Kuswali Kuelekea Popote Ikiwa Hajui Wapi Qiblah

SWALI:

 

ASALAAM ALAYKUM WARAHMATU LLAHI WABARAKAT. Naamshekhe swali langu ni mm nimfanya biashara nasafiri nchi tofauti. Hivi juzi nilikuwa safari nilivyofikakule bag langu lilipelekwa nchi nyengine ndani yake kulikuwa na mswala wenye dira unaonionesha nielekee wapi nikiswali, nikawa sijui kibla kipo wapi nikawa naswali tu kwa kuelekea mbele. jee swala zangu zimeswihi au vipi                   

 


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani kwa swali lako kuhusu kuelekea Qiblah pasi na ujuzi.

Hakika ni kwamba Muislamu anapofika katika mji au nchi ambayo ni ngeni anatakiwa ajue mazingira ya mji ule na ulivyo kutoka Makkah kwani lolote laweza kumfikia mmoja wetu kama vile wewe kuukosa mzigo wenye dira. Ukisha juwa hilo jaribu kwa kiasi unachoweza kwa utumiaji wa akili yako kukijua Qiblah kwa kipimo ulipo na mji wa Makkah.

 

Baada ya kufanya hivyo na ukajua kuwa Qiblah ni mbele ulipoelekea au ni upande mwengine wowote ule. Unaanza kuswali kuelekea huko Swaalah yako inakuwa sahihi hata ukigundua baadaye kuwa ulielekea makosa.

Na huu ni usahali wa Dini yetu na kuwa hakuna udhuru wa Muislamu kuacha Swaalah.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share