Anaweza Kuwamiliki Majini Na Kuwaamrisha Atakavyo?

SWALI:

 

Assalam alikum warhmatu Allaahu taala wabarakatuh.

 

Kuna kitu chochote binadamu anaweza kufanya ili majini wake wamuogope na kumfanyia vitu anavyovitaka? Ahsante


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Shukrani kwa swali lako kuhusu kuweza kuwamiliki majini na kuwaamrisha.

 

Hilo linawezekana kwani Allaah Aliyetukuka Amewapatia uwezo wanaadamu juu ya viumbe wengine vyote.

 

Hata hivyo, utumiaji huo unakuwa ni wa pande mbili, yaani nipa nikupe. Yeye atakutumikia nawe ni lazima ufuate yale yake ayatakayo ambayo yanamuingiza mmoja wetu katika ushirikina na ukafiri.

 

Hivyo, pamoja na kuwezekana jambo hilo, lakini si jambo ambalo Muislamu anapaswa kulifanya au kujifunza. Na haifai kushirikiana na watu wanaojihusisha na mambo kama hayo.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share