Adhabu Inayompata Baba kwa Kutowaangalia Watoto Wake

 

SWALI:

 

Adhabu gani inaompata baba anaye mtupa mwanawe au wanawe wa halali?


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu kwa swali lako kuhusu baba kutowaangalia watoto wake.

Hakika hakuna adhabu maalumu ambayo shari’ah imetoa kuhusiana na suala hilo. Katika shari’ah tofauti, baba anaadhibiwa kwa kutowaangalia watoto wake ambao ana jukumu juu yao kuhusu hilo. Na katika shari’ah ya Kiislamu pia, lau baba atashitakiwa kwa Qaadhi basi Qaadhi mwanzo atamlazimisha awatunze na kuwahudumikia. Kushindwa kufanya hivyo itabidi achukuliwe hatua na Qaadhi kutoa adhabu ya ta’ziyr kulingana na dhulma yenyewe.

 

Ama Kesho Akhera, adhabu yake itakuwa kubwa kwani hilo huingia katika dhulma.

Na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

Ogopeni dhulma kwani dhulma ni kiza Siku ya Qiyaamah” (Muslim).

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share