Mwanamme Anaweza Kuvaa Pete Ya Ndoa?

SWALI:

 

Asalaam aleykum,

Kwa jina naitwa ****** nna swali nataka kuuliza. Ni kuhusu kuvaa pete ya ndoa ya silver si dhahabu kwa mwanamume je hukumu yake ni nini?

 

Ahsante sana

 


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu uhalali wa kuvaa pete ya fedha ya ndoa kwa mwanamme.

 

Hakika ni kuwa kuvaa pete ya fedha inafaa kwa mwanamme Muislamu. Ni jambo ambalo hajilakatazwa kuvaa pete. Hata hivyo, kuvaa pete ya fedha ya ndoa kwa mwanamme Muislamu haifai kwani kufanya hivyo ni kuwaiga makafiri jambo ambalo tumekatazwa na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).

 

Kwa hiyo, kuvaa tu pete ya fedha haina neno lakini kuivaa ya ndoa haifai kishari’ah.

 

Uislamu hauna taratibu za pete ya ndoa au keki ya harusi au mwanamke kutolewa na veli na kulishana na mwanamme keki kwenye harusi hadharani na baya zaidi kupigana mabusu mbele za watu na kucheza muziki. Hayo yote ni matendo ya kikafiri yaliyoingizwa na wajinga kwenye jamii za Kiislamu.

 

Aliulizwa mfano wa swali hilo Shaykh 'Abdul-Muhsin Al-'Abbaad (Allaah Amhifadhi), kuhusu wanandoa kuvishana pete ya ndoa inayojulikana kama 'Ad-Dublah' na mtu kuvaa mkono wa kulia wakati wa posa na baada ya posa anavaa hiyo pete mkono wa kushoto.

Akajibu kwa kusema,  hiyo ni katika bid´ah iliyozushwa ambayo Waislamu wameiga Makafiri. (Kuivaa hiyo pete) ikiwa ni mkono wa kulia au wa kushoto, yote mawili hayajuzu. Na ni sawa likiwa hilo litafanywa kabla ya ndoa au baada ya ndoa.

[http://www.alharamain.gov.sa/index.cfm?do=cms.scholarsubject&schid=9636&subjid=3...]

 

Bonyeza viungo vifuatavyo upate manufaa zaidi kwenye kitabu cha ndoa cha Imaam Al-Albaaniy (Allaah Amrehemu) na pia kwenye viungo vingine hapa chini:

 

40 Kukataa Kufanya Mambo Yanayopingana Na Shariy'ah (Kitabu Cha Adabu Za Ndoa Cha Imaam Al-Albaaniy)

 

Mwanamume Kuvaa Pete

 

Mwanaume Kuvaa Fedha

 

Yanayopasa Na Yasiyopasa Kutendeka Katika Ndoa

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share