Asiyekuwa Muislamu Kukualika Futari Inafaa Kuitikia Mwaliko?

SWALI:

 

Assalaaam aleykum,

Poleni na majukumu swali langu ni kwamba je mtu asiye kuwa muislam akikupa mualiko wa kufturu ni sahihi ama si sahihi?


 

JIBU: 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho. 

Shukrani kwa swali lako kuhusu asiyekuwa Muislamu kukualika futari.

Katika kutengeneza na kuamiliana na watu kwa uzuri hakuna ubaya kwa Muislamu kualikwa na kula kwa asiyekuwa Muislamu ikiwa chakula kitakachopikwa ni cha halaal na vyombo vitakavyotumika uhakikishe ni visafi havina najisi au mabaki ya chakula cha haraam ikiwa wanakula vyakula haraam kama nguruwe n.k., au vinnywaji vya haraam kama pombe n.k.

Lakini kama una wasiwasi na waliokualika kuhusu vyakula vyao na vyombo vyao, ni bora kujiepusha na mialiko hiyo.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share