049-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Kusimama Kwa Ajili Ya Rak’ah Ya Tatu, Kisha Ya Nne

Kusimama Kwa Ajili Ya Rak’ah Ya Tatu, Kisha Ya Nne

 

Kisha, alikuwa  (صلى الله عليه وآله وسلم)akinyanyuka kwa ajili ya Rak’ah ya tatu pamoja na takbiyr([1]) na alimuamrisha "aliyeswali vibaya" kufanya hivyo: “….kisha akifanya hivyo katika kila Rak’ah na Sajdah kama ilivyotangulia”

Na alikuwa   (صلى الله عليه وآله وسلم)anaposimama kutoka kikao alisema takbiyr, kisha akasimama"([2]) na "Alikuwa akinyanyua  (صلى الله عليه وآله وسلم)mikono yake([3]) pamoja na takbiyr mara nyingine.

 

Na alikuwa anapotaka kusimama kwa ajili ya Rak’ah ya nne, akisema: ((Allaahu Akbar))"([4]) na alimuamrisha "aliyeswali vibaya" hivyo kama kabla na alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akinyanyua   mikono yake([5]) pamoja na takbiyr mara nyingine.

 

Alikuwa akiketi barabara juu ya mguu wake wa kushoto, kwa utulivu hadi kila mfupa ulirudi sehemu yake kisha akisimama, akijisaidia kwa mikono yake, alikunja ngumi([6]) na kutegemea mikono yake katika kuinuka.([7])

Alikuwa akisoma Suratul-Faatihah kaitka Rak’ah zote mbili na alimuamrisha "aliyeswali vibaya" kufanya hivyo. Katika Swalah ya adhuhuri aliongeza mara nyingine Aayah chache kama ilivyoelezewa katika 'Kisomo cha Swalah ya Adhuhuri'.

 



[1]Al-Bukhaariy na Muslim.

[2]Abu Ya'alaa katika Musnad yake (284/2) ikiwa na isnaad nzuri. Imetolewa katika Silsilatul Al- Ahaadiyth As-Swahiyhah (604).

[3] Al-Bukhaariy na Muslim.

[4]Kifungu kile kile kilichotajwa hapo mbeleni.

[5]Abu 'Awaanah na An-Nasaaiy ikiwa na isnaad Swahiyh.

[6]Ina maana 'kama mtu anayekanda unga'.

[7] Al-Harbiy katika Hadiyth Al-Ghariyb. Maana yake inapatikana katika Al-Bukhaariy na Abu Daawuud. Ama kuhusu Hadiyth kuwa 'alimkataza mtu kujisaidia kwa mikono yake anapoinuka katika Swalah', ni Munkar na sio Swahiyh kama nilivyoelezea katika Silsilatul-Ahaadityh Adhwa'iyfah (967).

Share