Pilau Ya Nafaka Na Nyama Ya Kusaga

Pilau Ya Nafaka Ya Nyama Ya Kusaga

VIPIMO

Mchele  - 3 vikombe

Nyama ya kusaga -  1 LB

Mchanganyiko wa Nafaka upendazo; maharagwe, njegere, mbaazi n.k 1 mug 

Vitunguu maji  kata vipande vipande -  3 vya kiasi

Kitunguu saumu(thomu/galic) na Tangawizi - 2 vijiko vya supu

Mafuta - ½ Kikombe

Mchanganyiko wa bizari (Garam Masala) - 2 vijiko vya chai

Mraba ya supu ya nyama - vidonge 2, au supu yenyewe kiasi cha kutia ladha (hakikisha supu isizidi kipimo kwa kupunguza kipimo cha maji).

Maji (inategemea mchele) - 5

Chumvi  - Kiasi

 

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

 1. Osha mchele na roweka.
 2. Weka mafuta katika sufuria na kaanga vitunguu mpaka viwe brown.
 3. Tia Thomu na tangawizi, kaanga kidogo.
 4. Weka nyama ya kusaga, chumvi na garam masala, endelea kukaanga mpaka nyama iwive.
 5. Mwaga maji yaliomo katika kopo la nafaka na utie nafaka pekee humo.
 6. Tia maji  na  vipande vya supu (Maggi cubes) huku unavivuruga, koroga kidogo.
 7. Tia mchele, koroga kidogo.
 8. Funika na pika kwa moto mdogo mpaka karibu na kukauka ukikorogoka kidogo.  (kama unavyopika pilau ya kawaida)
 9. *Epua uipike katika moto wa oven 350-400  Deg kwa muda wa dakika  15. 
 10. *Kama sufuria uliyotumia sio ya kupikia katika oven, mimina katika chombo chochote kinachotumika kwa oven kama bakuli la  pyrex au treya za  foil.
 11. Pakua katika sahani na iko tayari kuliwa.

 

 

Share