwa kuwa hiyo ni vazi la firauni msivae nyeusi kwa kuwa ni vazi la Firauni’ na  imekuja katika  tafsiri Swaafy katika kutafsiri kauli yake Ta’alaa: 

 

وَلَا يَعْصِينَكَ فِي مَعْرُوفٍ ۙ ﴿١٢﴾

Wala hawatakuasi katika mema…, [Al-Mumtahinah:12]

 

 

kuwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliwabai wanawake kuwa wasivae nguo nyeusi, wala wasichane nguo wala wasinadi maangamivu, bali katika kitabu (Furu’ul-Kaafiy) cha Kulayn kuwa yeye alimuusia Faatwimah (Radhwiya Allaahu ‘anha) akasema: “Mimi nitakapokufa usirarue uso, wala usiteremshe nywele wala usiniomboleze kwa maangamivu, wala usinisImamuishie maombelezaji” yaani usilete watu watakaoniomboleza kwa kupiga mayowe, na hili ni kama

lilivyotajwa katika kitabu, ‘Al-Kaafii’ Juzuu ya pili ukurasa wa 528.

 

 

Na huyu Sheikh wa Shia Muhamad bin Husain bin Babawayhi Al-Qamy aliyepewa jina la Suduuq kwa Mashia anasema: Katika matamshi ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ambayo  hayakutanguliwa ni: “Kuomboleza (An-Niyaaha) ni katika amali za Jahiliya” kama wanavyopokea wanazuoni wao, Majlisy An Nuury na wanazuoni wao wengi toka kwa Nabiy (Swalaah llwahu  alayhi Wasallam) kuwa amesema: “Sauti mbili zimelaaniwa Allaah anazichukia mayowe wakati wa Msiba (Yaani mayowe wakati wa msiba) na kughani wakati wa neema”

 

Swali na mushkeli ambao na wauliza wenye akili wa Mashia baada Ya riwaya zote hizi kwa nini Shia wanahalifu haki iliokuja na wanajipiga katika kumbukumbu yao katika Husainiyaat[3] kwa kujitoa damu na kupiga na kuchana mifuko? Sasa tumkubali nani tuwakubali wao au tumkubali Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Ahlul Bayt wake watoharifu (Radhwiya Allaahu ‘anhum).

 

 

Utata Mwengine:

 

Tatbiyr: Maana yake ni kujitoa damu kichwani kama wafanyavyo Shia katika Siku ya Ashura - nasema: Iwapo kujitoa damu na kujipiga vifua na kuchana nguo na kujiliza kwa sauti kuna ajira kubwa mbele ya Allaah, basi vipi Masheikh wenye kuvaa nguo nyeusi ambao ni kizazi cha Husayn (‘Alayhis- salaam) kama wanavyosema hawafanyi hivyo?  Iwapo hili lina ujira kwa nini wao hawajitoi damu, kwa nini hawajipigi na kwa nini hawajimwagii damu nyusoni mwao? Hilo halifanywi isipokuwa na hao masikini ambao wanadhani kuwa wako katika haki, na wao sio hivyo kwa nini hawafanyi hivyo? Tunawataka wenye akili wa Shia tuwaulize swali hili na wajibu swali hili.

 

 

Utata Mwengine: Ibada haiwi isipokuwa kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kujivunja na kujinyenyekeza katika daraja za kuabudu hakuwi isipokuwa kwa Allaah Ta’aalaa; Allaah Anasema: “Bali Allaah muabuduni” Na hapa kuna mushkeli, kwa nini Shia wanajiita mja wa Husayn (AbduHusayn), mja wa ‘Aliy (AbduAli), mja wa Zahraa (Faatwimah) na mja wa lmam? Kwa nini hawakujiita hivyo Maimamu Ma’aswuum kama Hasan, Husayn, Sajaad, Kaadhim, na Maimamu Ma’aswuum kwa Shia? Kwa nini hawakuwaita watoto wao au kwa nini yeyote miongoni mwao hakumwita mwanae mja wa ‘Aliy, mja wa Zahraan, Je inaswihi kuwa maana ya Abdul Husayn yaani: Mtumishi kama wanavyohalalisha baadhi ya Shia? Wanasema: Abdul Husayn maana yake, mtumishi wa Husayn, Je anakuwa mtumishi baada ya kufa kwa shahidi Husayn (Radhwiya Allaahu ‘anhu) inaingiaje akilini kupelekewa chakula na maji na kumiminwa maji ya udhu katika kaburi lake mpaka awe mtumishi kama wanavyohalalisha hao masheikh (Al-Mu’amamiin) kwa waumini wao hao maskini, hili halifai.

 

 

Utata Mwengine: Alipotawazwa ‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) hatukumuona kutofautiana na Makhalifa waongofu kabla yake, na kuchukia uongozi, hatukumuona akimhalifu Abu Bakr, wala ‘Umar wala ‘Uthmaan hakuwatolea watu Qur-aan zaidi ya ile iliyokuwa kwao na hakupinga chao chochote, bali kauli zake zilikuwa nyingi juu ya mimbari. ‘Kheri ya ummah huu baada ya Nabiy wake ni Abu Bakr na ‘Umar’ hakuhalalisha Mut-ah wala hakurudisha fadak, na hakuwahalalishia watu Mut-ah katika Hajj, wala hakuongeza haya njooni katika amali ya kheri –katika adhana wala hakuondoa – Swalaah ni bora kuliko usingizi– na kama Abu Bakr na ‘‘Umar wangekuwa makafiri walionyang’anya ukhalifa kwa Ali kama Shia wanavyodai, kwa nini hakulibainisha hilo aliposhika uongozi, na alikuwa na nguvu na ulinzi (Radhwiya Allaahu ‘anhu)! Kwa nini hakubainisha na alikuwa na nguvu mkononi mwake? Bali kwa ukamilifu tumemuona akifanya kinyume cha hayo yote, aliwasifu wote wa tatu, na kawataja kwa wema aliposema: “Bora ya ummah baada ya Rasuli wake ni Abu Bakr na ‘Umar” Nawaambia hao wenye akili, basi itoshe au itutoshe yale yaliowatosha nyinyi ‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) pale alipowasifu wale watatu, (Radhwiya Allaahu ‘anhum).

 

 

Utata Mwengine: Shia wanadai kuwa Mu’aawiyah alikuwa kafiri, kisha tunamuona Hasan bin ‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhuma) anajiuzulu ukhalifa na yeye ni Imamu Ma’aswuum, Imamu wa pili Hasan bin ‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhuma) anajiuzulu kwa ajili ya kafiri mpinga dini, na hili ni kinyume na ‘Ismah  kama mnavyodai au kuwa Mu’aawiyah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ni Muislamu aliyestahili muadilifu.

 

 

Mushkeli Mwengine: Ni kuhusu swali tunalolifikiria vizuri, na hiyo ni alama ya wazi kwa Shia kwa ujumla wake – Ithnaa ‘Ashariya (Maimamu kumi na mbili) swali linasema: Je, Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisujudia kijiwe (turbah) cha Husayn ambao Mashia wanasujudia hivi sasa? na udongo huo unaitwa turba Karbalaa? Je Nabiy alisujudia kijiwe kile?

 

Ikiwa wanazuoni wa Shia watasema: Ndio, tutasema: Huu ni uongo hili halikuthibitika toka kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Leteni dalili zenu ikiwa nyinyi mnasema kweli na kama watasema. Hakusujudu, na hili ni kweli, tutasema: Ikiwa hili ni hivi, je nyinyi ni waongofu zaidi kuliko Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)?

 

Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakusujudia kijiwe cha Husayn, basi kwanini nyinyi mnasujudia udongo kwenye udongo wa Husayn kwa nyuso zenu? Pamoja na kujua kuwa mapokezi ya Kishia yanataja kuwa Jibril (‘Alayhis-salaam) alikuja na kifumba cha mchanga wa Karbalaa na imekuja  katika baadhi ya athari, kuwa ardhi hii ni ambayo au imechanganyika na damu ya Husayn, au damu yake tohara (Radhwiya Allaahu ‘anhu) imechanganyika na udongo huu, hapo alilia kama zinavyosema riwaya, kwa hiyo kwanini basi Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)  hakuusujudia? Je, Shia wameongoka zaidi kuliko Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)? Utata huu unahitaji jibu.

