Maziwa Ya Lozi Ya Hiliki

Maziwa Ya Lozi Ya Hiliki

 

 

Vipimo

 

 

Maziwa freshi – lita 1 na ½

Maziwa mazito (condensed milk) ½ kikombe

Lozi  -  ½  kikombe

Hiliki – ¼ kijiko

Asali au sukari - ukipenda kuongezea utamu

 

 

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika   

 

  1. Tia maji ya moto katika kibakuli uroweke lozi. Kisha zimenye na zikatekate slaisi.
  2. Weka maziwa kidogo na lozi kiasi katika mashine ya kusagia usage.
  3. Chemsha maziwa pamoja na hiliki kisha mimina maziwa ulosaga na lozi.
  4. Changanya na maziwa mazito ukoroge.
  5. Epua umimine katika vikombe au gilasi. Nyunyizia lozi zolobakia
  6. Kolezea asali au sukari ikiwa tayari. Kunywa upendavyo moto au ikiwa unapenda baridi weka katika friji.

 

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

 

 

 

 

 

 

Share