Chow Mein Za Kuku Pilipili Boga Mahindi (Guyana)

Chow Mein Za Kuku  Pilipili Boga Mahindi (Guyana)

Vipimo na namna ya kutayarisha

Tambi nene Chambua katakata -  500 gms

Kuku bila mifupa (kidari) Katakata vipande vipande - 1 Lb/ ½ Kilo

Mahindi Chambua  - 1 kikombe

Pilipili boga jekundu (capsicum)Katakata - 1

Pilipili boga la orengi Katakata – 1

Tangawizi mbichi kuna (grate) - 1 kijiko cha supu

Kitunguu saumu (thomu) kuna (grate) - 1 kijiko cha supu

Pilipil manga ya unga -  1 kijiko cha chai

Mdalasini wa unga - ½ kijiko cha chai

Bizari manjano/haldi/tumeric  - 1 kijiko cha chai

Sosi ya soya (soy sauce) - 2 vijiko vya supu

Chumvi  - Kisia 

Mafuta - ¼ kikombe

Namna Ya Kupika:

  1. Chemsha tambi, ziwive kiasi, mwaga maji, chuja. Tia siagi ili zisigandane.
  2. Chemsha chembe za  mahindi kidogo tu kiasi ya kuivisha. Mwaga maji chuja.
  3. Weka mafuta katika karai, pasha moto, kisha tia tangawizi mbichi na kitunguu thomu kaanga kidogo tu, kisha  haraka tia kuku, sosi ya soya,  bizari, pilipili manga, chumvi.
  4. Funika kuku awive huku unafungua kumkaanga.
  5. Karibu na kuwiva tia pilipili boga na mahindi.
  6. Tia tambi changanya vizuri kisha pakua katika chombo.

Picha za aina ya tambi zinapatikana katika viungo vifuatavyo:

 

Chow Mein (Tambi Nene Za Kukaanga) Za Nyama Kusaga Na Mboga Mchanganyiko

 

Chow Mein (Tambi Nene Za Kukaanga) Za Kamba Na Mboga Mchanganyiko

 

 

 

Share