Chila - 2

Chila  - 2

 

Vipimo

 

Mchele  vikombe 2

                                                         

Sukari  kikombe 1

                            

Tui la nazi zito vikombe 2 na nusu

 

Hamira 1 kijiko cha chai

 

Hiliki nusu kijiko cha chai

  

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

 

  1. Osha mchele kisha urowanishe kwa masaa mengi.
  2. Tia katika mashine ya kusagia (blender). Tia sukari, hamira, hiliki.
  3. Tia tui la nazi kidogo tu kwanza ili usage mchele hadi uwe laini kabisa.
  4. Maliza kutia tui lote kisha mimina katika bakuli uache uumuke.
  5. Choma/pika katika chuma kisichoganda (non-stick frying pan) 
  6. Kupika kwake ni kumimina mchoto mmoja wa upawa na kutandaza katika chuma.
  7. Kisha unasubiri hadi ufanye matundu, ukauke na kuwiva chini.
  8. Unaepua na kuweka katika sahani, mmoja juu ya mweziwe upande mweupe uwe juu.

 

Share