Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Anashabihiyana Vipi Na Nabiy Muusa (عليه السلام)?

SWALI:

 

In which aspects does Prophet Muhammad resemble Prophet Moses?

 


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Shukrani zetu kwa swali lako kuhusu kufanana baina ya Manabii wawili, Nabii Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Nabii Muusa (‘Alayhis Salaam).

Manabii hawa wawili wanafanana katika mambo yafuatayo:

 

1-      Wote walioa zaidi ya mke mmoja na kupata watoto.

 

2-      Wote ni Uwlul-‘Azm.

 

3-Wote walikataliwa na watu wao kisha wakawa ni wenye kukubaliwa na 3-kufuatwa.

 

4-Wote waliletewa shari’ah mpya kutoka kwa Allaah Aliyetukuka.

 

5-Wote waliwashinda maadui zao katika vita.

 

6-Wote walihama kutoka katika miji yao waliyozaliwa.

 

7-Wametoka katika kizazi cha Nabii Ibraahiym (‘Alayhis Salaam).

 

8-Walikufa kifo cha kawaida na kuzikwa.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share