Urithi Kwa Watoto Wa Kaka Aliyefariki

SWALI:

 

 

A SALAAM ALEYEEKUUM WARAHAMATULAHI WABARAKATU, MIMI NINA KAKA YANGU, YEYE ALI FARIKI MWANZ0 NA BAADAYE AKAFARIKI BABA YETU, JE WATOTO WA HUYU KAKA YETU WANASTAHILI KUPEWA URITHI NA KAMA NDIVYO. MGAO WAO UTAKUWAJE, NAOMBA UFAFANUZI KUPITIA MAKALA ZENU.

ASANTE

 


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Shukrani kwa swali lako kuhusu urithi wa wajukuu ambao babu yao ameaga dunia.

 

Hakika ni kuwa watoto wa kaka yako watakuwa ni wenye kumrithi baba yao bila ya shaka yoyote ile. Watoto hao wanaweza kumrithi baba yako ikiwa baba yako hana mtoto wake kabisa.

 

Ama kwa hali hiyo uliyotaja watoto wa baba yako wako ukiwa wewe ni mmoja wao, basi hao wajukuu hawatakuwa na sehemu ya kurithi.

 

Ili kuweza kukuelezea mgao wa kila mrithi huna budi kutuandikia jamaa walio hai. Kwa mfano, je, ameacha mke? Je, mzazi au wazazi wapo hai? Je, ana watoto wangapi, wanaume na wanawake?

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share