 

 

Utata Mwengine: Shia wanadai kuwa Swahaba wa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) waliritadi baada ya mauti yake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na wakageuka baada Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) Swali: Je Swahaba walikuwa kabla ya mauti yake walikuwa ni Ithnaashariah kisha wakabadilika kuwa Sunnah iliyosImamuishwa?”Au wao kabla ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) walikuwa Ahlu Sunnah? Kisha wakabadilika kuwa Shia Ithnaashariah? Kwa kuwa kubadilika ni kutoka hali moja hadi nyingine tunataka jibu kwenye swali hili.

 

 

Walikuwa Waislamu kisha wakaritadi wakageuka wakabadilika kama zisemavyo riwaya za Shia, kuanzia zama za Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) Je Swahaba walikuwa Shia Ithna ‘Ashariyah, kisha baada yake wakabadilika kuwa ahlu Sunnah au walikuwa ahlu Sunnah na juu ya Sunnah ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na wakati huo ushia ulikuwa bado haujafahamika na kujitokeza? Tunataka jawabu katika hili.

 

 

Utata Mwengine: Inajulikana kuwa Hasan (Radhwiya Allaahu ‘anhu) yeye ni mtoto wa ‘Aliy na mama yake ni mwema Mtukufu Bi-Faatwimah (Radhwiya Allaahu ‘anha) Na yeye ni miongoni mwa watu waliofunikwa (nguo) ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa Shia na yeye vile vile ni katika Maimamu Ma’aswuum Shani yake katika hilo ni shani ya ndugu yake Husayn (Radhwiya Allaahu ‘anhu). Hapa kuna utata ambao tunataka utatuliwe: Kwa nini Uimamu umekatwa au kuzuiwa kwa watoto wa Hussan na ukaendelea kwa watoto wa Husayn? Baba yao ni mmoja mama yao mmoja na wote hao ni Mabwana, mabwana wa watoto wa vijana wa peponi, bali Hasan anamzidi Husayn katika jambo moja yeye amemzidi Husayn umri, na yeye ndiye mtoto wa kwanza kwa baba yake, kwa nini umekatwa na kuzuiwa kwa watoto wa Hasani  nakuwekwa kwa watoto wa Husayn (Radhwiya Allaahu ‘anhu)? Utata huu unahitaji majibu na ufafanuzi na uchambuzi wa kielimu.

 

 

Utata Mwengine: Kwa nini ‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) hakuswalisha Swalaah japo moja katika maradhi ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ambayo amekufa ndani yake ikiwa yeye ni Imamu wa baada yake kama mnavyodai? Na kuwa jambo hili ni msingi katika misingi ya dini, halina budi lijulikane kwa mapokezi ya Mutawaatir bali hili ni asili katika asili za dini, kwa nini ‘Aliy bin Abi Twaalib hakuswalisha Swalaah hata moja katika maradhi ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wala baada ya kutawafu kwake, kwanini hakuswalisha wala Swalaah moja? Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakumwamrisha ‘Aliy bin Abi Twaalib kuswalisha hata Swalaah moja, na Uimamu mdogo ndio dalili katika Uimamu mkubwa na huu ni mushkeli.

 

 

Utata Mwengine: Nyinyi mnasema: Sababu ya kupotea Imamu wenu wa kumi na mbili nae ni Muhamad bin Hasan Askary katika Saradib ni hofu ya dhulma, kama ilivyokuja katika riwaya zenu nyingi khofu ya dhulma basi kwa nini kupotea huku kunaendelea pamoja na kutoweka hofu hii, kwa kuwepo dola za Kishia kutawala kwa mujibu wa historia? Kama Dola Al-‘Abidiyiin Fatimiyah, Buwayhiiyiina, Swafin na mwisho ile dola ya Irani ya sasa ambayo nayo ina mitambo ya nyukilia, kwa nini asitoke hivi sasa? Na nyie mnasema ikiwa yeye hakujificha isipokuwa kwa hofu ya madhalimu na mashambulizi ya majabari, na zimekwishawahi kusimamia Dola za kishia jabari zenye nguvu, kwa nini asitoke sasa na kuna shia wenye nguvu wa kuweza kumnusuru, na kumlinda katika dola zao”? Bali kuwa mamilioni ambao wanajitoa roho zao kwa ajili yake asubuhi na jioni, tunataka majibu ya utata huu kwa nini hatoki?

 

 

Utata Mwengine: Kulayn ameandika mlango maalumu katika, ‘Al-Kaafii’ kwa anuani! “Hakika wanawake hawarithi chochote katika ardhi” Imepokewa ndani yake toka kwa Abu Jaafar amesema: “Wanawake hawarithi chochote ardhini wala katika ‘Iqari kitu chochote.” Hili ni katika juzuu ya Suba ukurasa wa 127 katika kitabu, ‘Al-Kaafii’ cha Kulayn.

 

Tunsi katika, ‘Tahdhib’ katika juzuu ya tisa ukurasa wa 254 toka kwa Maysarah kauli yake! Nilimuuliza Abu Abdillaah (a.s) kuhusu wanawake, nini haki yao katika urithi? Akasema, “Wao wanathamani ya tofali na jengo, mbao na Qaswab ama ardhi na ekari hawana chochote humo.”

 

Toka kwa Muhamad bin Muslim toka kwa Abu Jaafar amesema, “Wanawake hawarithi ardhi wala katika ekari”.

 

Na kutoka kwa Abdul Malik bin A’ayun toka kwa mmoja wao (‘Alayhis- salaam) yaani – mmoja wa Imamu Ma’aswuum kwa Mashia – amesema:wanawake hawana chochote katika (“Ad-Dar wal ‘Iqaar” Nyumba na mali isiyohamishika kama vile ardhi na mashamba nk.)” katika riwaya hii hakuna uhusisho au kufunga, si kwa Faatwimah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) wala kwa Mwengine, juu yahili haistahiki kwa Faatwimah (Radhwiya Allaahu ‘anha) kudai urithi wa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa mujibu wa riwaya ya Shia kwa kuwa Shia wanamkosoa Abu Bakr wanasema: kuwa yeye alinyang’anya urithi wa Fadak, au anachomiliki  Faatwimah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) katika mirathi yake katika Fadak  pia kila lililokuwa la Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hilo ni la Imamu zingatia kuwa imekuja katika riwaya za Kishia kutoka kwa Muhamad bin Yahya toka kwa Ahmad bin Muhammad toka kwa Amri bin Shammar toka kwa Jabir.

 

 

Toka kwa Jaabir kuwa Abu Jaafar (‘Alayhis Salaam) amesema: Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Allaah amemuumba Adamu akamkatia kipande cha dunia kwa hivyo lililokuwa la Adam (‘Alayhis- salaam) ni la Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na lililokuwa la Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni la Maimamu katika kizazi cha Muhammad.” Na hili pia liko katika ‘Usuulul Kaafi’ cha Kulayn ‘Kitabul Hujuh’ mlango kuwa ardhi yote ni ya Imamu (‘Alayhis-salaam) Juzuu ukurasa wa 476.

 

 

Imamu wa kwanza baada ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa mujibu wa Shia ni ‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwa hiyo mwenye haki ya kudai ardhi ya Fadak ni ‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu)  na sio Faatwimah (Radhwiya Allaahu ‘anha) na hatukumuoa ‘Aliy akifanya hilo, kwa hiyo tunataka jawabu kwa utata huu.

 

 

Utata Mwengine: Ahlu Sunnah na Shia walikubaliana pamoja na tofauti yao kuwa Ali ni shujaa asiyeshindwa na kuwa yeye hakuhofia lawama yoyote kwa ajili ya Allaah. Na ushujaa huu haukukatika hata mara moja tangu mwanzo wa uhai wake mpaka alipouliwa kwa mkono wa Bin Muljam. Na Shia kama inavyojulikana wanatangaza kuwa ‘Aliy bin Abi Twaalib yeye ni wasii baada ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) bila upambanuzi wowote nae ni wasii wa moja kwa moja baada ya Nabiy bila ya utata wowote.

 

 

Nasema: Hapa kuna utata! Je ushujaa wa ‘Aliy ulikoma baada ya kufa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) mpaka Ambay-‘i (Ahadi ya Utiifu) Abu Bakr kisha Ambay-‘i (Ahadi ya Utiifu) baada yake ‘Umar kisha baada yake ‘Uthmaan bin Afaan, (Radhwiya Allaahu ‘anhu) Je alishindwa japo mara moja katika minbari na akaogopa kupanda japo mara moja na kusema kuwa ukhalifa umeporwa kwake yeye, na kuwa yeye ndie mwenye haki, kwa nini hakufanya hivyo? Na yeye ndie wasii wa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na kwanini hakudai haki yake?Na yeye ndie yule shujaa ajulikanae na yeye alikuwa na wafuasi wengi wa kumnusuru wanaompenda, ambao watajazana pembeni yake la angelisema katika mimbari ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)? kwa nini hakufanya hili (Radhwiya Allaahu ‘anhu)?

