Juisi Ya Embe Na Karakara/Pasheni (Passion Fruit)

Juisi Ya Embe Na Karakara/Pasheni

 

Vipimo

Passion fruit - 8

Embe - 6 za kiasi

Maji - kiasi

Sukari - kiasi upendavyo

 

Namna Ya Kutyarisha

  1. Kata passion fruit toa nyama weka mashine ya kusagia (blender) . Tia maji kiasi kisha saga na uchuje .
  2. Saga embe na maji kidogo kisha changanya na juisi ya passion.
  3. Tia sukari korogo  ikiwa tayari.

 

Share