Kuzuia Mtu Kuoa Mke Mwenye Sifa Za Kiislamu

SWALI

 

ASALAM ALEHKUM

 

NAOMBA KUULIZA .NINI HUKU YA WATU AMBAO WANAZUIA KIJANA WAO KUOA MWANAMKE ANAE MPENDA ILE HALI MWANAMKE MWENYEWE ANASIFA ZOTE ZA KISLAM. NAOMBA JIBU

 

MUNGU AWABARIKI SANA


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani kwa swali lako kuhusu wazazi kumzuilia kijana wao kuoa msichana mwenye sifa za Dini.

Kufanya hivyo ni makosa sana kwa wazazi na watakuwa wanafanya dhulma iliyokatazwa na Allaah Aliyetukuka na Mtume Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Na bila shaka dhulma ni jambo la makosa na la dhambi ambalo halifai kufanywa na wanaadamu na haswa wazazi kwa kijana wao. Haifai kwa wazazi kufanya hivyo, bali wangepata thawabu zaidi kama wangempa moyo na kumsaidia.

 

Na haya matatizo yanayotukumba duniani yanawezekana yametokana na hilo kwani Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametutahadharisha kuwa kama hilo la kuwaozesha wanandoa kwa ajili ya Dini yao halitofanyika basi kutakuwa na fitna katika ardhi na uharibifu mkubwa.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share