Dalili Gani Baada Ya Swalaah ya Istikhaarah? Je Kuna Muda Maalumu Wa Kuiswali

 

Dalili Gani Baada Ya Swalaah ya Istikhaarah Je Kuna Muda Maalumu Wa Kuiswali

 

 www.ahidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Assalamu alaykum. Unaposali Istikhara na ukaona kuwa sala yako haijajibiwa au hujaona dalili zozote kuna muda maalumu wa kusali Istighar au nisali mpaka nitakapo ona dalili zozote?

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.   

 

Hakuna muda maalumu wa kuswali Swalaah ya Istikhaarah.

 

 

Hakuna dalili yoyote isipokuwa tu baada ya kuswali Istikhaarah Allaah (‘Azza wa Jalla)  Atakufungulia kifua chako utapata hisia ya ima kulitenda jambo au kuliacha na ndio itakuwa ni mwongozo wake Allaah (‘Azza wa Jalla)  kutenda hilo jambo uloliswalia Istikhaarah na jambo hilo litakuwa bila shaka ni lenye na kheri nawe madamu umemkabili Allaah Akuongoze.

 

Swalaah ya Istikhaarah inaweza kukaririwa ikiwa bado mtu hakutumainika kulitenda jambo au kuliacha. [Fataawaa Imaam ibn Baaz]

 

Vile vile tafuta ushauri kwa watu wako wa karibu walio na taqwa na waaminifu.

  

Bonyeza viungo vifutavyo upate faida zaidi kuhusu Swalaah ya  Istikhaarah:

 

Muda Wa Swalaah ya Istikhaarah

 

 

Kwa Nini Tuswali Istikhaarah Na Iswaliwe Kwa Ajili Ya Nini - Ipi Du'aa Yake

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share