 

 

Utata Mwengine? Hadithi ya Kisaai (shuka iliyowafunika watu wanne katika familia ya ‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) na kuwasifu kwao kwa utoharifu. Wanne hao ni ‘Aliy, Faatwimah, Hasan na Husayn (Radhwiya Allaahu ‘anhum) wote. Swali, ni ipi dalili ya kuwaingiza wengine katika utoharifu wa uhifadhi (‘Ismah) ikiwa Hadithi ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) iko wazi kwa kuwa toharisha hao wanne, katika nyumba ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na ‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) Faatwimah, Hasan, na Husayn (Radhwiya Allaahu ‘anhu) wote? Basi ni ipi dalili ya kuwaingiza wengine katika utoharifu na Ismah na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakuweka wazi isipokuwa katika hao wanne tu? Hili ni tatizo, tunataka jibu lake.

 

 

Utata Mwengine: Shia wanapokea toka kwa Imamu Jaafari As-Swadiq (Radhwiya Allaahu ‘anhu) nae ndio Muasisi wa madhehebu ya Jaafariyah kwa mujibu wa itikadi yao kauli yake akijifakhirisha anasema: Abu Bakr amenizaa mara mbili, mwangalie vizuri Jaafar As-Swadiq Imamu Ma’aswuum kwa Shia anasema! Abu Bakr amenizaa mara mbili, na hili lipo ndani ya kitabu cha, ‘Kashful-ghummah’ cha Al-Arbaly Juzuu 2 ukurasa wa 373, amesema: Abu Bakr amenizaa mara mbili, kwa vile nasaba yake kwa Abu Bakr imekoma kwa njia mbili ya kwanza: Kwa njia ya mama yake. Faatwimah binti Qasim bin Abu Bakr ya Pili: Kwa njia ya bibi yake kwa mama yake Asmaa bint Abdi Rrahman bin Abu Bakr ambae yeye ni mama yake Faatwimah binti Qasim bin Muhammad bin Abu Bakr, kisha tunapata Shia wanapokea kwa Jaafar As-Swaadiq riwaya za uongo za kumtukana baba yake Abu Bakr (Radhwiya Allaahu ‘anhu) hili litakuaje? Swali Vipi Swaadiq atajifakhiri kwa babu yake upande mmoja? Na kisha kumtukana kwa upande Mwengine?!!

 

 

Maneno haya yanaweza kutoka kwa mtu mjinga lakini hayawezi kutamkwa na Imamu ambaye Shia wanamzingatia kuwa msomi zaidi katika wakati wake. Kwa hiyo tunataka mkajibu juu ya mushkeli huu.

 

 

Utata Mwengine: Shia wanadai kuwa ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhu) anamchukia ‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu). Wanazuoni wa Kishia wanadai katika Husayniyaat zao, kongamano na vikao vyao wanasema kuwa: ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhu) anamchukia ‘Aliy chuki kubwa mno, pamoja na hili tunapata kuwa ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhu) anatawalisha ‘Aliy Madiynah wakati alipotoka kupokaa funguo za Baytil Maqdis. Vipi yatakuwa haya? ‘Umar anamchukia ‘Aliy wala hampendi, na alipotoka ‘Umar kupokea funguo za Baytil Maqdis alimtawalisha Madiynah, naye ni ‘Aliy bin Abi Twaalib ambae hampendi na anamchukia sana, na kujua kuwa ‘Aliy atakuja kuwa Amiri wa Waislamu katika hali itakayomtokea ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwa makuruhu yoyote yale. Yaani: Lau ‘Umar angeuwawa (Radhwiya Allaahu ‘anhu) Ni nani ambaye angekuwa Khalifa wa Waislamu. Bila shaka angelikuwa ‘Aliy aliyepewa Uamiri wa Madina, Hili litakuwaje? Sasa vipi Shia wanadai kuwa ‘Umar bin Khatwab (Radhwiya Allaahu ‘anhu) anamchukia ‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kisha tunamuona ‘‘Umar anamtawalisha ‘Aliy uamiri wa Madina? Tunataka jawabu juu ya mushikeli huu.

 

 

Utata Mwengine: Sikilizeni vizuri enyi Mashia wenye akili. Wanazuoni wa Shia wanaona kuwa viungo vya Swalaah ni vinane, paji la uso, pua, viganja viwili, magoti mawili, nyayo mbili, na viungo hivi vinapasa kugusa ardhi katika hali ya kusujudu na haya yametajwa katika kitabu cha, ‘Wasaail Shiah’ cha Hurul Al-Aamily Juzuu 3 ukurasa wa 598, kadhalika wanasema uwajibu wa kusujudu juu ya kisicholiwa wala kuvaliwa, kwa ajili hii wanaweka Turbah chini ya maji ya nyuso zao, chini ya kiungo kimoja katika viungo hivi nane. Swali: Kwa nini Shia hawaweki Turbah iliyochanganywa na damu tukufu ya Husayn chini ya viungo nyote vya kusujudu? Kwa nini wameukhusisha uso peke yake katika kusujudia udongo huu wa Karbalai?

 

 

Na hali yakuwa nyinyi mmeamrishwa kusujudu juu ya viungo vyote vinane, paji la uso, pua viganja, nyao, na magoti. Kwa nini uso tu mlio wameukhusisha na huu udongo wa Husayn Karbalaai? Na hakuna dalili ya kuhusisha? Huku ni kupingana!  Na utata huu tunataka jawabu.

 

 

Imekuja katika baadhi ya riwaya za mushkeli Mwengine mfano wa kitabu  (Al-Ghiibah) katika kitabu, ‘Al-Ghibah’ cha At-Tuusi: Kuwa Shia –wanadai katika baadhi ya riwaya kuwa Mahdi wao wa kumi na mbili ni Muhammad bin Hasan Al-Askari atakapo tokea katika Sirdaab yake Akhir Zamaan (Mwisho wa zama) hakika huyo atahukumu kwa hukumu ya watu wa Dawuud.

 

Utata: Iko wapi shari’ah ya Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) yenye kufuta sheria zote zilizotangulia? Kwa nini anahukumu kwa sheria ya watu wa Daudi? Na shari’ah ya Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) iko wapi?

 

 

Utata Mwengine: Sikilizeni vizuri, Shia wanaitikadi kuwa Imamu wanabebwa na mama zao katika mbavu zao na kuzaliwa kwa mapaja yao ya kulia, kama alivyotaja Mas-uudi katika kitabu chake, “Ithbaat Al-Wasiyah” ukurasa wa 196: ‘Maimamu wanabebwa kwenye mbavu za mama zao na kuzaliwa kwenye mapaja yao ya kuume’ hapa kuna mushkeli na swali! Muhamadi si ndio bora ya Rusuli wa mtukufu wa Imamu na ni Mtukufu zaidi kuliko yoyote aliyewahi kukanyaga kwa unyayo wake ardhi hii (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).  Yeye ndiye bora wa hao wote, kwa jambo gani alibebwa kwa tumbo lake na kwanini ametoka kwenye Mfuko wake wa uzazi? Kwa nini yeye hakutokea kwenye paja la mama yake la kulia?’ Huu ni utata unabainisha ghuluwi (kuvuka mipaka) na kupingana kwa kauli zao katika madhehebu hayana itikadi hii, tunataka jawabu la wazi la kielimu lenye kukata.

 

 

Utata Mwengine: Shia wamepokea kuwa Abu AbdiIlaah Jaafar Swaadiq amesema: Mwenye jambo hii ni mtu hamwiti kwa jina lake isipokuwa Kafiri  na hili liko katika “Al-Anwaar An-Nuumaniyah’ na imepokewa kwa Abu Muhammad Hasan Al-Askary kuwa amesema kwa mama yake Mahdi: “Utabeba mimba ya mtoto wa kiume, na jina lake Muhamad yeye atasImamua baada yangu”  Je, huu sio mvutano hili limetajwa katika, ‘Al-Anwaar An-Nuumaaniyah’ ukurasa wa 55 Juzuu ya Pili yaani baada ya kurasa mbili za hadithi ya kwanza, kwa kuwa Hadithi ya kwanza ipo Juzuu ya Pili ukurasa wa 53. Na hivi sasa katika riwaya ya kwanza Abu Abdillah Jaafar Swaadiq anasema: Mwenye jambo hili ni mtu hamwiti kwa jina lake isipokuwa Kafiri.Yaani: Hatataja jina lake isipokuwa kafiri. Na tunaona kuwa Abu Muhamad Hasanal-Askary amesema akimwambia Umu Mahdi: Utabeba mimba na jina lake Muhamad naye atasImamua baada yangu, je huu sio mgongano? Mara mnasema: Mwenye kumwita kwa jina lake kafiri, na mara nyingine mnasema kuwa Hasan Askary alimuita kwa jina hilo Muhamad, Huu ni utata tunataka majibu.

