Kuku Wa Karai Na Viazi (Pakistani)

Kuku Wa Karai Na Viazi (Pakistani)

   

Vipimo 

Kuku - 1 mkubwa 

Mafuta ya kukaangia viazi - kiasi 

Kotmiri iliyokatwakatwa-  2 misongo (bunches)

Methi/fenugreek seeds/uwatu - ¼ kijiko cha chai

Haldi/tumeric/bizari ya manjano -  ½ kijiko cha chai 

Jiyra/cummin/uzile/bizari ya pilau - 1 kijiko cha chai 

Kitunguu saumu(thomu/galic) - 7 chembe 

Viazi/mbatata - 3

Nyanya/tungule-  6 - 7

Tangawizi mbichi -  1 kipande kiasi 

Pilipili mbichi iliyosagwa- 1 kijiko cha chai 

Ndimu -  1

Chumvi - kiasi

Mafuta ya kupikia -  ¼ kikombe

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

 

  1. Mkate kuku vipande vipande vya kiasi. Mwoshe vizuri kwa chumvi na siki atoke harufu mbayaa.
  2. Menya viazi/mbatata kisha katakata vipande vipande vya mraba (cubes)
  3. Katakata nyanya ndogondogo (chopped), Chuna tangawizi mbichi na kitunguu thomu, katakata kotimiri (chopped) weka kando.
  4. Weka mafuta katika karai, kaanga viazi/mbatata hadi viive kisha epua vichuje mafuta.  Weka mafuta kando.
  5. Weka mafuta ¼ kikombe katika karai weka katika moto yashike moto. Kisha tia tangawizi mbichi, kitunguu thomu, bizari zote.  Kakaanga haraka kidogo tu.
  6. Tia vipande vya kuku na kakaanga achanganyike na masala.
  7. Tia nyanya/tungule, chumvi, pilipili mbichi iliyosagwa endelea kukaanga na kufunika hadi kuku aive na itokee sosi ya nyanya.
  8. Tia ndimu, changanya, kisha mwagia viazi, changanya.
  9. Mwagia kotmiri ikiwa tayarii kuliwa kwa wali mweupe au aina yoyote ya mikate.

 

Share