Hedhi Haikujitokeza Kikamilifu Je, Swawm Inafaa Siku Hiyo?

 

Hedhi Haikujitokeza Kikamilifu Je, Swawm Inafaa Siku Hiyo?

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Asalam alykum warahamatu lwah wabarakatu,

Swali: Nilikuwa tanaka kwenda kuswali Adhuhur, kabla ya hapo nilijicheck kwa sababu nilikua nategemea kupata period siku inayoofuata, baada ya kujilazimisha kujicheck kwa mbali sana niliona alama ya mbali ya brown kwenye tissue, nikaacha kuswaali na nikasema ikifika saa tisa nitajicheck tena kama sitoona kitu basi nitaenda kuswali na nilifanya hivyo mpaka nikamaliza kuswali tarawehe sijaona kitu tena na ilipofika usiku saa 8 niliamka kutaka kwenda kuswali sasa nikaona damu. Naomba mnifahamishe vipi swaum yangu kwa siku ile na swala nilizoswali?

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.  

 

Kwa vile ulikuwa unategemea kuwa siku zako ziko karibu, kisha ukapata damu siku hiyo, basi hiyo siku itahesabika kuwa ni siku ya hedhi. Inavyoelekea ni kuwa haikutoka damu sawa sawa tu, lakini ishara zake tayari zilikuweko.

 

Kwa hiyo itabidi uilipe siku hiyo na Swalaah ikiwa umeziswali basi huna la kufanya, kwani mwanamke hatakiwi kulipa Swalaah ila anatakiwa alipe Swawm pekee.

 

 

Na Allah Anajua zaidi

 

 

Share