Pilau Ya Kuku Kwa Mchele Wa Mbeya

Pilau Ya Kuku Kwa Mchele Wa Mbeya

 

 

Vipimo

Mchele wa mbeya unaonukia - 1 kilo

Kuku - 1

Vitunguu - 3

Viazi/mbatata - 5

Jira/bizari ya pilau nzima - 3 vijiko vya supu

Mdalasini - 1 kijiti

Pilipili manga - 1 kijiko cha supu

Hiliki - 3 chembe

Karafuu - 5 chembe

Kitunguu saumu(thomu/galic) kilosagwa - 3 vijiko vya supu

Tangawizi mbichi ilosagwa - 3 vijiko vya supu

Mafuta ya kupikia - ½ kikombe

Chumvi - kiasi

 

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Baada ya kumsafisha kuku na kumkatakata, mchemshe kwa chumvi na ndimu, kijiko kimoja cha kitunguu thomu/somu na tangawizi yote..
  2. Menya viazi, katakata vipande vya kiasi.
  3. Katakata vitunguu maji kisha kaanga kwa mafuta katika sufuria ya kupikia pilau.
  4. Tia bizari zote isipokuwa hiliki.
  5. Saga hiliki kisha tia pamoja na kitunguu thomu/somu ukaange kidogo.
  6. Mimina kuku na supu yake ikichemka kisha tia mchele na viazi.
  7. Koroga kisha acha katika moto mdogomdogo wali uwive kama kawaida ya kupika pilau.

 

 

 

 

Share