 

 

Utata Mwengine: Na swali jingine, lau mtu anataka kuwa Shia, Lau mimi nataka kuwa Shia hivi sasa ni madhehebu gani ambayo nitayafuata, au ni madhehebu yepi ninanayopaswa kuyafuata kati ya madhehebu mengi ya Kishia? Baina ya Imamuia Ismailiyah, kwa tofauti zao nyingi; Ismailiya Arkani au Ismailiya Mukarima au baina ya Ismailiya Buhrah na Ismailiya Nasiiriyah, au baina ya ‘Alawiya na Zaidiyah, au baina ya Duruuz, na makundi mengi ya Kishia. Kwa hiyo ni kundi lipi la Shia ninaloweza kulifuata, na kuliamini kwani yote yanajinasibisha kwa watu wa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Na wote wanakubali Uimamu wa ‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) na wote ni adui wa Swahaba na wote wanaitakidi Uimamu wa ‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) na kuwa yeye ni nguzo na kuwa yeye ni khalifa baada ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)  bila mwanya wowote ule, na kuwa pamoja nao wana asili ya dini na wanasifu Maimamu kwa hiyo ni  madhehebu gani nitakayoyafuata? Imamuiyah Ithnaashariah? Au Ismailiya kwa aina zake au Naswiiriya Alawiyah? Au Duruuz katika baki ya Fatimiyah? Haya yanahitaji ithbaati.

 

 

Utata Mwengine: Wakati Shia wanapotaka kuthibitisha Uimamu wa Ithnaashariyah wao wanatoa dalili ya Hadithi ya Kisaai ambayo Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametaja watu wanne tu swali: Faatwimah ametajwa kwa Hadithi Sahihi kwa uwazi kwanini amewekwa mbali na Uimamu na wala hatajwi katika Maimamu wa kishia? Hao wametajwa amesema (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ‘Aliy na Faatwimah Hasan, Husayn kwanini mmemtoa Faatwimah katika Imamu kumi na mbili? Huu ni mushkeli unataka jawabu.

 

 

Utata Mwengine: Kwa nini Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakupiga makofi alipokufa mwanae Ibrahimu? Kwa nini hakujipiga kama wanavyojipiga Shia, Mashia wanajipiga katika msiba wa Husayn na katika Husayniyaat zao? Na kwa nini ‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) naye ni Imamu Ma’aswuum wakati wa kufa Faatwimahh (Radhwiya Allaahu ‘anha) Kwanini hakujipiga? Hakujiparuza, wala hakujitoa damu? Hakupiga Qaamaati kwa minyororo au kwa mikono yake, kwa nini hakufanya haya na hiyo ni dini na hakuna budi itekelezwe? Tunataka jawabu juu ya huu utata.

 

 

Utata Mwengine: Shia wanaitakidi kuwa Swahaba wengi walikuwa makafiri  na wanafiki walioritadi isipokuwa wachache, na hili wanalolisema wengi wa katika wanazuoni wa kishia (Al-Mu’amamiyn – wenye vilemba), katika itikadi zao, na Mashia wenye akili wanakiri haya yote, ikiwa Swahaba waliriadi isipokuwa wachache mno miongoni  mwao kuna waliokuwa wanafiki na baada ya mauti ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) isipokuwa watu saba tu, kwa sababu katika vitabu vya Shia kikiwemo  cha Kulayni kuwa Swahaba waliritadi isipokuwa saba kwa hiyo waumini ni saba au kwa uchache wa hali ni wachache mno, kwa hiyo basi kwa nini basi hao walioritadi wasiwavamie na kuwashambulie hao wachache wanyonge, na kuwauwa wote? Na kwa nini basi hali haikurudi kwenye ukafiri na ujahiliya kama walivyokuwa babu zao na baba zao? Kwa nini hawa Swahaba hawakufanya hivi? Nyinyi mnasema hao waliritadi na kuwa wao ni wanafiki walingojea mauti ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kisha wakaritadi wakamkufuru Allaah, wakarudi  basi kwanini hawakurudi kwenye  dini za baba zao Majahilia wa mwanzo, na kwanini hawakuwaua wale wachache waliobaki na imesemwa walikuwa saba au zaidi kidogo, hili linataka jawabu enyi Shia wenye akili,

 

 

 

 

Utata Mwengine: Shia wanasema: Kulia juu ya Husayn ni Sunnah. Je, kulia huku kumejengwa juu ya dalili au hawaa (matamanio ya nafsi)? Ikiwa ni kwa dalili basi iko wapi dalili hiyo? Hili jambo moja, iko wapi hiyo dalili inayojuzisha kumlilia Husayn tukijua Husayn alimuusia dada yake asimlilie kwa kupasua nguo wala asijipige wakati Husayn atakapokufa. Dalili hiyo iko wapi? Kisha mbona hajafanya hivyo yeyote miongoni mwa Maimamu wa Ahlul Bayt ambao mnadai kuwa mnawafuata na mnaenda juu ya uongofu wao, tunataka jawabu.

 

 

Utata Mwengine: Shia wanaamini kuwa ‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ni bora kuliko mwanae Husayn, na iwapo hali iko hivyo ni kwa nini hamumlilii kwa kukumbuka mauaji yake kama ambavyo mnalia kwa Husayn, nae aliyeuawa kama alivyouwawa Husein kwa nini hamlii kwa ajili ya Nabiy  (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) mkajitoa damu mkajipa na kutoa rambi rambi kwa ajili ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)?  Na yeye ni mtukufu wa wote? Na yeye ameuwawa kwa kupewa sumu na Mayahudi. Kwa nini msiba wenu huu mnauita Husayniyaati kwa nini msiunasibishe kwa Imamu wenu wa kwanza ‘Aliy na ukaitwa, ‘Alawiyaati au Muhammad ukaitwa, ‘Muhamadiyaati’ kwa nini mnaunasibisha kwa Husayn (Radhwiya Allaahu ‘anhu)? Kwa nini hamfanyi Husayniyati aina nyingi au sehemu za kupokea rambi rambi, kama mnavyouita kwa Husayniyaati iteni ‘Alawiyaati, iteni Muhamad yaani iteni kwa majina ya Maimamu. Kwa nini hamfanyi hivyo.

 

 

 

 Utata Mwengine: Iwapo Uimamu wa ‘Aliy ni Uimamu wa wanawe baada yake nguzo ambayo haikamiliki imani ila kwa imani hiyo. Na aliyeamini hivyo amekufuru na anastahiki Jahanamu, kama hilo lilivyokuja katika vitabu vya Maimamu wa Kishia hata kama atashuhudia “Laailaa illa llah na Muhamad Rasuulullaahi” akasimamisha Swalaah akatoa Zakaah akafunga mwezi Ramadhani na akahiji nyumba Tukufu kama wanavyoitakidi Shia, basi kwanini nguzo hii kubwa hatuioni iko wazi katika Qur-aan Tukufu? Iwapo jambo hili kwa utukufu wake na katika dini hii kuwa ambae hataleta Uimamu basi hatanufaishwa na Swalaah, Swawm, Zakaahah wala Hajj wala hata Shahadah mpaka aamini juu ya Uimamu, kwa hiyo masuala haya kwa ukubwa wake kwa nini hayakutajwa katika Kitabu cha Allaah wazi wazi?

 

 

Wakati ambao tunaiona Qur-aan  Tukufu kuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) mengine ameyaweka wazi katika nguzo na wajibu ambao huo sio Uimamu kwa Mashia, kama Swalaah Zakaah, Swawm na Hajj, bali (Subhaanahu wa Ta’aalaa)  ameweka wazi katika Qur-aan baadhi ya Mubahaat (yaliyoruhusiwa), kama kuwinda kwa mfano kwa hiyo iko wapi nguzo kubwa? Uko wapi uzito mkubwa? Na huo ni Uimamu kwa nini haujaletwa wazi katika Qur-aan? Ikiwa ni kwa kiwango hiki cha utukufu. Na umuhimu wake mkubwa katika dini ya Allaah. Tunataka jawabu juu ya hili.

