Wakati Maalumu Wa Kitendo Cha Ndoa?

 

SWALI: 

Assalaama alaykum, naomba jawabu kama kuna wakati maalum na siku maalum au mchana au usiku kumeelezwa kuwa bora katika kufanya kitendo cha kujaamiiana kati ya mume na mke katika mafundisho ya uislamu na kama kuna siku ama makruh au haramu na kama kuna maelezo yanayoshauri kufanya kitendo hicho. Kwani kuna misemo kama hiyo inatembea katika baadhi ya mitandao lakini nahofia huenda sio ya kiislamu thabiti
Shukran



 

JIBU: 

Sifa zote njema Anastahiki Allah Mtukufu, Swalah na salamu zimfikie kipenzi chetu, Mtume Muhammad (s.a.w.w.), Ahli zake na Maswahaba zake (r.a.) na Watangu Wema na waliowafuata kwa kheri mpaka Siku ya Kiyama. 

Shukrani kwa swali hilo lenu kuhusu wakati unaofaa wa tendo la ndoa baina ya mume na mke.

Kwa hakika hakuna wakati maalumu uliowekwa kwa ajili ya kustarehe baina ya wanandoa. Wakati wowote ambao mutakuwa muko tayari munaweza kukutana, mchana au usiku, Jumamosi, Jumatatu au siku nyingine yoyote.

Na kwa hakika Mtume (s.a.w.w.) amewahimiza wake wawe ni wenye kuwatekelezea waume zao haja hiyo ya kindoa hata kama mwanamke alikuwa akipika, aache na amtimizie mumewe matamanio yake.

Na ameeleza ikiwa mwanaume ametoka nje ya nyumba na akakutana na mwanamke na akavutiwa naye sana  basi arudi haraka kwa mkewe ili apate kumtosheleza na hivyo kuondoa ile dhamira mbaya moyoni mwake.

Na Allah Anajua zaidi.

 

Share