Mpunga Wa Nazi Kwa Mchuzi Wa Samaki Na Rojo La Bilingani Na Viazi/Mbatata

Mpunga Wa Nazi Kwa Mchuzi Wa Samaki Na Rojo La Bilingani Na Viazi/Mbatata

 

Wali Wa Nazi

Mpunga - 4 vikombe                                   

Tui la nazi - 6 vikombe

Chumvi - Kiasi          

                                                               

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Osha mchele kisha
  2. Bandika tui jikoni likichemka tia mchele na chumvi.
  3. Funika uchemke,  tui likikauka wacha moto mdogomdogo hadi wali uive ukiwa tayari. Ikiwa unatumia mkaa unapalia juu yake. 

Mchuzi Wa Samaki Nguru

Samaki - 4 

Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi - 2 viijiko vya supu

Kitunguu maji kilokatwakawa - 2 slice ndogo                                  

Nyanya/tungule - 4

Nyanya kopo - 3 vijiko vya supu

Pilipili mbichi - 2

Kotmiri ilokatwakatwa - 3 msongo  (bunches)

Bizari ya mchuzi (simba 2) - I kijiko cha chai

Ndimu - 1 kamua

Mafuta - ¼ kikombe

Chumvi kiasi

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Katakata samaki mkaange kwa kumtia viungo.
  2. Weka mafuta katika sufuria, kaanga kitunguu. Vinapogeuka rangi thomu na tangawizi mbichi, nyanya, nyanya kopo, kitunguu na bizari ya mchuzi endelea kukaanga.
  3. Tia maji kiasi  na ndimu, pilipili mbichi ilosagwa kisha tia kotmiri.
  4. Mwisho tia nusu ya samaki  alokaangwa ukiwa tayari

Bilingani Za Kukaanga Na Viazi

Bilingani -  4 madogodogo

Viazi/mbatata - 3

Nyanya  -  3

Majani ya mchuzi/mvuje/curry leaves - kiasi 6-7

Nnyanya kopo -  2 vijiko vya supu

Methi/uwatu ulosagwa - 1 kijiko cha chia

Rai/mustard seeds - 1 kijiko cha supu

Bizari ya manjano/haldi/turmeric - 1 kijiko cha chai

Chumvi - kiasi

Mafuta ya kukaangia - kiasi

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

1.   Weka mafuta ya kukaangia katika karai

2.   Katakakata bilingani vipande vipande vya mraba (cubes) kaanga katika mafuta ya moto hadi yageuke rangi. Eupa weka kando.

3.   Katakataka viazi/mbatata vipande vidogodogo vya mraba (cubes) Kaanga hadi viive epua weka kando.

4.   Ondosha mafuta yote katika karai bakisha kidogo tu kiasi ya vijiko 2 vya supu.

5.   Kaanga rai kisha majani ya mchuzi, na methi/uwatu kisha kaanga nyanya.

6.   Tia nyanya ya kopo kisha changanya pamoja bilingani na viazi ikiwa tayari.

 

 

Share