 

 

 

Utata Mwengine: Shia wanaitakidi kuwa Qur-aan imeondolewa baadhi ya Aayah na imebadilishwa baadhi ya Aayah wakati wa Abu Bakr na ‘Umar. Wanapokea kwa Abu Jaafar kuwa aliambiwa: Kwa nini ‘Aliy aliitwa Amirul Muumiinina? Alijibu: Allaah ndio aliomwita na hivi ndivyo alivyoshusha katika kitabu chake,

Na pale Mola wako Alipowaleta katika wanaadamu kutoka migongoni mwao kizazi chao, na akawashuhudisha juu ya nafsi zao, akawaambia: Je, Mimi si Rabb Mlezi wenu? Na ya kuwa Muhammad ni Mtume wangu na ‘Aliy ni Amiri wa Waumini Hili ni limo katika usuul Al-Kaafii” (1:412)

 

Kulayn anasema katika tafsiri yake ya Aayah, “Basi wale walio muamini yeye” (7:157) yaani: Maimamu,

 “na wakamhishimu, na wakamsaidia, na wakaifuata nuru iliyo teremshwa pamoja naye - hao ndio wenye kufanikiwa”[7:157] yaani! ambao wamejiepusha masanamu kuyaabudu hii ni kauli ya Kulayni, kisha anasema Jibti na Twaghuti ni fulani na fulani.

 

 

Hili limo ndani ya Al-Kaafii ukurasa wa 429 Angalia katika kitabu cha Al-Kaafii hakutaja majina ya haya Matwaghuti mawili kwa sababu Al-Kulayn, (mwandishi wa kitabu hicho) alikuwa wakati wa udhaifu na unyonge; yeye ni Muhamad bin Yakub Al-Kulayni akasema – fulani na fulani wakati ambapo Al-Majlisiy Sheikh wa dola ya Swafawiyah katika wakati wa nguvu na ulinzi alisema katika kitabu chake, “Bihaar-ul-Anwaar’ Juzuu 23 ukurasa wa 306, ‘Muradi wa Fulani na Fulani ni Abu Bakr na ‘Umar. Na hivi ndivyo Al-Majlisiy alivyoona kuwa ‘Umar na Abu Bakr ni mashetani, Allaah atukinge. Imekuja kaika tafsiri yake kwa kauli yake Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَلَا تَتَّبِعُوا خُطُوَاتِ الشَّيْطَانِ ۚ إِنَّهُ لَكُمْ عَدُوٌّ مُّبِينٌ ﴿١٦٨﴾

Wala msifuate hatua za shaytwaan. Hakika yeye kwenu ni adui wa wazi. [Al-Baqarah:168]

 

 

wamesema: Hatua za shetani Wa-Allaahi ni utawala wa fulani na fulani. Na imepokewa kuwa Abu ‘Abdillaahi amesema:

 

“Na mwenye kumtii Allaah na Nabiy wake katika utawala wa ‘Aliy hakika huyo amefuzu kufuzu kukubwa”

 

Amesema: Hivi ndivyo ilivyoshuka, hili limo ndani ya “Usuul-ul-Kaafi” Juzuu ya Kwanza ukurasa wa 314.

 

Kadhalika imepokewa kwa Abu ‘Abdillaahi (‘Alayhis Salaam) amesema: Jibrili ameshuka kwa Muhamad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na ali zake kwa aya hizi,

 

“Enyi mliopewa kitabu aminini yaliyoteremshwa kwa ‘Aliy ni nuru ilio wazi” angalia vizuri “kwa Ali nuru ya wazi” hili limo ndani ya “Usuulul Kaafi” Juzuu ya Saba ukurasa wa 66.

 

 

Athari na Hadithi ni nyingi katika kuwatusi Mashaykh wawili na kuwa wao walipondoa na waliibadilisha kitabu cha Allaah. Hapa kuna swali au mushkeli kwa Mashia, mimi nalipeleka kwa Mashia wenye akili ili watafiti ndani yake. Ikiwa Abu Bakr na ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhum) wamepondoa Kitabu cha Allaah katika Aayah hizi, basi kwanini ‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) hakuzinyoosha baada ya kuwa Khalifa wa Waislamu kwa kuweka wazi jambo hili. Kwa nini hakusema wakati wa ukhalifa wake na nguvu zake, na baada ya kufa Abu Bakr na ‘‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwa nini hakusema: Abu Bakr na ‘Umar wamepondoa na kuibadilisha Quran hii, na usawa ni kadha wa kadha katika dini ya Allaah Ta’aalaa?

 

 

Kwanini hakuzirudisha Aayah hizi katika Qur-aan kama zilivyoteremshwa? Hili ni wajibu kwake, bali hili ni faradhi katika faradhi zilizo juu yake kurudisha yaliyopondolewa na kubadilishwa katika aya za kitabu cha Allaah Taalaa baada ya mauti ya Abu Bakr na ‘Umar ambao wamepondoa hiki kitabu kama wanavyoitakidi wanazuoni wa Shia, kwa nini hakufanya hili (Radhwiya Allaahu ‘anhu) hili linahitaji jawabu.

 

 

 

Utata Mwengine: Abul Faraj Al-Asfahany ametaja katika “Maqaatil Twaalibiyn” ukurasa wa 88, 142 na 188 chapa ya Beiruti na Al-Arbaly pia imetajwa hivyo katika ‘Kaashiful-Ghummah’ Juzuu 2 ukurasa wa 66 na Majlisy katika, Jalaa-ul-Uyuun ukurasa wa 582 kuwa Abu Bakr bin ‘Aliy bin Abi Twaalib alikuwa ni miongoni mwa waliouawa katika Karbalaa angalia vizuri hao watatu ni wanazuoni wa Kishia wametaja katika vitabu vyao kuwa Abu Bakr bin ‘Aliy bin Abi Twaalib ni miongoni mwa waliouwawa katika Karbalaa pamoja na ndugu yake Husayn (Radhwiya Allaahu ‘anhu) na vile vile ameuawa pamoja na mtoto wa Husayn bin ‘Aliy ambae jina lake ni Muhamad Al-Asghar aliyekuwa maarufu kwa kun-ya Abu Bakr wote hao waliuawa pamoja na Husayn.

 

 

Utata na Swali: Kwa nini Shia wanaficha jambo hili kwa wafuasi wao? Kwa nini Shia wanazuoni wao wanaficha jambo hili kwa wafuasi wao wala hawatilii mkazo isipokuwa kifo cha Husayn? Je ni kwa kuwa majina yao ni Abu Bakr na wao daima wanatoa dalili ya ukafiri wa mtu huyu (Radhwiya Allaahu ‘anhu) tunataka jawabu la swali hili.

 

 

 

Utata Mwengine: Ilikuwa katika zama za Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuna watu wanaomuona Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) mara moja katika maisha yao, kisha wanaenda kwenye miji yao, na hili limepokewa kwa njia mutawaatir katika vitabu vya Ahlu Sunnah na Shia anakuja Swahaba au mtu anamwona Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) mara moja kisha anarudi wala hamuoni tena baada ya hapo, na hao ambao hawakumuona Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) mpaka akafa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) mara au akafa yeye hao hawakusikia uongozi wa ‘Aliy wala wanawe na wajukuu zake mimi nauliza! Je Uislamu wao ni pungufu. Wanazuoni wa Shia wakisema: Ndio tunawaambia: Lau ni hivyo Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) angestahiki zaidi kusahihisha Uislamu wao, na angewabainishia  jambo la Uimamu katika kikao cha kwanza ili wasije wakafa na hali ya kuwa wao wameacha nguzo ya Imamuah, hiyo nguzo kubwa, haifai kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)  afiche nguzo hii muhimu na hali ya kuwa anajua huyu yu mchungaji  au huyo ‘bedui’ atarudi kwenye miji yao na hatarudi tena kabisa, hatujamuona Nabiy akifanya hivyo, na hili linathibitisha na kuonyesha kuwa Immah sio nguzo katika nguzo za dini hii.

