Kumuozesha Mtoto Wa Kiume Kwa Mtoto Wa Mke Wa Pili Inafaa?

 

SWALI:

Assalaam alaykum Sheikh.

Tafadhali naomba majibu ya jambo hili kwa haraka, Ishaallah!!!

Kuna Jamaa kamuozesha mwanae mwanamme kwa mtoto wa mkewe ambae wakati anamwoa huyu mke tayari alikuwa na huyu mtoto wa umri wa miezi tisa (anaeyenyonya) kutoka kwa mume wake wa mwanzo ambae waliachana.Pia huyu mke alishika mimba kwa huyu mume bila kujua aliendelea kumnyonyesha mwanae huyu kwa muda ndipo alipomwachisha.Vile vile mtoto huyu aliendelea kulelewa pamoja na watoto wengine wa mumewe na aliyezaa nae hadi wamekuwa. Je ndoa hii ni halali, ingawa idhini kutoka kwa Baba wa mtoto ilipatikana.


 

JIBU:

Shukran kwa swali hili zuri. Hakika mas-ala yote katika Uislamu yameelewa kiukamilifu, hivyo kuondoa aina yoyote ya utata au mushkeli. Na ndoa pia inaingia katika msingi huo wa Dini. Uislamu umeeleza wazi ni nani anaweza kuolewa na nani na nani hawezi kumuoa. Unaweza kuangalia Suratun Nisaa’ (4): aya 22 – 24 kwa wanawake ambao huwezi kuwao na tayari tuliwataja katika swali lingine. Unaweza kuangalia jibu hilo katika tovuti hii ya Al-hidaaya  tazama swali la : 'NDOA YENYE UHUSIANO'  katika kitengu cha NIKAAH (NDOA).

Katika swali ulilouliza Uislamu haujakataza ndoa hiyo, na hiyo nikaha yao ni sahihi kabisa na haina tatizo lolote. ikiwa kunyonya unamaanisha kuwa huyo bwana harusi na bibi harusi walinyonyeshwa na mama mmoja basi hiyo harusi itakuwa batili.

Kawaida katika ndoa idhini inatoka kwa baba wa msichana (bibi harusi) na wala sio baba wa mtoto (wa kiume). Ikiwa baba hayupo basi walii wake kwa upande wa kuumeni kwake.

Na Allah Anajua zaidi.

 

 

Share