Jimai: Mwenye Kujitoa Manii Mchana Wa Ramadhaan

SWALI:

 

Assalam alaykum wa rahmatullahi wa barakaatuh.

Shekh mm nataka niulize swali kwamba je mtu ambaye alijitoa manii siku ya Ramadhani anatakiwa afanye nini ili asamehewe.


 

JIBU: 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho. 

Shukrani kwa swali lako kuhusu mwenye kujitoa manii mchana wa Ramadhaan.

Muislamu anayefunga Ramadhaan anatakiwa ajiweke mbali katika kujikurubisha katika hali ya kutokwa au kujitoa manii. Kwa kuwa manii yanapotolewa yanavunja funga ya mtu. Na suala la kujichua ni suala haraam ambalo limekemewa na shari’ah. 

Kufanya hivyo ni kosa kubwa mbele ya Allaah Aliyetukuka japokuwa hakuna kafara yoyote ile. Inabidi mwanzo arudi kwa Allaah Aliyetukuka aombe msamaha kwa dhambi hilo alilofanya. Kisha aweke Niyah ya kutolirudia tena. Na anafaa ajizuilie asiwe ni mwenye kula chochote siku hiyo pamoja na kuwa hana funga. Baada ya Ramadhaan itabidi ailipe hiyo siku moja. Kadhalika kwa kufuta makosa yake inambidi azidishe mema kama kufunga funga za Sunnah na mengineyo kwani mema hufuta maovu.

Tafadhali bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi: 

Kutokwa na Manii kwa Matamanio Ramadhaan Bila Ya Kitendo Cha Ndoa

Ametazama Sinema Mbaya, Je Alipe Swawm Yake?

Ameota Yuko Na Mwanamke Wake Akatokwa Na Madhii Katika Ramadhaan, Nini Hukmu Ya Swawm Yake

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share