 

 

 

Utata Mwengine: Ulamaa wa Shia hawawezi, na mimi siongei na Shia wa kawaida, kwa kuwa Shia wa kawaida ni watu wenye kufuata tu na miongoni mwao kuna wengi wenye ikhlasi na ukweli na mimi ninapoelekeza maneno yangu nayaelekeza kwa wajuzi wanaowaathiri watu wa kawaida nasema: Shia (wanazuoni) hawawezi kukataa kuwa Abu Bakr ‘Umar, ‘Uthmaan, walimbai’ Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) chini ya mti na kuwa Allaah Taalaa ameeleza katika Qur-aan kuwa amewaridhia na amejua yalio nyoyoni mwao kadhalika. Allaah Anasema,

 

لَّقَدْ رَضِيَ اللَّـهُ عَنِ الْمُؤْمِنِينَ إِذْ يُبَايِعُونَكَ تَحْتَ الشَّجَرَةِ فَعَلِمَ مَا فِي قُلُوبِهِمْ فَأَنزَلَ السَّكِينَةَ عَلَيْهِمْ وَأَثَابَهُمْ فَتْحًا قَرِيبًا﴿١٨﴾

Kwa yakini Allaah Amewawia radhi Waumini walipofungamana nawe ahadi ya utiifu (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) chini ya mti, (Allaah) Alijua yale yaliyomo nyoyoni mwao; basi Akawateremshia utulivu, na Akawalipa ushindi wa karibu. [Al-Fat-h:18] 

 

 

Kwa hiyo Allaah anawaridhia hata hao watatu, na amejua yalio nyoyoni mwao miongoni mwa imani, tauhidi na ukweli na usafi na basi vipi itafaa kwa wanazuoni wa Kishia baada ya hapo, kukufuru habari ya Allaah alioitoa katika Qur-aan, na kudai kinyume chake ni kama kwamba wanasema, Ewe, Rabb wewe hujui kitu kutoka kwao kama tujuavyo sisi, sisi tunajua kuwa wao ni Wazandiki na tunajua ya kuwa wamebadilisha dini, tunajua ya kwamba wamepotosha dini hii, nawe hujui haya yote’ Allaah atukinge na hili na huu ni mushkeli unaotaka majibu.

 

 

Utata Mwengine: Mara nyingi mara kwa mara wanazuoni wa Kishia wamekuwa wakitaja katika kueleza mauaji ya Husayn (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kuwa amekufa akiwa na kiu kikali, katika vita na imekuja katika baadhi ya riwaya kwamba alikuwa akisema, “Enyi Shia wangu kila mnywapo maji ni kumbukeni kwa kila mnywapo maji ni kumbukeni” na kwa ajili hiyo utaona Shia wanaandika katika mabirika na mafriji ya maji ibara ifuatayo: “Kunywa maji na kumbuka kiu cha Husayn” Haya ni maneno mazuri.”

 

 

Swali na Mushkeli kwa wakati huo huo, madamu Maimamu kwa mujibu wa ufahamu wa Shia wanajua ghaibu, je hilo halikuwa katika uwezo wa kujua kuwa atahitaji maji katikati ya vita? Hakuwa akijua pengine atakufa kwa kiu?  Kwa hiyo angehitaji kukusanya kiasi kikubwa cha maji kwa ajili ya kujitosha kwa vita, kwa nini hakufanya hilo? Hili linahitaji jibu.

 

 

Utata Mwengine: Dini ya Uislamu ilikamilika wakati wa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa kauli yake Subhaanahu wa Ta’alaa: 

 

الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ﴿٣﴾

Leo nimekukamiliishieni Dini yenu.. [Al-Maaidah:3]

 

Na madhehebu ya Shia yamedhihirika baada ya kufa Nabiy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) tunataka jawabu sahihi la kielimu na uthibitisho wa kielimu juu ya jambo hili Allaah Anasema: Leo nimekukamiliishieni Dini yenu [Al-Maaidah:3] na madhehebu ya shia ilisImamua baada ya kutawafu Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) Je, tutatatuaje tatizo hili?

 

 

 

Utata Mwengine: Ikiwa ‘Aliy na wanawe wana miujiza hiyo ambayo inapokewa katika vitabu vya Shia kuwa miujiza hiyo inawanufaisha na hata sasa inawanufaisha na wao hata kama wamekufa kama wanavyodai kuwa wao wana miujiza, ‘Aliy bin Abi Twaalib Husayn na Hasan, na hao wanawanufaisha watu na wako katika makaburi yao, swali: Kwa nini hawakujinufaisha wenyewe na miujiza hiyo wakiwa hai, Tumemuona ‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) Ukhalifa wake haukutulia kisha akafa kwa kuuwawa, tumemuona Hasan  kadhalika amelazimika kujiuzulu Ukhalifa kwa Mu’aawiyah Mzandiki mkubwa kwa Shia? Na ambae Mashia wengi wanamwona kuwa ni shetani, kwanini alijiuzulu kwa ajili yake Mu’aawiyah? Bali tumemuona Husayn anajipeleka kwenye dhiki kisha kwenye mauti, na hakupata aliokuwa akitamani, na hivi hivi wafuasi wake baada yake, ziko wapi miujiza hiyo ambayo ilikuwa kwao, huu ni utata na kuna mgongano.

 

 

 

Utata Mwengine: vipi Nabiy atazikwa mbele ya Abu Bakr na ‘Umar na kwa mtazamo wa Shia ni makafiri na Muislamu hazikwi mbele ya kafiri hili lilikuwaje?

 

 

Vipi atazikwa Mtukufu zaidi wa viumbe wa Allaah na mbora aliyekanyaga kwa nyayo zake ardhi Muhamad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) azikwe mbele ya makafiri? Hili likoje?  Vipi liwe kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) Na kwa nini Allaah hakumhifadhi katika ujirani wa makafiri katika mauti yake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)?  Kwa nini hakumlinda kipenzi chake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)? Kwanini hakumhifadhi kipenzi chake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuzikwa na makafiri? Kisha alikuwa wapi ‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) simba wa masimba kwenye hayo yote? Kwanini hakuzuia jambo hili kubwa na kuzuia kuzikwa na kupigana kwa ajili yake?  Muhamad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anazikwa baina ya makafiri wapinzani waliopondoa na kubadilisha sheria na wakaondoa Qur-aan na wakaritadi baada ya mauti ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)? Vipi ‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) anyamaze kwenye hili?

Huu ni utata unahitaji dalili na ufafanuzi wa uwazi.

 

 

 

Utata Mwengine: Wanazuoni wa Kishia wanadai kuwa andiko kuhusu Uimamu wa ‘Aliy na ustahiki wa Uimamu wake limethibitika katika Qur-aan. Lakini Swahaba walificha. Kauli hii iko katika riwaya nyingi za Shia, kuwa Uimamu wa ‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) na ukhalifa wake umethibitika katika Qur-aan Tukufu isipokuwa swahaba wameficha na kunyamazia. Madai hayo ni batili, kwa kuwa sisi hatukuwaona Swahaba wakificha Hadithi inayothibitisha na Shia juu ya Uimamu wa ‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) mfano wa Hadithi, “Wewe kwangu ni kama daraja la Haruna kwa Muwsaa”  (Muslimu  4418) Na nyingine miongoni mwa Hadithi zinazofanana na hayo kwa nini Swahaba hawakuficha Hadithi hii, kama walivyoficha jina la ‘Aliy katika Qur-aan Tukufu. Na dalili iko katika kitabu cha Allaah Ta’alaa? Hili linahitaji ufafanuzi kwa vile ni utata (mushkeli).

 

 

 

Utata Mwengine: Kwa kuwa Abu Bakr na ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhum.) wamefanikiwa katika majaribio ya kikhabithi kama wanavyodai Shia katika kumuondoa ‘Aliy katika ukhalifa kwa hiyo ni faida gani ambayo wao wenyewe waliipata kwa ajili ya nafsi zao wenyewe? Ni faida gani aliipata Abu Bakr? Na faida gani aliipata ‘Umar?  Na kwanini Abu Bakr hakumwachia ukhalifa mmoja wa wanawe kama alivyofanya ‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu.) lau nao wangetaka utawala kwanini Abu Bakr hakumtawalisha utawala yoyote wanawe! Kama alivyofanya ‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) na kwanini ‘Umar hakumtawalisha uongozi yoyote miongoni mwa wanawe kama alivyofanya ‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) na wote? Huu ni Mushkeli unahitaji majibu.

 

 

 

Utata Mwengine: Shia wanapokea toka kwa ‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kuwa alipotoka kwa Swahaba zake akiwa na huzuni anapojua alisema: “Nyie vipi mko katika zama ambazo ndani yake mipaka inakiukwa, na mali inafanywa mpokezano na mawalii wa Allaah wanafanyiwa uadui na wanatawalishwa ndani yake adui wa Allaah? Wakasema: ewe, Amiri wa waumini, vipi tukizikuta zama hiyo tufanyeje? ‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu.) alisema: kuweni kama wafuasi wa Issa walichanwa kwa misumeno na kusulubiwa juu ya mbao kisha akasema, Mauti katika utii wa Allaah ni bora kuliko uhai katika kumuasi Allaah”

Hili limo ndani ya kitabu “Nahjus Saadah” Juzuu ya 2 Uk. 639.

