Kuku Wakitiwa Maji Ya Moto Kabla Ya Kutolewa Manyoa Hawafai Kuliwa? Na Kuna Hadiyth Inayosema Hivyo?

SWALI:

 

Assalamu Alaykum WRWB,

Naomba nipewe jibu kwa suala langu hili: Baadhi ya waislamu wanaamini kuwa kuku waliowekwa kwenye maji ya moto kabla ya kutolewa manyoya hawafai kuliwa kwa vile washakuwa haramu. Hujja yao ni kuwa kuna Hadiyth ya Mtume SAW ambayo mafhoom yake ni kama hivi: "Kuku yoyote anapotiwa kwa maji ya moto kabla ya kuchunwa basi ule uchafu wote ulioko kwenye manyoya yake huganda kwenye nyama zake na huisababisha ikawa haram kula." Nimeitafta ithbati ya hii hadithi bila ufanisi ndio nakuombeni mnifafanulie. Jazakallahu Bilkheir.Ma'assalaam.

 


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani kwa swali lako kuhusu uharamu wa kula kuku aliyetiwa maji moto akiwa na manyoa yake.

 

Hatukuweza kuipata Hadiyth hii katika vitabu vya Hadiyth.

 

Kwa hiyo, kuku baada ya kumchinja unaweza kumtia maji ya moto ili iwe sahali kumtoa manyoa na baadaye kumpika na kumla bila ya tatizo lolote lile, na ni halali wala si haramu kuliwa.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share