Mchuzi Wa Samaki Nguru Na Bilingani Za Kukaanga

Mchuzi Wa Samaki Nguru Na Bilingani Za Kukaanga

 

 

 

Vipimo Vya Samaki

 

Samaki Nguru                                                         4-5  vipande

Pilipilimbichi ilosagwa                                          1 kijiko cha supu                      

Kitunguu saumu(thomu/galic) kilosagwa         1 kijiko cha supu

Tangawizi mbichi ilosagwa                                   1 kijiko cha supu

Bizari ya samaki                                                      1 kijiko cha chai

Paprika (pilipili nyekundu ya unga ilokoza)      1 kijiko cha chai

Chumvi                                                                     kiasi

Ndimu                                                                       ¼ kikombe

 

 

Vipimo vya mchuzi

 

Bilingani                                                                   2  ya kiasi

Vitunguu (katakata chopped)                               2 vikubwa

Nyanya/tungule    (katakata chopped)               3

Nyanya kopo (paste)                                              2 vijiko vya supu

Chumvi                                                                    kiasi

Ndimu kavu/lumi                                                  1

Mafuta  (ya kukaangia)                                          kiasi

 

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Samaki

 

 1. Changanya viungo vyote vya samaki upake katika vipande vya samaki, vikolee.
 2. Weka kwenye treya ya oveni, na choma (grill) huku unageuza samaki hadi wageuka rangi na karibia kuiva.
 3. Epua samaki weka kando.
 4. Masalo yatakayobakia katika treya weka katika kibakuli kidogo.

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Mchuzi

 

 1. Weka mafuta katika karai yapate moto vizuri.
 2. Katakata bilingani vipande vya mraba (cubes) kisha kaanga katika mafuta  hadi vigeuke rangi.  Epua katika chujio  bilingai  zichuje mafuta.
 3. Weka mafuta kiasi ya vijiko 3 vya supu katika sufuria, tia vitunguu kaanga hadi vigeuke rangi ya hudhurungi (golden brown).
 4. Tia nyanya/tungule, nyanya kopo (tomato paste) endelea kukaanga.
 5. Tia maji kidogo, kisha tia samaki na masala yaliyobakia, tia chumvi.
 6. Pasua lumu (ndimu kavu) vipande kiasi 3-4 tia na uache mchuzi uchemke kidogo bila ya kuvurugika samaki
 7. Epua tayari.

 

Share