Wali Wa Sosi Ya Samaki Tuna Na Viazi

Wali Wa Sosi Ya Samaki Tuna Na Viazi

 

 

Vipimo:

               

Sosi Ya Tuna

 

Tuna (samaki/jodari) -  2 Vikopo

Vitunguu (kata kata)  - 3

Nyanya katakata - 3

Viazi (vilivyokatwa vipande vidogo - cubes)  -  4

Mchanganyiko wa bizari - 1 kijiko cha supu

Chumvi    -  kiasi

Kidonge cha  supu – 1 

 

Wali:
 

Mchele  -    3 Vikombe vikubwa (Mugs)

Mdalasini -  1 kijiti

Karafuu -  chembe 5

Zaafarani kiasi roweka

Chumvi kiasi

 

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika 

 

 1. Kosha mchele roweka kidogo.
 2. Kaanga viazi hadi viwive, epua chuja mafuta.
 3. Kaanga vitunguu hadi viwe rangi ya hudhurungi (brown).
 4. Tia nyanya kaanga, kisha tia bizari ukaange kidogo.
 5. Weka kidonge cha supu katika kibakuli kidogo tia maji ya moto kikombe kidogo cha kahawa uchanganye.
 6. Changanya supu katika sosi ulokaanga.
 7. Tia viazi changanya, Pamoja na vipande vya samaki tuna.  
 8. Chemsha mchele pamoja na mdalasini na karafuu.
 9. Karibu na kuwiva, chuja maji kisha mwagia katika sosi ya tuna.
 10. Nyunyizia zaafarani kisha funika upike moto mdogo mdogo kama unavyopika biriani.
 11. Pakua katika sahani ulie kwa saladi upendayo
 12.  

 

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kuburudika)

 

 

Share