 

 

 

Swali Na Mushkeli: Taqiyah ya Shia iko wapi hapa? Kwanini ‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) Imamu Ma’aswuum kwa Shia ana waamuru wafuasi wake wasubiri hata wakichomwa kwa msumeno na kusulubiwa juu ya mbao, kisha anasema: Mauti juu ya utii ni bora kuliko uhai juu ya uasi. Iko wapi Taqiyah hapa wanayoinadi Shia?

 

 

 

Utata Mwengine:   Ni nani ambae alimlazimisha Abu Bakr katika kusuhubiana na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika Hijra yake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)? Lau angekuwa mnafiki kama wasemavyo Shia kuhusu Abu Bakr (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwa nini akimbie watu wake makafiri na wao wana nguvu katika Makkah?

 

 

Na iwapo ni masilahi ya kiduiia kwa kuwa hao (Shia) mara nyingine anasema:Hakutoka isipokuwa Masilahi ya kidunia, tunawaambia: Ni maslahi gani aliokuwa akiyatarajia Abu Bakr pamoja na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)  katika saa ile?

 

 

Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alitoka peke yake akiogopa? Pamoja na kuwa anaweza kujipeleka kwenye kifo kutokana na makafiri ambao hawakumsadiki? Hili linahitaji ushahidi wa kutosha wa kumtuhumu Abu Bakr kuwa hakutoka isipokuwa unafiki. Ni jambo gani la kumtuhumu na kumlazimisha kutoka na asibakie pamoja na familia yake, wanawe, shangazi zake, miongoni mwa makafiri katika Makkah? Mnasema kuwa hakutoka isipokuwa kwa masilahi ya kidunia, Ni masilahi gani hayo ya kidunia aliyokuwa akitaka, kwa ajili yake pamoja na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)? Hakuna masilahi ya dhahiri ya kidunia.

 

 

 

Utata Mwengine:  Swali jingine ikiwa Swahaba (Radhwiya Allaahu ‘anhum) waliritadi baada ya mauti ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) basi kwa nini walipigana na walioridadi katika wafuasi wa Musaulamah al-Kadh-dhaab na wafuasi wa Tulayha bin Khuwaylid na wafuasi wa Al-Aswad ‘Insy na wafuasi wa Sajaah na wengine na wakawarudisha kwenye Uislamu. Kwa nini hawakuwanusuru hao wapingaji ambao walidai Utume katika wakati huo madamu ni mfano wao wameritadi kama wao, ikiwa Swahaba waliritadi baada ya mauti ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa nini waliwapiga vita walioritadi na kuwalazimisha kurudi kwenye Uislamu? Kwa nini hawakumnusuru Al-Aswad ‘Insy ambao hao walidai Utume? Huu ni mushkeli unahiaji majibu ya kielimu.

 

 

 

Utata Mwengine: Tumemuona ‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) hakuwakufurisha mahasimu wake, hata wale Khawaarij ambao walimpiga vita na kumuudhi na kumkufurisha ‘Aliy hakuwakuwafurisha wao. Kwa nini basi Shia hawamuigi ‘Aliy na wao ndio ambao wanawakufurisha wabora wa Swahaba wa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)?  Bali wake zake ni mama wa waumini na ‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) hakumkufurisha yoyote miongoni mwa aliopigana nao si katika khawaarij wala wengine, bali katika baadhi ya athari amesema alipoulizwa kuhusu Khawaarij alisema: ‘Je! Ewe Abal-Husayn hao ni makafiri? Akasema: “Hao wamekimbia ukafiri” wakasema: Sasa ni nani hao, ni wanafiki? Akasema: Hapana, wanafiki hawamtaji Allaah isipokuwa kidogo, wakasema: Unasemaje Ewe Abal Husayn wal Hasan? Nasema kuhusu wao: “Ni ndugu zetu waliotudhulumu (waliotufanyia uadui) hatuwaanzishii vita hadi watuanze.”

Shia wanawakufurisha viumbe bora wa Allaah baada ya Nabiy nao ni Swahaba wa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).

 

 

 

Utata Mwengine: ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhu) alikuwa kwa makubaliano ya watu wa Sunnah na Shia akishauriana na ‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) katika mambo mengi na hili lipo ndani ya ‘Nahjul Balaaghah’ ukurasa wa 325 na 340 uhakiki wa Subhi Swaalih! Lau ‘Umar angekuwa dhalimu kama wanavyodai Shia asingewashauriana na watu wa haki. Kwa kuwa dhalimu hataki haki abadan, ‘Aliy alikuwa mshauri wa dhalimu huyu? Basi kwa nini? Huu ni utata Unahitaji majibu.

 

 

 

Utata Mwengine: Imethibitika kwa makubaliano kuwa Salmaan Farsiy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) alikuwa Amiri wa Madaain katika wakati wa Ukhalifa wa ‘Umar na vile vile Amaar bin Yaasir alikuwa Amiri wa Kufah katika ukhalifa wa ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhu) na Shia wanadai kuwa Salmaan Farisy na Amaar bin Yaasir walikuwa wanusuru wa ‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) na walikuwa ni katika kundi lake, na kama ‘Umar kwao angekuwa Murtad, dhalimu jeuri dhidi ya ‘Aliy kwanini Salmaan alikubali na kwa nini Amaar alikubali, kwa nini walikubali kuwa maamiri katika ukhalifa wa ‘Umar bin Al-Khattwaab (Radhwiya Allaahu ‘anhu)? Kwa nini Anmaar aliafikianakuwa Amiri wa Kufah? Na kwa nini Salmaan alikubali kuwa Amiri wa Madaain? Je inafaa kwao kumsaidia dhalimu na Murtadi na Allaah Anasema: “wala msiwasaidie ambao wamedhulumu” Huu ni mushkeli tunataka jawabu.

 

 

 

Mushkeli Mwengine: Kuna swali liliulizwa kwa mmoja wa Shia sikilizeni vizuri, “Enyi Shia wenye akili, enyi mnaotafuata ukweli. Enyi mnaotarajia kuwa ni wapokezi wa bendera ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi Wasallam) Siku ya Qiyaamah, Shia mmoja aliambiwa! Je Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakutuamrisha kuchagua wake wema? Na kuwa na wakwe watukufu katika watu, hakuwa na jawabu isipokuwa alisema:  Ndio, bila shaka, akaambiwa: Je unaridhia kuwa na mkwe mtoto wa zina? Akasema, Najilinda kwa Allaah kuwa na mkwe mtoto wa zina akaambiwa nyie mnasema: au wanazuoni wa Shia wanasema katika vitabu vyao wanadai uongo kuwa, ‘Umar bin Khatwaab alikuwa mtoto wa zinaa na jina lake lilikuwa ni Swahaak hilo amelitaja Bahrany katika kitabu “Al- Kashkuul” Juzuu ya 3 ukurasa wa 212 na anadai kuwa mwanazuoni huyu wa Kishia ni Imatullah Al-Jazairy anadai: Nasema kwa uhakika wote: “Kuwa ‘Umar alikuwa hatulii isipokuwa kwa maji ya wanaume”. Allaah atukinge, bali Shia wanadai kuwa binti yake Hafswah alikuwa mnafiki khabithi kama baba yake, bali alikuwa Kafiri.

 

 

 

Hapa kuna swali: Unadhania Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anakuwa mkwe wa mtoto wa zina? Allaah atukinge, au anaridhia mwenyewe mke fisadi mnafiki? Wa-Allaahi nyie mnamzulia Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), Enyi Mashia na mnaridhia kwa Nabiy yale msiyoyaridhia kwa Nafsi zenu wenyewe. Tunataka jawabu juu ya mushkeli huu.

 

 

 

Utata Mwengine: Malik bin Ashtur mmoja wa wakuu wa Swahaba wa ‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) nao ni miongoni mwa wanaotukuzwa na Shia, anasema: Enyi watu – Hakika Allaah Mtukufu anakutumieni Rasuli wake Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa mbashiri muonyaji. Na amekuteremshieni kitabu ndani yake kuna halali na haramu, faradhi na Sunnah, kisha akamfisha akiwa ameekeleza wajibu wake kisha amemfanya Khalifa wa watu Abu Bakr naye ataenda mwendo wake na kufuata Sunnah zake. Na Abu Bakr akamwachia ‘Umar naye akiendelea kufuata Sunnah hiyo. Hili limo ndani ya kitabu “Malik bin Ashtar Khutwabuhu wa Aaraauhu ukurasa wa 89”.

