Imaam Wakubwa Wanavyosema Kuhusu Mashia

Imaam (Wanachuoni) Wakubwa Wanavyosema Kuhusu Mashia

 

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

Imaam Ash-Shaaf'iy

 

Imam Ash-Shafi’iy alisema siku moja kuhusu Mashia, ‘Sijawahi kuona miongoni mwa makafiri watu wanaojulikana kwa kusema uongo kuliko Mashia.’ [Minhaaj as-Sunnah an-Nabawiyyah, 1/39] Wakati mwingine alisema, ‘Simulia elimu kutoka kwa yeyote yule utakayekutana naye isipokuwa Mashia, kwani wao hutunga Hadyith na kuzifanya sehemu ya Dini yao.’ [Minhaaj as-Sunnah an-Nabawiyyah, 1/38].

 

 

 

Imaam Abuu Haniyfah

 

Imesimuliwa kuwa Imaam Abu Haniyfah alikuwa akikariri kauli ifuatayo kuhusu Mashia, ‘Yeyote mwenye mashaka kuhusu ukafiri wao basi nae pia ni kafiri.’

 

 

 

 

Imaam Maalik

 

Siku moja Imaam Maalik aliulizwa kuhusu wao (Mashia) akajibu, ‘Usiongee nao wala kupokea hadithi zao, kwani hapana shaka wao ni waongo.’ [Minhaaj as-Sunnah, 1/37] Ilitajwa katika darsa yake kuwa Mashia wanawatukana Swahaba. Katika kujibu akataja Aayah: 

 

مُّحَمَّدٌ رَّسُولُ اللَّـهِ ۚ وَالَّذِينَ مَعَهُ أَشِدَّاءُ عَلَى الْكُفَّارِ رُحَمَاءُ بَيْنَهُمْ ۖ

Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) ni Rasuli wa Allaah. Na wale walio pamoja naye ni wakali zaidi dhidi ya makafiri; wanahurumiana baina yao…[Al-Fat-h 29]

(mpaka alipofika)

..لِيَغِيظَ بِهِمُ الْكُفَّارَ…..﴿٢٩﴾

ili liwatie ghaidhi makafiri.’’ 

 

Kisha akasema, ‘Basi yeyote anayebughudhiwa wakati Maswahaba wanapotajwa basi na yeye kakusudiwa pia na aayah hii.’ (Yaani yeyote anayechukizwa kwa kutajwa Swahaba basi amekusudiwa katika Aayah hii kwa sababu Allaah Anasema,

..لِيَغِيظَ بِهِمُ الْكُفَّارَ…..﴿٢٩﴾

ili liwatie ghaidhi makafiri.’’ 

 

 

 

 

Imaam Ibn Al-Mubaarak

 

Imaam Ibnul Mubaarak amesimuliwa akisema, ‘Dini hupatikana kwa Watu wa Hadiyth (Ahlul Hadiyth), falsafa na udhuru wa kijanjajanja unapatikana kwa watu wa rai (Ahlur Rai) na uongo unapatikana kwa Mashia.’ [Al-Muntaqaa min Minhaaj al-I`tidaal, uk. 48]

 

 

 

Imaam Abu Zur’ah Ar-raaziy

 

Mwanachuoni huyu mkubwa amenukuliwa akisema, ‘Ukimuona mtu yeyote anayewadharau Swahaba, basi jua ya kuwa yeye ni kafiri. Hiyo ni kwa sababu Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). alikuwa mkweli na alituletea ukweli ambao umetufikia kwa njia ya Swahaba. Hao makafiri (Mashia) lengo lao ni kutia shaka katika wasimulizi wa ukweli huo (Swahaba) ili kutia shaka pia katika Qur-aan na Sunnah. Basi makafiri ndio wanaostahiki zaidi kudharauliwa.’

 

 

 

Imaam Al-Qaadhiy Abu Ya’alaa

 

Imesimuliwa kuwa Imaam Abu Ya’alaa alisema, ‘Msimamo wa Wanachuoni wa Fiqhi kuhusu mtu anayewalaani Swahaba, ilhali akiamini kuwa kufanya hivyo inajuzu, ni kwamba amekufuru. Kama anawalaani ilhali akiamini kuwa kufanya hivyo haijuzu, basi atakuwa ametenda kosa la ufasiki, na sio kosa la ukafiri.’ [As-Swaarim al-Masluul, uk. 569].

 

 

 

Imaam Atw-Twahaawiy

 

Katika kitabu chake kuhusu itikadi za Uislamu, al-Aqiydah atw-Twahaawiyyah, anasema, ‘Tunawapenda Maswahaba wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) bila kupituka mipaka katika mapenzi yao au kujiweka mbali na yeyote katika wao. Tunawachukia wale wanaowachukia na hatusemi ila kheri kuhusu wao (Swahaba). Kuwapenda ni kitendo cha kidini, na dalili ya Imani na uchaji Allaah na (kwa upande mwingine) kuwachukia ni kitendo cha ukafiri, unafiki na ufasiki.’ [Sharhul-Aqiydah atw-Twahaawiyyah, uk. 528]

 

 

 

Imaam Ibn Hazm Al-Andalusiy

 

Siku moja, wakati wa utawala wa Waislamu katika nchi ya Hispania Imaam Abu Muhammad Ibn Hazm alikuwa akijadiliana na Mapadri Wahispania wa Kikatholiki kuhusu baadhi ya maandiko ya dini yao. Aliwaletea dalili na hoja kuhusu kubadilishwa sehemu nyingi katika Biblia na kupotea kwa maandiko ya asili. Walipomjibu kwamba Mashia pia wanadai kuwa Qur-aan ilibadilishwa na hii tuliyonayo sio ile ya asili, akajibu, ‘Mashia hawawezi kutumiwa kama hoja dhidi ya Qur-aan na Waislamu kwani wao wenyewe si Waislamu.’ [Ibn Hazm, al-Fiswaal fiy al-Milal wa an-Nihal, 2/78 na 4/182] Madai hayo yao (Mashia) yamejibiwa na wanachuoni wengine wengi wa zamani kama Ibn Taymiyah katika Minhaaj us Sunnah, adh-Dhahabiy katika Muntaqaa min Minhaaj al-Itidaal, Ibn Kathiyr katika kitabu chake mashuhuri cha historia Al-Bidaayah wan-Nihaayah, Ibn al Jawziy katika Talbiys Ibliys, na al-Qaadhiy Ibn al-‘Arabiy katika al-Awwaasim min al-Qawaasim]

 

 

 

Imaam Al-Auusiy

 

Mwanachuoni huyu aliwatangaza Mashia kuwa ni makafiri kwa sababu ya kutukana kwao Maswahaba. Msimamo wake ulikuwa umechukuliwa kutoka kwenye kauli za Imaam Maalik na wanachuoni wengine waliokuwa wakiwafikiana nae katika suala hilo.Kuhusu madai yao kuwa wao ni katika Ahlul Bayt (familia ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema, ‘Hapana, ukweli ni kwamba wao (Mashia) ni wafuasi wa Shaytwaan, na Ahlul Bayt hawana uhusiano wowote na wao (Mashia).’

 

 

 

Share