052-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Tashahhud Ya Mwisho Na Uwajibu Wake

 

Tashahhud Ya Mwisho

 

Wajibu Wa Tashahhud Hii

 

Kisha baada ya kumaliza Rak’ah ya nne, alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akikaa kwa ajili ya Tashahhud ya mwisho. Aliwaamrisha kuhusu hii na akifanya kama alivyofanya katika Tashahhud ya kwanza isipokuwa “alikaa mutawarrikan”([1])  “paja lake la kushoto likiwa ardhini na miguu yake yote miwili ikitokeza kutoka upande mmoja (yaani upande wa kulia)”([2]) “Aliweka mguu wake wa kushoto chini ya paja (la kulia) na muundi”([3]) “mguu wake wa kulia akiuinua”([4]) au mara nyingine “akiulaza pamoja ardhini”([5]) “paja lake la kushoto lilifunika goti lake (kushoto) akiliegemeza”([6])

 

Ameweka mfano wa kumswalia yeye (صلى الله عليه وآله وسلم) katika Tashahhud, kama Tashahhud ya kwanza. Njia za kumswalia (صلى الله عليه وآله وسلم) zimetajwa kabla katika sehemu yake.

 [1]  Al-Bukhaariy.

[2] Kifungu kile kile kilichotajwa hapo mbeleni. Ama katika Swalah ya rakaa mbili kama Alfajiri, Sunnah ni kukaa muftarishan. Tofauti hii imeelezewa kirefu kutoka kwa Imaam Ahmad katika Masaail ya Ibn Haaniy kutoka kwa Imaam Ahmad (Uk. 79)

[3]  Abu Daawuud na Al-Bayhaqiy ikiwa na isnaad Swahiyh.

[4]  Muslim na Abu ‘Awaanah.

[5]  Kifungu kile kile kilichotajwa hapo mbeleni

[6]  Kifungu kile kile kilichotajwa hapo mbeleni

Share