 

 

Swali hapa ni: Malik bin Ashtur anamsifu Abu Bakr na ‘Umar kwa wanayostahili, pamoja na haya Shia wanajitia upofu juu ya sifa hizi wala hawataji katika vikao vyao na katika Husayniyaat zao, ambazo haziishi kuwatusi Abu Bakr na ‘Umar kwanini wanaficha?

 

 

 

Utata Mwengine:  Kwanini Shia wanampa (‘Iswmah) uhifadhi kwa Faatwimah na kuizuia kwa dada zake Ruqayyah na Umu Kulthuum? Na wao ni watoto wa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kama Faatwimah?  Huu ni mushkeli unahitaji jibu.

 

 

 

Mushkeli Mwengine: Shia anapoambiwa: Kwa nini ‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) alinyamaza kuhusu kugombania Ukhalifa baada ya kifo cha Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) nae ni kama mnavyodai ametajwa katika maandiko? Wanazuoni wa Kishai wanajibu haraka: Kwa vile Nabiy alimuusia kuwa asilete fitina baada yake na wala asichomoe upanga na wala asimwage damu kwa kuhifadhi damu za Waislamu. Shia wataambiwa: Basi kwanini ‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) alichomoa upanga kwa watu wa Jamal na Swiffiyn? Na katika vita vile walikufa maelfu ya Waislamu Je ni lipi bora la kupigania ni vita vya Jamalina Swiffiyn au kuthibitisha Uimamu hata wakifa watakaokufa ndani ya vita hivyo? Hili linahitaji jawabu la wazi.

 

 

 

Utata Mwengine: Shia wanadai kuwa Maimamu ni Ma’aswuum, imekuja kwa makubaliano yanatengua hii ‘Iswmah’  chukua kwa njia ya mfano kama Hasan bin ‘Aliy anamkhalifu baba yake ‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu)  katika kutoka kwake kupigana na wanaodai damu ya ‘Uthmaan (Radhwiya Allaahu ‘anhu)  bila shaka  mmoja wao yuko sawa na Mwengine amekosea na wote hao ni Maimamu wawili, Ma’aswuum kwa Shia, hili ni jambo geni, vile vile Husayn amemkhalifu Hasan katika kadhia ya Sulhu pamoja Mu’aawiyah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) na bila shaka mmoja wao yuko sawa na Mwengine amekosea na ajabu wote hao ni Maimamu wawili ambao hawakosei.

 

 

Utata Mwengine:

Iliposhuka kauli Yake, Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُكُمْ أَن تُؤَدُّوا الْأَمَانَاتِ إِلَىٰ أَهْلِهَا ﴿٥٨﴾

Hakika Allaah Anakuamrisheni kurudisha amana kwa wenyewe. [An-Nisaa:58]

 

 

Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliwaita Bani Shaybah na akawapa funguo za Kaabah, na kumwambia, “Chukueni enyi Bani Twalhah milele na milele katika nyinyi hadi Siku ya Qiyaamah hatukunyang’anyeni isipokuwa dhalimu”.

 

 

Hili analisema katika Shani inafungana na ulinzi wa Kaabah, basi kwanini hakusema katika Shani ya Ukhalifa wa ‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) na hilo ni jambo kubwa zaidi kwa Waislamu na juu yake kuna Masilahi ya Waislamu wengi, bali Imani inasImamua juu yake, kwa nini hakumwambia ‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ‘Chukua Ewe ‘Aliy, chukua Uimamu kwako wewe na kizazi chako milele na milele hatakupokonyeni isipokuwa dhalimu’.

 

 

Kwa nini hakulisema (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na badala yake amesema katika usImamuizi wa Kaabah?

 

 

 

Utata Mwengine: Mashia wanadai kuwa ‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) anayo nakala ya Qur-aan iliyopangiliwa kwa jinsi ilivyoshuka. Kwa nini ‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) alipokuwa Khalifa baada ya ‘‘Uthmaan hakutoa msahafu huu Kamili?

 

 

 

Utata Mwengine: ‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) alishiriki katika vita dhidi ya walioritadi zama za Ukhalifa wa Abu Bakr (Radhwiya Allaahu ‘anhu) akachukua kijakazi katika mateka wa Bani Hanifah na baadae kijakazi hicho kilizaa mtoto aliyeitwa Muhammad Bin Al Hanafiyah hii inalazimika kusema kuwa ‘Aliy ameridhia ukhalifa wa Abu Bakari vinginevyo asingeshiriki kwa radhi yake katika jambo hili. Lau kama isingekuwa Ukhalifa wa Abu Bakr ni wa kisheria basi asingeshiriki katika jambo hili na kumchukua kijakazi (As-Sabiyah) aliyekuja na Muhammad bin Hanafiyah.

 

 

 

Utata Mwengine: Shia wanadai katika simulizi zao. Kuhusu Mahdi aliyejificha na huyo ni Imamu wa kumi na mbili, Muhammad bin Hasan Al-Askari wanataja: kuwa yeye alipozaliwa ndege walimshukia toka mbinguni wakipangusa mbawa zao kwenye kichwa chake na uso wake na mwili wake. Kisha wanaruka, baba yake alipoambiwa hivyo alicheka, akasema: Hao ni Malaika wa mbinguni wanashuka kupata baraka kwa mtoto huyu na hao ndio wanusuru wake atakapotoka. Hili lipo ndani ya kitabu cha “Raudhatul-Waadhiin” ukurasa wa 260.

 

 

 

Swali na utata: Madamu malaika ndio wanusuru wake basi kwanini ana hofu na kuingia katika Sirdaab? Huu ni utata na mushkeli.

 

 

 

Utata Mwengine: Shia ambao wanadai kuwa Allaah amerefusha Umri wa Mahdi wao anangojewa mamia ya miaka, kwa ajili ya haja ya viumbe – bali ulimwengu wote – lau Allaah angerefusha uhai wa yoyote kwa ajili ya mahitaji ya viumbe kwa huyo, basi angerefusha miaka ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) basi kwa nini hakurefusha muda wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) isipokuwa ni kwamba amekamilisha sheria kwake yeye (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).

 

 

 

Mushkeli Mwengine: ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhu) alichagua watu sita katika wafuasi wake kwa ajili ya Shura baada ya kufa kwake, kisha watatu katika wao wakajitoa. Kisha Abdur-Rahmaan akajitoa wakabaki wawili. ‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu)  na ‘Uthmaan (Radhwiya Allaahu ‘anhu)  kwanini  ‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu)  tangu mwanzo hakutaja mbele yao kuwa yeye  ni wasii wa Khalifah toka kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) Je, alikuwa anamhofia yoyote baada ya mauti ya ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhu)? 

 

 

Haya ndio tuliojaaliwa enyi ndugu zangu katika kutaja baadhi ya utata na matatizo na maswali kuhusu madhehebu haya yenye kugongana. Ninawaomba mashie wenye akili wafanye utafiti kuhusu mas-ala haya tata huenda yakawarudisha katika haki waliyokuwa nayo Swahaba wa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) pamoja na watu watukufu wa nyumba yake.

 

 

Namuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Atuthibitishie katika Kitabu chake na katika Sunna ya kipenzi chake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).

 

 

Ee Allaah! Jaalia mwisho wa maneno yetu tusemayo pindi tutakapotoka hapa duniani ni neno hili tukufu lililobarikiwa, “Laa Ilaaha Illa Allaah Muhammadun RasuuluLlaah”

 

 

Kadhalika tunamuomba Ar-Rahmaan kwa ukarimu Wake Atujaalie makaburi yetu kuwa ni bustani katika bustani za peponi, na Atufufue siku ya Qiyaamah nyuma ya bendera ya kipenzi Chako Muhammad bin ‘Abdillaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) miongoni mwa Swahaba zake, watu wa nyumba yake waliotoharika kwa hakika yeye ni Mkarimu na tunamshukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa).

 

 

 

[1] Ma’aswuum ni mtu aliyehifadhiwa na baadhi ya mambo; watu wa namna hii katika dini ni kama Mitume na Manabii.

 

[2] Laqab ni jina la kupachikwa

 

[3] Husainiyaat ni sehemu za kuomboleza misiba ya kishia na ni sehemu za kufanyia ibada zao vile vile

 

 

Share