Anataka Kujiajiri Mwenyewe Lakini Hana Mtaji

SWALI:

 

assalam aleykum

 

Asante kwa alhidaya kutuwekea website nzuri yenye mafundisho.

 

naomba muniambie kama nahitaji kujiajiri mwenyewe lakini sina mtaji nifanye nini? Mimi nimeajiriwa lakini mshahara una isha wote sina hata akiba. Naomba ushauri. wabillahi tawfiq


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Shukrani kwa swali lako kuhusu mashauri ya kutaka kujiajiri.

Kama ulivyosema kujiajiri kunatakwia mtaji ambao utakusaidia kuweza kufanya shughuli au kazi unayoona itakukimu kimaisha. Zipo njia nyingi za kufuatwa ili kufikia hilo kutegemea na nchi unayoishi. Nazo ni kama zifuatazo:

 

1.      Kupata mkopo kutoka kwa jamaa, marafiki au rafiki, taasisi za Kiislamu, benki ya Kiislamu au njia nyengine yoyote ambayo haina ribaa.

 

2.      Kushirikiana na mtu mwengine au taasisi ambaye/ ambaye inaweza kukupatia mtaji na faida mnayopata mgawane kulingana na mlivyoafikiana. Kumaanisha wewe utatumia wakati wako na nguvu na mwengine atatoa pesa za shughuli hiyo.

 

3.      Kutafuta kazi nyengine ambayo mshahara wake haujambo ili uweze kuweka akiba ambayo itakuwa mtaji wa kuanza shughuli yako mwenyewe.

 

Katika kutafuta mtaji, jiweke karibu na Allaah Aliyetukuka kwa kufanya ‘Ibaadah na kumuomba aufanye mtaji huo kuwa wa kheri.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share