051-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Qunuut Katika Swalah Ya Witr

 

Qunuut Katika Swalah Ya Witr

 

"Alikuwa   (صلى الله عليه وآله وسلم)akifanya Qunuut katika Rak’ah za Witr kwenye Swalah ya Witr"([1]) mara nyingine([2]) na "alifanya kabla ya rukuu"([3])

Alimfundisha Al-Hasan Ibn 'Aliy (رضي الله عنه) kusema [baada ya kumaliza kisomo chake katika Witr]:

 

اللّهُـمَّ اهْـدِنـي فِـيمَنْ هَـدَيْـتَ، وَعـافِنـي فِـيمَنْ عافَـيْتَ، وَتَوَلَّـني فِـيمَنْ تَوَلَّـيْتَ، وَبارِكْ لـي فِـيمَا أَعْطَـيْتَ، وَقِـني شَرَّ ما قَضَـيْتَ، (فَ) إِنَّـكَ تَقْـضي وَلا يُقْـضى عَلَـيْك، (وَ) إِنَّـهُ لا يَـذِلُّ مَنْ والَـيْتَ،  (وَلا يَعِـزُّ مَن عـادَيْتَ)، تَبـارَكْـتَ رَبَّـنا وَتَعـالَـيْتَ. (لاَ مَنْجَا مِنْكَ إِلاَّ إِلَيْكَ)

 

Allaahumma-Hdiniy fiyman Hadayta, wa 'Aafiniy fiyman 'Aafayta, wa Tawallaniy fiyman Tawwallayat, wa Baarik liy fiymaa A'twayta, wa Qiniy sharra maa Qadhwayta, [fa]Innaka Taqdhwi wa laa yuqdhwaa 'Alayka, [wa] innahu la yadhwillu man Walayta, (wa laa yai'izzu man 'Aadayta) Tabarakta Rabbanaa wa Ta'aalayta [La manjaa Minka illa Ilayka]

 

“Ee Allaah, Niongoze pamoja na Uliowaongoza, na Unipe afya njema pamoja na Uliowapa afya njema, na Nifanye kuwa ni mpenzi Wako pamoja na Uliowafanya  wapenzi na Nibariki katika Ulichonipa na Nikinge na shari ya Ulilolihukumu kwani] Wewe Unahukumu wala Huhukumiwi.  [Na] Hakika hadhaliliki Uliyemfanya mpenzi [wala hatukuki Uliyemfanya adui] Umetakasika Ee Mola wetu na Umetukuka [Hakuna mahali pa kuokoka isipokuwa Kwako]([4])

 

 



[1]  Ibn Naswr na Ad-Daaraqutwniy ikiwa na isnaad Swahiyh.

[2]  Tumesema, "…. Mara nyingine", kwa sababu Maswahaba waliosimulia

Swalah ya Witr, hawakutaja qunuut humo, kwani ingelikuwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) alifanya daima humo wangelitaja wote. Lakini 'Ubayy Ibn Ka'ab pekee amesimulia qunuut katika Witr, hivyo inaonyesha kwamba alikuwa akifanya mara nyingine. Kwa hiyo, ni dalili kwamba qunuut katika Witr sio wajibu,  na hii ni rai ya Maulamaa wengi. Kwa sababu hii, Mwanachuoni mtafiti wa Hanafi Ibn Al-Humaam, ametambua katika Fat-h Al-Qadiyr (1/306/ 359, 360) kwamba rai ya kuwa ni wajibu haikuthibiti kwa dalili na ni dhaifu. Na hivi ni katika kusahilisha mambo na sio kufanya magumu, kwani rai hii aliyoipa nguvu ni kinyume na madhehebu yake.

[3]   Ibn Abi Shaybah (12/41/1), Abu Daawuud, An-Nasaaiy katika Sunan Al-

Kubraa (218/1-2), Ahmad, At-Twabaraaniy, Al-Bayhaqiy na Ibn 'Aasakir (4/244/1) amesimulia hii pamoja na du'aa inayofuatia, ikiwa na isnaad Swahiyh. Ibn Mandah amesimulia du'aa katika Tawhiyd (70/2) pekee ikiwa na isnaad tofauti ya Hasan. Takhriyj yake imetolewa katika Al-Irwaa (426).

[4]  Ibn Khuzaymah (1/119/2) na pia Ibn Abi Shayah n.k kwa Hadiyth ya mwisho.

 

TANBIHI:

An-Nasaaiy ameongeza katika mwisho wa qunuut: ‘Wa Swalla Allaahu ‘alaan-Nabiyyil-Ummiyy’ (Allaah Amswalie Mtume asiyejua kusoma na kuandika), imesimuliwa ikiwa na isnaad Dhwa’iyf. Miongoni mwa waliokiri ni dhaifu ni Ibn Hajar Al-‘Asqalaaniy na Az-Zurqaaniy. Hivyo hatukuitia katika muundo wetu wa kuunganisha usimulizi unaokubalika. Al-‘Izz bin ‘Abdus-Salaam amesema katika Al-Fataawa (66/1/19): “Kumswalia Mjumbe wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) katika qunuut sio sahihi, wala haifai kuongeza kitu katika Swalah ya Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa vyovyote. Rai hii inaonyehsa kwamba hakuipanua kwa hoja ya kuingiza fikra ya bid’ah hasanah (uzushi mzuri) kama Maulamaa wa mwishoni wanavyodai.Lakini, imethibitika katika Hadiyth kuhusu ‘Ubayy bin Ka’ab akiswalisha watu katika Swalah za masiku ya Ramadhan kwamba alikuwa akimswalia Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) katika mwisho wa qunuut, na hii ilikuwa katika ukhalifa wa ‘Umar (رضي الله عنه), imesimuliwa na Ibn Khuzaymah katika Swahiyh yake (1097). Vile vile imethibitika kutoka kwa Abu Haliymah Mu’aadh Al-Answaariy ambaye alikuwa akiwaswalisha wakati wa ukhalifa wa ‘Umar – imesimuliwa na Ismaa’iyl Al-Qaadhwiy (Namba. 107) na wengineo, hivyo ziada hii imethibitika kutokana na desturi ya Salaf na hivyo haifai kuipa kauli kwamba ni bid’ah. Na Allaah Anajua zaidi.

Share