Ana Matatizo Ya Kutomridhisha Mkewe Kwenye Tendo La Ndoa

 

SWALI:

 

Aaww. NAOMBA MNISAIDIE MIMI NINA NDOA YAPATA MIEZI 4 SASA ILA NIA TATIZO LA KUWAHI KUFKA KILELENI NA MKE WANGU LINA MCHUKIZA .LICHA YA KUFANYA YOTE YA KUMWANDAA NA KILA KTU BADO HANA RAHA NA SASA HATAKI KUFANYA TENDO HILO NA MIMI JE ANAHAKI HIYO?  NA MIMI PIA NINA HAKI GANI? JE TUACHANE SASA? NA DAWA NINI HASA YA TATTIZO HILI? NAOMBA MSAADA MKUBWA NIA UMRI WA MIKA 24 TU. (tutawasialan kupitia ******** nisaidien juu ya hili kuokoa ndoa hii naona sasa ndoa  ni dhuruba ya matatizo tuuu!!!!!

AAWW

NAOMBA KUULIZA JE MIMI KAMA MWANAUME MKE WANGU NAJARIBU KUMBEMBELEZA KWA NAMNA ZOTE NA BDO HATAKI  KUINGILIANA NAMI NIFANYEJE HII IMEKUJA TUU KWA SABABU  NINA TATIZO LA KUWAHI KUFIKA KILELENI KABLA YAKE NIMEFUATA MAFUNDISHO YENU NINAMFANYIA KILA KITU LAKIN HATIMAYE SASA HATAKI HATA KULALA NAMI  HATA NIKIMWAMBIA NJOO HATAKI JE NIMWACHE SASA? JAMANI NAHISI IKIFANYA HILI LA MWAISHO NARUDIN KWENYE ZINZAA ISYO KIFANI. NAOMBA MNISAIDIE HARAKA IWEZEKANAVYO KWA KUZINGATIA NIMEWATOA HOFU VIJANA WENGI NA SASA WAPO MBIONI NAO KUFANYA JAMBO KAMA LANGU LA NDOA NA KUACHANA NA ZINAA HUKU TULIPO.

JE MWANAMKE ANAYO HAKI YA KUKATAA KUINGILIWA NA MUME WAKE IKWA TUU ETI MUME ANATATIZO LA KUWAHI KUFIKA KILELENI? NA MWAMUME HUYU ANAJITAHIDI KUMTAYARISHA IPASAVYOO ILA KE HATAKI KABISAAA NINI LA KUFANYA.

 


 

 

JIBU: 

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho. 

 

Shukrani kwa swali lako kuhusu tatizo ulilonalo na ndoa na mkeo.

 

Katika mas-ala ya wanandoa kustarehe na mwenziwe haifai kwa mume kumkatalia mkewe na kinyume chake. Na ikiwa mke atakataa kumstarehesha mumewe, na mume akalala akiwa amekasirika basi mke analaaniwa na kila kiumbe mpaka mume amridhie. Kwa hiyo, si haki kwa mkeo kukataa kukustarehesha kwa sababu una tatizo. 

 

Huenda ikawa anaumia na anapata machungu lakini kukiwa na tatizo ni muhimu kwa wanandoa kusaidiana ili kufikia suluhisho muafaka. Katika kutatua tatizo hilo inabidi wewe na mkeo mkae kitako kama wanandoa na kutazama ni njia gani mnaweza kutumia ili mpate suluhisho na muishi kwa wema na uzuri. Mke ni muhimu akusaidie ili kila mmoja aridhike. Kwa ajili hiyo, inafaa mkeo apewe ushauri nasaha kuhusiana na hilo. 

 

Pili kuna haja kubwa sana kwako kwenda kwa daktari au twabibu ili upate dawa kwani huo ni ugonjwa. Na hakika ni kuwa Allaah Aliyetukuka hakuteremsha ugonjwa isipokuwa Ameleta na dawa yake. Hivyo, tafuta dawa kuhusiana na tatizo lako hilo.

 

Tafadhali bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi:

Mume Ana Tatizo La Kumaliza Kabla Ya Mkewe Kwenye Tendo La Ndoa

Ikiwa Hawaridhiani Katika Kitendo Cha Ndoa Wafanye Nini? 

Mume Hamtoshelezei Matamanio Yake Ya Tendo La Ndoa, Anaomba Ushauri

 

Na Allaah Anajua zaidi

Share